Nakumbuka zamani

Pearl

JF-Expert Member
Nov 25, 2009
3,036
309
Nakumbuka zamani.............,zamani kwakweli ilikuwa raha sana na heshima tele,zamani
1.Marufuku kupita makaburini na ikitokea umepita basi ni mwendo wa haraka tena bila kuangalia nyuma wala kungea,lkn siku hizi makaburi yamegeuzwa gesti.

2.zamani mvua kama hizi zinazoendelea kunyesha Dar watu wako busy na kukinga maji na watoto kuoga kabisa,tena maji hayo yanakuwa salam kwa kunywa lkn siku hizi watu ni ma dispenser na maji ya chupa kwa sana.

3.Zamani mtu mzima akipita kwanza unampokea mzigo na kumfikishia kule aendako,lkn siku hizi watu wanawapiga mpaka vikumbo na salamu si lazima.

4.Zamani hasa kwetu Tv tulikuwa tunaangalia taharifa ya habari tu,au bada ya kumaliza kazi za shule tena jumamosi na jumapili tu,siku hizi watoto wanajua ratib zote za vipindi.

5.Zamani mgeni akifika kwako unampokea,anaingia ndani mnataniana hili na lile alafu salamu inafuata lakini siku hizi ukiskia hodi tu na salamu inatolewa hapo hapo utasema huyo mgeni haingii ndani.

6.Zamani hatukuangaika na vitafunio vya chai maana mihogo,viazi,magimbi vipolo vya ugali na wali asb ni kupasha na kula tu lkn siku hizi mara mkate ,sausage,mayai .

7.Zamani msiba unaheshimika lkn siku hizi msibani watu wamegeuza sehemu za kupata wachumba,kujipodoa na kuoneshana vitu tofauti tofauti.

8.Zamani hasa jioni nilipenda sana hadithi za bibi maana zilinifunza mambo mengi na ya kunijenga,hata michezo ya zamani hasa rede,kombolela,lakini sasa hakuna michezo hiyo.

NAJUA DUNIA YA SASA NI KIJIJI LKN KIJIJI HIKI MMMH WALA HAKIFANANI NA KILE CHA KWETU MAANA KIJIJINI KWETU WATU WALIISHI KWA UPENDO,AMANI NA UMOJA.

WEWE ZAMANI UNAKUMBUKA NINI?
 
yani nakumbuka kweli zamani heshima ilikuwepo kweli ukikosea mbele ya wakubwa unachapwa hapo hapo na ukienda kusema kwenu babafulani kanichapa baba yako anakuchapa tena, siku izi mpige mtt wa jirani yako uone kivumbi.

zamani mkubwa akikutuma unakwenda mbio siku izi mtume mtt wa jirani usikie alafu uwe ujabahatika kuzaa.
zamani misiba ilikuwa watu wanaheshimu kwa hofu siku izi imekuwa fashion yakuonyeshana milio ya simu
 
Zamani mkubwa akisimama kwenye daladala unampisha kiti, lakini siku hizi kama mtoto kalipa nauli kamili hapishi mtu
 
Zamani unakutana na mkubwa unamuuliza njia na anajua hujala , atakununulia chakula au kukupa chakula na wala hataki kujua atakuona lini tena
 
Zamani ukisikia wimbo wa Taifa unaimbwa hata kwenye redio, utasimama kikakamavu na hakuna kutingishika hadi wimbo uishe.

Zamani bendara ya Taifa ikiwa inashushwa, afande hupiga filimbi na wote hata wapita njia husimama mpaka bendera ishushwe yote.
 
Zamani nilifaidi michezo mbalimbali kwa vitendo kama vile kombolela,kiboreni,rede,stika, kuzungusha ringi nk lakini siku hizi watoto wanaishia kuangalia kwenye T.V tu wakijitahidi sana kwa vitendo ni kucheza kamari
 
Zamani ukisikia wimbo wa Taifa unaimbwa hata kwenye redio, utasimama kikakamavu na hakuna kutingishika hadi wimbo uishe.

Zamani bendara ya Taifa ikiwa inashushwa, afande hupiga filimbi na wote hata wapita njia husimama mpaka bendera ishushwe yote.

hehe hii bora imepita,hii sio ile zamani ninayoitamani.
 
zamani watu tulikuwa tunaokota hela barabarani hasa coins siku hizi thubutu! hata mfukoni hakuna....
 
Zamani wajameni ilikuwa bomba sana,soda tulikuwa tunakunywa wakti wa eid,xmas,mwaka mpya au pasaka, na ilikuwa mnanunuliwa double cola alafu mnapimiwa kwenye vikombe vya plastic then mkubwa anakunywa kwenye chupa,kivumbi ni pale ukinywa lazima machozi yakutoke sababu ya gesi na kukosa uzoefu wa kunywa soda,wacha siku hizi mtt wa mwaka 1 anakupigia koka kubwa macho makavuuuu wala halii.
 
daaa umenikumbusha mkuu...tulikuwa tunaingia kumbi moja hivi ya kuonesha video kiingilio kinywaji..kikiisha unatolewa,basi tulikuwa tunafannya kupuliza soda mpaka picha inaisha:A S 109:
 
ah wewe, zamani tulikuwa tukicheza tiali bado kwenye majani hapo unapata na ka-mchumba kwa siku hiyo ...aah nakumbuka zamani, baba alikuwa na radio ya mbao betri kubwa mbili, zikiisha charge anazipondaponda na kuanika juani then anaweka radioni tunaendelea kusikiliza mama na mwana kipindi cha Debora Mwenda, ah zamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
daaah debora mwenda! yuko wapi huyu mama? nilikuwa ckosi kila jmosi!
 
saa nane kama sikosei, unakumbuka ile hadithi ya bibi Aga...!! ah long time mkuu...huyu mama sijui yuko wapi?
 
saa nane kama sikosei, unakumbuka ile hadithi ya bibi Aga...!! ah long time mkuu...huyu mama sijui yuko wapi?[/QUOTE

alikuwa anawaelezea wahusika kwa utaalam mpaka na wewe unajihisi umo...halafu anakuacha na nyege za jmosi inayofuata we acha tu!
 
ah zamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ! na ile hadithi ya ADILI NA NDUGUZE mwaikumbuka...zamani raha jamani..
 
Zamani unakutana na mkubwa unamuuliza njia na anajua hujala , atakununulia chakula au kukupa chakula na wala hataki kujua atakuona lini tena
what is zamani, miaka kumi ishirini salasini au
 
Nakumbuka kile kipindi cha redio tanzania kinaitwa 'mshikamano' (sina hakika sana) kilikuwa kila Jmos mida ya asubuhi flani hivi. Nakumbuka jingo ya kile kipindi mwimbaji anataja makabila mbalimbali ya TZ basi akitaja "Wahaya" nyumba nzima tunaruka ruka kwa furaha.
Ulikuwa unaimbwa "..Tweende mshikamano twende mshikamanoo,... Wanyakyusa mshikamanooo...wahayaa mshikamanoooo...." (Na makabila mengine mengi)
 
uje tena shangazi,uje tena shangazi,shangazi shangazi chei,chei shangazi tufurahi shangazi!
 
Back
Top Bottom