Nakupenda kwa moyo wote.

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,020
576
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.
Nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni kheri mama weee!
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote.

Niliimba wimbo huo kama kasuku hapo zamani za kale. Lakini siku hizi najiuliza, ni ya kweli maneno hayo???? Kila mtanzania anayachukulia kwa uzito sawa? Kweli Tanzania ni mama ambaye hawezi kukimbiwa? Tanzania huyo anawapenda wanawe? By the way, Who is Tanzania anayeotwa nilalapo na njaa sina hakika kama kesho nitakula, lakini nawaona watu wanaporomosha marichmond na wanapora madini, viranja wanatuambia tuwe na subira mara miezi 18 ya kujifunga mkanda, mara ruksa hata kula vyura, mara tunaambiwa ni wafinyu wa kufikiri na wenye wivu wa kijinga pale tunapouliza maswali kwamba wote ni watoto wa mama mmoja tusinyimane, na sasa tunaambiwa ngonjera nyingine - maisha bora kwa kila mtanzania (ngawa kwa kweli bora maisha kwa kila mtanzania kwa kweli)????? Au kina kaka na dada waliotangulia kuzaliwa nwa mama yetu Tanzania wanatudanganya kutokana na udogo wetu? Hawapatikani maofisini na daima dumu ama wako safari za per diem au mikutano ya per diem, sisi hata tukitishia kugoma tunaahidiwa kupewa peremene tu na tunanyamaza.
 
sisi hata tukitishia kugoma tunaahidiwa kupewa peremene tu na tunanyamaza.

wajanja wengi,chkukua chako mapema!!!!!!!!!
 
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.
Nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni kheri mama weee!
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote.

[/COLOR][/SIZE]

Uminirudisha MBALI kweli kweli asante....
 
Kumbe kipindi kile na utoto ulikuwa unachangia ..eti nilalapo nakuota wewe niamkapo ni kheri mama weee
Hivi na mafisadi waliimba wimbo huu??
 
some wounds never heal

tna mnaniumiza kabisaaaaaaaa mwenzenu!!! Watoto wa hii Tanzania ndo wabaya!!!

na kweli where are you Mama Tanzania!!
 
Kumbe kipindi kile na utoto ulikuwa unachangia ..eti nilalapo nakuota wewe niamkapo ni kheri mama weee
Hivi na mafisadi waliimba wimbo huu??

yes waliuimba n they are still doing it kwenye mihadhara....they will do it again if we are not careful come October this yr.
 
oooh my daughter:

wewe unaona hata dalili za watu kuwa careful mpaka hapa tulipo kweli??

labda miujiza ya huyu Mungu wa Ibrahim na Yakobo tu....
 
Hivi ni nani mtunzi wa wimbo huu??

Back
Top Bottom