Nakumbushia tu jamani

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,534
1,089
Wale vyura wetu wa Kihansi wanaotoa umeme wakapelekwa US kuhifadhiwa walisha rejeshwa?

2. Vile vitwiga vilivyo pandishwa ndege ya Qatar vilisha rejeshwa? Au vilipewa full scholarship?

3.Ile kesi ya aliekuwa anakwapua Nil.7 kwa dakika bado IPO?Au RAIS alikuwa anatania?

4.Coco beach alie ikwapua alisha irejesha sirikalini? Au ulikuwa utani tu?

5.Vigogo wanaolipwa zaidi ya Milioni 30 walishaanza kufyekwa au RAIS alikuwa anachomekea tu?

6.Watumishi WA Sirikali walishapata nyongeza ya mishahara yao au hadi ndege 5 zinunuliwe?

7.Kesi ya Gwajima iliishaje au ilikuwa kutafuta Kiki kama Rayvann?

8.Walio ahidiwa kupangiwa KAZI nyingine walisha pangiwa WOTE hasa mama yake mdogo na Kaka Lemtuz? Au baada ya X mass?

10. Walio Dhulumiwa Malipo wa usimamizi na usahihishaji Mock Form Four TARIME walisha lipwa au ndio imetoka?

11. Yule Ofisa ELIMU aliewekwa ndani TARIME MJI akatejeshwa kabla HATA mwezi kuisha kazini aliemuweka ndani bado yuko ofisini kwake? Au ilikuwa kutafuta kiki?

12. Mke WA RAIS kutibiwa Mhimbiri Mrema kugharamiwa India matibabu!!!Kumbe Mrema ni mdosi kuliko WAMA ajae?

Ninachomekea tu jamani, Cyber crime Act inisamehe bure.
 
Back
Top Bottom