Nakusudia kumshitaki Abdallah Bulembo (Mb) kwa kumnadi Magufuli 2015

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,021
2,000
Bulembo ndiye aliyekuwa meneja wa JPM ktk kampeni za kuwania urais 2015. Alizunguka nchi nzima kuwaaminisha watanzania kuwa huyu ndiye bora zaidi ya wagombea urais wengine.

Lkn mambo yamekuwa kinyume kabisa na matarajio ya wengi. Nani alaumiwe? Ni Abdallah Bulembo aliyetuongopea. Lkn yy alizawadiwa ubunge wa kuteuliwa.

Anastahili kushitakiwa kwa "kufanya utapeli wa uaminifu wa kisiasa kwa watanzania". Alitutapeli kisiasa, tukamwamini. .

Mtu aliye mnadi amelipelekea taifa kuingia ktk matatizo makubwa yafuatayo:-
*biashara zinakufa
*watu wanatekwa na kupotezwa hovyo
*watu wanashambuliwa kwa risasi mchana kweupe
*uhasama na chuki za kiitikadi vimepandikizwa na kuwa sehemu ya utamaduni wa mtanzania
* mazao ya mimea na mifugo yanakosa soko
*demokrasia na Uhuru wa kujieleza vyote vimebinywa.
*wavuvi wanaporwa zana zao na kupigwa kama wezi.
n.k
Kwa haya na mengine mengi nakusudia kumburuza Abdallah Bulembo mahakamani kwasabb mwenye kuyatenda ana kinga. Na kwa msaada wa wanasheria nitashinda.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
80,248
2,000
Hiyo kesi ina msingi wa kusajiliwa pale masjala. Kila la kheri na nakuombea ushindi ili mahakama imwadhibu Bulembo.
Ona uwezekano wa kumwongeza na Antony Dialo
Diallo wala hata usihangaike naye , Mungu kishamtandika tayari
 

chuma cha mjerumani

JF-Expert Member
Dec 4, 2013
8,651
2,000
jpm kaleta nuksi kwenye inchi.


kiongozi akishakuwa mwenye roho ya uharibifu miaka yake ni hasara kwa taifa na kwa inchi.
 

chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,670
2,000
Bulembo hajavuna alichopanda,kapiga kampeni weeee lakini sasa katulizwa,kimya,hana lolote la kumwambia yeyote
 

THE LOST

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
1,067
2,000
kwenye list mweke na Nape maana nashindwa kuwaelewa wanaomuonea huruma huyu chalii.
 

bibinnaa

JF-Expert Member
Jan 17, 2017
1,502
2,000
Kusema uwongo pia ni kosa,kwa vile Mzee EL hakujinyia jukwaani kama tulivyo aminishwa,na kwa vile sasa amerudi kwao,na kwa vile kesi ya jinai haina time frame kuisajili,kwa nini mtu,watu au taasisi iliyopanga au kuratibu uwongo huo usijumuishe katika hiyo kesi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom