Nakupenda Tanzania, nawapenda Watanzania wenzangu

code4494

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
798
1,204
Habari za wakati Kama huu ndugu zangu wana JF, katika harakati zangu za kutafuta maisha nimebahatika kuishi nchi tofauti tofauti lakini niseme ukweli sisi watanzania tupo tofauti Sana na nchi nyingine zilizotuzunguka,

Naongelea nchi km Zambia, Congo, Kenya, Uganda, Malawi, Namibia, Somalia, Mozambique kiukweli tupo tofauti Sana kwa style ya maisha tunayoishi,

Tanzania tumebarikiwa sana tukianzia jiografia ya nchi. Tanzania ina Hali ya hewa ya aina zote, kuna nyanda zenye baridi, kuna nyanda zenye joto, tuna pwani nzuri, tuna sehemu zenye Hali ya jangwa,tuna sehemu zenye rutuba ya kutosha, hii ipo tofauti kwa hz nchi nyingine ambazo hazina sifa zote tulizonazo sisi.

Kutokana na kuwa na Hali ya hewa tofauti tofauti imesababisha kuwepo na aina tofauti za udongo na virutubisho tofauti tofauti hvyo kufanya tuwe na mazao ya Kila aina ,mfano kwa hapa kwetu Tanzania kifungua kinywa asubuhi unauwezo wa kuamua nile magimbi,viazi,uji ,mkate,mihogo katika nchi nyingine machaguo ni machache mno, ndo maana hapa kwetu ni ajabu au aibu kusikia mtu au watu kuvamia na kuiba sokoni.

Umeshawahi kula wali maharage Nazi na dagaa wa uono pale chumbageni Tanga jirani na Kijiji Cha miaka 21? Ndo utajua maharage Ni km maini au Umeshawahi kula mboga ya majani ya maboga yaliyoungwa na karanga ukala na ule wali wa kunukia tukuyu kyela

Tanzania kwa misosi hapa ndo mahala pake, ukiachilia Somalia na Mombasa Kenya, Tanzania tunamapishi yanyofanya chakula kiwe kitamu kupita maelezo, nchi kama Congo nyama ya ng'ombe wanakula matajiri, Mara nyingi wafanyakazi wa UN, ukimuambia mzulu akupikie ugali au wali,utaona kituko cha maisha

Ukija kwa dada zetu nao hawapo nyuma,huku kwetu Tanzania wapo wasichana warembo wa Kila aina na maumbile tofauti hii ipo tofauti Sana na nchi km Rwanda au Congo wadada wa huko wengi ni wa aina moja.

Hata sisi wanaume tukienda nchi jirani wadada wa kule wanatupenda sana, mfano Congo wanaume wa kitanzania wanaitwa wamerakani weusi, hii inatokana vijana wa Kitanzania tuna swagger za kutosha, kuanzia muonekano wa maumbo yetu na mavazi ya kijanja.

Yaani kwa kifupi sisi taifa la Tanzania ni kama bidhaa zenye sifa tofauti tofauti.

Lakini vyoto hyo tuna utajiri wa kutosha wa maliasili hapa kila mmoja anajua hilo.

La kumalizia pamoja na kuwa nchi yetu ni kubwa lakini mikoa imeunganishwa na lami tofauti na nchi km Congo, Ethiopia, Zambia na hata ukienda mikoani hakuna tofauti Sana na miji mikuu, mfano mtu alieko kijiji cha kipara mnero mkoani Lindi anapata asilimia 80 ya mahitaji kama alyeko mjini.

Lahiti km kiingereza kingekuwa lugha ya taifa, tungekuwa mbali sana watanzania wengi lugha ya Kiingereza inawatatiza inadumaza harakati za maisha!
 
Mkuu mbona English ni lugha ya taifa au unamaanisha American English ya wakina 2 Pac
 
mkuu mbona English ni lugha ya taifa au unamaanisha American english ya wakina 2 pac
Nilikuwa sijui , Asante kwa kunijuza lakini mbona tukiwa nje ya nchi tunapata tabu katika lugha?nimeona Kuna baadhi ya nchi ukiomba kusoma lazima uambatanishe na certificate ya TOELF au ILETS
 
code4494,
Wenyewe wanaita Ngeli
1f602[1].png
 
mimi nipo kijiji cha ngumi jiwe, naperuzi na kudadisi network hadi niende mlimani ndio nawapa vizuri huko dar!
Yeah sio mbaya angalau una smart phone na network ipo. Kuna sehemu inaitwa KOLOWEZI ipo Congo ukiugua malaria unaota jua.... madereva wa magari ya mizigo watakuambia.
 
Mimi namiss chipsi yai na mishkaki, kuku sekela na nyama choma na ugali wa pale arusha chini ya mti Tanzania kwa vyakula mmejaaliwa.
 
Mimi namiss chipsi yai na mishkaki, kuku sekela na nyama choma na ugali wa pale arusha chini ya mti Tanzania kwa vyakula mmejaaliwa.
Ndo maana waking Christian bella baada ya kuonjeshwa chips za rojo za kinondoni ,yenye ukwaju na mayonnaise wamegoma kurudi makwao
 
Back
Top Bottom