Nakwenda Hijja Inshallah | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nakwenda Hijja Inshallah

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by HM Hafif, Oct 20, 2009.

 1. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wana JF.

  Kama kuna watu walikuwa wanasikia tetesi basi leo napenda kuweka bayana kuwa Mimi Hamad Moh'd Hafif Al- Mugheiry na wake zangu wawili Bi Kuruthum Suleiman Al yahayai na Bi Zelekha Khamis Al Harthy na bint yangu Mpenda Dr Mufiydat Hamad Al Mugheiry sote kwa pamoja tunasafiri kwenda kwenye mji mtakatifu wa Makkah na Madinna kwa ajili ya kuhirimia Hijja.

  Kama ilivyo addah kuwa yeyote anaekwenda huko basi ni sharti pamoja na kuhakikisha kuwa wale wote wanaomtegemea kuwa hawata pata taabu kipindi yeye hayupo lakini pia unatakiwa uwaage ndugu, jamaa na marafiki wote na kupata radhwi zao.

  Na mimi kwa niaba ya familia yangu nawaaga rasmi kuwa nakwenda hijja tarehe 10 Nov 2009 kwa yemen air na baada ya Ibada ya hijja nitakwenda kusalimia jamaa huko Muscat na Yemen na insh'Allah nataraji kurudi Tanzania mwishoni mwa December.

  Nawatakia kila la kheir na naomba dua zenu katika safari yangu hiyo. Tuwiane radhi kwa niliowakosea na nimewawia radhi walionikosea.

  Nawatakia barza njema
   
 2. October

  October JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuwa makini tu wakati 'wanapomponda shetwani' wasije wakakuponda na wewe
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Oct 20, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  “Ewe Mwenyezi Mungu Muongoze mja wako huyu na familia yake, pamoja na Uliowaongoza, na Umpe afya njema yeye na familia yake, pamoja na Uliowapa afya njema, na Mfanye kuwa ni kipenzi chako yeye na familia yake pamoja na Uliowafanya wapenzi na umbariki katika katika safari yake hiyo tukufu, Hakika ameitikia wito wako pamoja na hao walio itikia kabla, basi zikubali dua zake na zetu pamoja na familia zetu… Mbariki katika Ulichompa na mkinge na shari ya Ulilolihukumu kwani Wewe Unahukumu wala Huhukumiwi. Hakika hadhaliliki Uliyemfanya mpenzi (wala hatukuki Uliyemfanya adui) Umetakasika Ewe Mola wetu na Umetukuka, basi tuwezeshe na sisi tuweze kuitikia wito wako mtukufu, ili nasi tuweze kwenda kwenye nyumba yako tukufu…" Amin Insha'Allah


  “Ewe Mwenyezi Mungu, Wewe tu Ndiye tunaekuabudu, na Kwako tunaswali na tunasujudu, na Kwako tunakimbilia na tunakutumikia, tunataraji rehema Yako na tunaogopa adhabu Yako, kwani adhabu Yako hakuna shaka kuwa makafiri itawifikia. Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakutaka msaada na tunakutaka msamaha na tunakusifu kwa kheri na wala hatukukufurishi na tunakuamini Wewe, na tunakunyenyekea na tunamuepuka anaekukufuru”

  Subhaanal-Malikul-Qudduus
  Subhaanal-Malikul-Qudduus
  Subhaanal-Malikul-Qudduus  Rabbul-Malaaikati War-Ruuh

  Tunakutakia safari njema Insha'Allah

  X-Paster
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Shukurani sana kwa kunihadharisha. lakini hii ni mara ya Pili kwenda hijja.
   
 5. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aamin Yarabbi Aamin.

  Allah atuongoze
   
 6. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,984
  Likes Received: 1,554
  Trophy Points: 280
  Tunawaombea nyinyi na wote waliokwenda na wataokwenda, hijja maqbul

  mola awape afya ya kutekeleza yote yaliyoamrishwa katika safari hii na mwende na kurudi kwa salama .
  Musitusahau na sisi kwa dua tu inshaallah
   
 7. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=7BAxDzUCl8M"]http://www.youtube.com/watch?v=7BAxDzUCl8M[/ame]
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  HM Hafif,
  Mw'mungu awajaalie kheri ww na watu wako...na waislamu wote mnaolekea huko kwa ibada hii tukufu...mwende na mrudi salama salimini...Mkuu usisahau dua kwa Qudsi na Falastine...na waislamu wote wanaishai katika dhulma...again, nakutakia safari na hija yenye kukubaliwa ww na watu wako na waislamu wote wanaoelekea huko.
   
 9. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Safiri salama, na bwana akutangulie........
   
 10. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Inshallah, Mungu akusaidie na hijja yako pamoja na za wake zako na mwanao zikubaliwe pamoja na hao wote watakaoenda huko. Tuombee na sisi tuliyokutakia heri Mungu atukumbuke mambo yetu mema yawe rahisi. Ibada njema!
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  marhaba yaa Al Mugheiry.

  Awali ya yote kwanza nakupongeza sana kwa kutekeleza sunna ya Rasul Mohammad S.A.W kwa kuoa wake WAWILI. na kwa taarifa yako mkeo Zulekha ni mtoto wa Binamu yangu Sheikh Khamis Fahad Al Harthy, ambaye baba yake Mzee Fahad Saleem Al Harthy ni ndugu na Sheikh Abdullah Saleem Al harthy na Mama Yangu mzazi Bi Faharataji Saleem Al Harthy. Wote hao wanatoka RUWI, Muscat Oman. Na huko Unguja ni wazawa wa Kianga, Mwera , Zanzibar.

  Pili nakupongeza kwa kuitika wito wewe pamoja na jamii yako. {Rabbaikkah). nawaombea kwa Allah awarahisishie safari na muweze kutimiza Hijja zenu salama usalimin na Hijja zenu ziwe zenye kukubaliwa.

  Mwisho tumekusamehe na tumekubali msamaha wako. Tunaamini kuwa ukirudi huko basi utakuwa umefungua ukurasa mpya wa maisha. Lakini tu usisahau kumtoa Askofu Abdulhalim katika blacklist yako ili nae awe huru kuchat nawe.

  Tafadhali ukiwa huku basi tuwasiliane ufike japo hapa Qatar na insh'Allah gharama za ticket na jamii yako nitalipa. tafadhali sana karibu Doha.
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Al haj Hafif.

  Vipi huyu Binti yako Dr Mufiyda ameshapata mchumba? Nina barubaru moja hapa linatafute mke kutoka huko. Yeye ni Mhandisi hapa Qatar Petrolium aitwa Saleh said Al Namaan.i
   
 13. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Baba nakushukuru sana. Kwa hakika nimefurahi mno kujuana kwani hata wifu anamjua sana huyo Bibi yake tokea akiwa Pale Kariakoo Mkunguni Str na mpaka sasa pale Sahadhabi Muscat.

  Tutafurahi sana kukuona ee na familia yako yote Muscat kwani lazima tufika Al Kheir kwa Engineer mstaafu Sheikh Abdullah. Tuonane pale.

  Kwa kifupi nimemwacha huru na nimewasamehe AbdulHalim na wengine wote waliokuwa kwenye black list yangu .
   
 14. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Baba huyu Mjukuu wako ameshaposwa tayari lakini mengi tutaongea tukionana inshallah.


  Nawashukuru wote kwa dua zenu. nami Inshallah nitawakumbuka kwenye dua zangu na inshallah Allah atawafanyia wepesi katika shughuli zenu, atawaepusha na mabalaa na sheitwani kuwapa baraka na kheir nyingi.
   
 15. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Uiombee nchi yetu ili Mafisadi walaniwe na wakome kuchukua kile ambacho Mwenyezi Mungu ametujaaalia. Ishallah utarudi salama
   
 16. I

  Iddi Rajab Member

  #16
  Oct 21, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Allah akufanyieni wepesi katika Safari yenu na Ibada yote kwa Ujumla wenu na wengine wote waliokusudia kwenda Hijja Allah kwa Huruma yake nao pia awarahisishie Safari zao INSHALLAH.
   
 17. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana, Allah atuzidishie kheir kwa wingi na kutuokoa na maovu.
   
 18. M

  Mandago JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 238
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Nakutakieni safari njema Inshallah, Amin.

  Utakapo fika katika Al-Kaaba usinisahau na mimi katika dua zako.
   
 19. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inshallah wote nitawaombea
   
 20. r

  remyshas Member

  #20
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenyesi mungu akufikishe salama na ailinde familia yako kipindi ulioiacha hapa nyumbani kipindi hayupo.tuombee na sie waislam wenine mwenyezi mungu atuoe rizq tupate kutimiza hiyo nguzoameen.
   
Loading...