Nakutana na wakwe siku za usoni: Wakongwe, naomba tips.

The Alchemist

Senior Member
Jun 15, 2016
177
148
Habari wadau wa JF.

Mdau mwenzenu nadhani nimefikia tamati ya ujana. Niko na mwenza ambaye kiukweli, anatarajia kuwa mama watoto mwaka huu.

Kwa kipindi changu chote cha mahusiano karibu miaka 10 na wanawake tofauti, skuwai kukutana na wazazi wa yeyote. Skuwai kuwa na ilo wazo. Skuwai kushawishika. Sikuwa kuwa na iyo motivation.

Kwa sasa niko na mwenza ambaye tulikutana miaka mitatu nyuma. Miaka miwili ya urafiki. Mmoja wa uchumba. In short, nimeanza zoezi la urasimishaji na linanza kwa wakwe.

Nategemea kuanza kukutana na wakwe, then zoezi la mahari na washenga na utaratibu mzima nadhani utanzia apo. Ni zaidi ya NIDA kiukweli na kwa watu rebellious wa formality kama mimi ni shida isiyoepykika.

Mimi binafsi sio muumini sana wa hizi formality, natamani ingekuwa ni mimi nayeye, na short cut kama ingewezekana. Ila ndoa, uku kwetu si yako tuu na hivyo sina budi.

Naombeni tips, kwa wale waliobahatika kufanya ili zoezi, za namna ya kufanya, kuongea, kubehave, kucheka wakati gani n.k.
Nini kuvaa, kutokuvaa etc.

Asanteni.
 
Omba upate mama mkwe poa kama wangu, utaenjoy maisha sana.

Pia omba wanafamilia wenzake wasiwe na mambo ya kiswahili(much know nyingi), utaenjoy sana.

Pia omba ukoo/familia yake iwe ni ile wenye mashirikiano ya hali na mali, utaenjoy sana.

La mwisho omba baba mkwe awe mwenye maono chanya kuhusiana na mahari, asiwe yule mwenye maono ya kutajirikia kwenye mahari, utaenjoy sana.

Unforgetable
 
The Alchemist,
We uchumba mmeingia sa ngapi na unasema ujawai waona wakwe? Inamaana ujui mtu kuitwa uchumba ni hatua gani inafikia au ulimvalisha pete ufukweni tayari mkajiita wachumba! Kuhusu kucheka we chekacheka tu kama una mood nzuri watakuchukulia ivoivo
 
Mi sio muumini wa maombi sana.

Ila asante mdau wangu.

Omba upate mama mkwe poa kama wangu, utaenjoy maisha sana.

Pia omba wanafamilia wenzake wasiwe na mambo ya kiswahili(much know nyingi), utaenjoy sana.

Pia omba ukoo/familia yake iwe ni ile wenye mashirikiano ya hali na mali, utaenjoy sana.

La mwisho omba baba mkwe awe mwenye maono chanya kuhusiana na mahari, asiwe yule mwenye maono ya kutajirikia kwenye mahari, utaenjoy sana.

Unforgetable
 
Sjui neno equivalent na “dating” kwa kiswahili.

Nadhani siyo necessary uwe umekutana na wazazi kama mnadate.

We uchumba mmeingia sa ngapi na unasema ujawai waona wakwe? Inamaana ujui mtu kuitwa uchumba ni hatua gani inafikia au ulimvalisha pete ufukweni tayari mkajiita wachumba! Kuhusu kucheka we chekacheka tu kama una mood nzuri watakuchukulia ivoivo
 
Usiwe na nidhamu ya uoga na usijiamini saana kupita kiasi

Usiwe muongeaji saana kiasi cha kuonekana u-mjuaji

Vaa mavazi ya heshima na nadhifu (kuwa wewe)

Epuka hasira *baadhi ya wazazi huuliza maswali ya kukaraisha kwa lengo la kupima kiwango cha uvumilivu ulichonacho*
 
Asante sana mkuu.

Back
Top Bottom