Nakuru, Kenya: Mume aliye na matatizo ya kiakili amuua kwa kumchinja mkewe aliyekuwa mjamzito

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,053
2,000
5e2957532abc0fda223705a8858d389b.jpg
Hali ya huzuni ilitanda katika kijiji cha Kikopey, eneobunge la Gilgil, Kaunti ya Nakuru baada ya mwanamume aliye na matatizo ya kiakili kuua kwa kumchinja mkewe aliyekuwa mjamzito.

Kulingana na mashahidi, mshukiwa alifanya mauaji hayo saa chache baada ya kutibiwa katika zahanati moja kijijini hapo.

Kiongozi wa Kanisa la Trinity United Methodist, Alex Karuri aliiambia Taifa Leo kuwa alikuwa miongoni mwa waliompeleka mshukiwa hospitalini mapema asubuhi kabla ya mauaji hayo.

Alisema baada ya kutoka hospitali, walimpeleka mshukiwa hadi nyumbani kwa wazazi wake ambapo alilala fofofo.

"Alipoamka usingizini saa chache baadaye mchana, alianza kuzua vurugu hivyo mama yake akalazimika kuniita niende kumsaidia kumtuliza", alisema Pasta Karuri.

Baadaye mwanamume huyo alisisitiza kuwa alitaka kwenda kumtembelea rafiki yake anayeishi karibu na barabara ya Naivasha-Nairobi.

Aliruhusiwa kwenda kumtembelea rafiki yake, lakini mchungaji na mama yake walimfuata nyuma ili kuona alipokuwa akienda.

Ghafla

"Alishindwa kumpata rafiki yake na kuanza kutimua mbio kurudi nyumbani. Mimi na mama yake ambaye ana umri mkubwa tulijaribu kumkimbiza lakini akatuzidi kwa kasi", alisema Bw. Karuri

Baadaye majirani walisikia kelele na walipokimbilia katika eneo la tukio walikuta mke wa mshukiwa akiwa amelala chini huku damu zikimvuja. Mshukiwa alikuwa ameshikilia kisu chenye damu mkononi karibu na mwathiriwa.

"Alitishia kuwashambulia vijana waliojaribu kumpokonya kisu hicho. Lakini baadaye alizidiwa na akanyang'anywa kisu hicho", alisema mchungaji huyo.

Mkuu wa Polisi wa Gilgil, Sarah Koki alithibitisha kisa hicho huku akisema kuwa maafisa wa usalama walifahamishwa kuhusu mauaji hayo jioni.

Alisema polisi wameanza uchunguzi kuhusiana na kisa hicho. Na mshukiwa alikamatwa na anazuiliwa katika kituo cha polisi huku maiti ya mkewe ikiwa imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Gilgil.

Chanzo: TaifaLeo
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,053
2,000
Ukweli unabaki pale pale tu, kuwa mgonjwa wa akili si wa kumpeleka hospitali na kurudi naye nyumbani. Wangembakisha hospitali mpaka wapate ripoti ya daktari kuwa sasa walau yuko sawa.

ili kuchelea madhara makubwa kama haya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom