Nakushauri ndugu yangu Emmanuel Mbasha, hata wajinga huzeeka

Huyu jamaa ni msanii kama wasanii wengine ,sioni kosa lake

Ni msaka riziki kama wajanja wengine , Anajipendekeza kwenye Utawala huu , anaimba nyimbo za kusifu na si kukosoa

Kwahiyo acha ale bata

Mwenye shida ni wewe unayemuona ni mtumishi , Wakati yeye anajiona ni msanii kama wasanii wengine
Mwenye shida ni wewe unayemuona ni mtumishi , Wakati yeye anajiona ni msanii kama wasanii wengine

Umemaliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kwa mtu aliebise na kazi zake anaweza kuwa na muda wa kufuatilia life la watu wengine? Hizi nielement za kimasikini
Mkuu hii ni forum,siyo kila kinachochapishwa humu lazima ucomment.......kuna taarifa unazopenda wewe wengine hawapendi so kila mtu ukimfuatilia utapata tabu sana.


Then,next week nitakuja niangalie ile project yako ya ujenzi wa ghorofa lako kama umeshafanya finishing maana unaonekana upo busy sana na mambo ya msingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kwa mtu aliebise na kazi zake anaweza kuwa na muda wa kufuatilia life la watu wengine? Hizi nielement za kimasikini

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa tajiri,ila kwenye hii forum ukiwa busy kufuatutilia nani kapost nini na kina mantiki au hakina.....na wewe ukaconclude kuwa anachezea muda,wewe unayefuatilia nani kafanya nini ndiyo huna chakufanya maana kitu ukiona hakina manufaa kwako huna haja ya kucomment Mkuu
 
Wadau poleni kwa majukumu. Kuna picha mitandaoni inayomwonesha muimba nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha akiwa beach (nadhani), amevaa taulo tu huku sehemu ya boxer ikionekana.

Wachangiaji wamemshauri kwa hekima kwamba, angejisitiri vizuri maana yeye ni mtumishi wa Mungu (pengine kweli).

Lakini pia siku za nyuma, huyuhuyu Mbasha aliwahi kupost picha ya nyani (au sokwe) wakijamiiana!! Nayo ikazua balaa. Pia aliwahi kupost picha akiwa Zanzibar na binti yake (huku ikijulikana kwamba hakuwa na mkewe, walishaachana).

Sasa mimi najiuliza, Mbasha kama kweli ni mtumishi wa Mungu kwa nini hawi kioo?

Mambo anayoyafanya si kielelezo hata kidogo kwamba, kwa matendo yake mwingine anaweza kusema 'awe kama yeye.'

Ninavyojua Mimi, mtu anayejipambanua kuwa ni mtumishi wa Mungu anatakiwa awe kielelezo. Afanane tabia na uadilifu wa jamii yake. Huwezi mtaani kusema umeokoka au unamwimbia Bwana huku unaoneshewa kidole kwa matendo yako yenye kutia shaka.

Yesu walipomshutumu kwamba alikuwa kinyume na mafundisho ya uadilifu, aliwataka mafarisayo wataje kazi zake mbaya, mafarisayo wakashindwa kuzitaja (hazikuwepo).

Uadilifu wa Yesu uliingia mpaka kwa wanafunzi wake. Walimuiga kila kitu. Ndiyo maana Petro alipomfuata Yesu, kwa Kuhani Mkuu baada ya kukamatwa, watu waliomuona walimjua kuwa, alikuwa mwanafunzi wake, licha ya Petro kukataa.

Lakini wakasema 'hata kutembea kwake' kunafanana na Yesu, achilia mbali ongea yake. Mtu anayesema ameokoka anategemewa awe mfano mzuri kwa matendo yake ili watu waseme zamani alikuwa hivi, kabadilika, kweli wokovu upo (Kama jambazi anapoacha ujambazi wake).

Ndugu yangu Mbasha amekuwa kama ameokokea fasheni. Akumbuke zamani alikuwa Muislamu, akaenda ukristo. Kwa hiyo anatakiwa kusimama sawasawa bila kutia mbwembwe.

Nasema mbwembwe kwa sababu anayoyafanya huwezi kusema 'ni ubinadamu', bali anajiendekeza na kujipuuza, pia hajijali kwamba yeye ni nani!

Anasahau kwamba, kuwa mtumishi wa Mungu maana yake Mungu ndiyo bosi (mkuu), Sasa inakuaje mkuu awe mwema, lakini msaidizi wake ndiyo Mbasha? Mimi namshauri Mbasha kutafakari sawasawa, ayafanyayo hayana ubinadamu bali ni ushamba au kutotumia akili kuwaza sawasawa kabla ya kuamua kutenda.

Vyema kila mara kumwomba Mungu hekima kwani mwisho wa siku uzee utamfika na watu hawataweza kumpa cheo cha 'ana hekima' kwa sababu ya uzee kwani hata wajinga nao huzeeka!!

Kwa matendo yake ya mitandaoni, itafika nahali watu hawatakuwa na shaka na yeye, bali huyo mchungaji wake, kwamba anashindwa wapi kumnyoosha 'bwana mdogo' kama Mbasha?


Sent using Jamii Forums mobile app
Mbasha Mtumishi wa Mungu !
 
Kama ana akili kuna jambo atakuwa amejifunza na wangeacha mchomvu mabangi amvue utumishi kabisa
 
Back
Top Bottom