Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,552
- 19,420
- Thread starter
- #21
Rubani akiitwa SAIDI KARAMA, alizikwa siku ya jumatano katika makaburi ya Kisutu, maiti ilitokea mtaa wa Congo nyumba namba 40, mahali palipokuwa na ule mti mkubwa uliokuwa unatumiwa sasa na wanga wa mitaa ya Kariakoo,maarufu kama MTAMBANI maziko yaliongozwa na Mzee Kawawa,sina hakika by then alikuwa ni waziri mkuu au waziri wa ulinzi.
Ile ajali ya ndege imebaki kwenye kumbukumbu za wengi walioshuhudia na kusikia kwenye radio, enzi hizo hakukuwa na TV. Walikuwa marubani wawili, Capt. Said Karama na Capt. Abdallah (?) Kikunda. Inawezekana jina la kwanza la marehemu Kikunda likawa sio sahihi, lakini jina la ukoo ni Kikunda. Nadhani baada ya hapo ilipita miaka mingi bila kuwa na hizo air shows, sina hakika kama zimerudishwa miaka hii. Mungu Awalaze pema.
Jamani, hawa mashujaa mbona hatuweki habari zao kwa maandishi ili vizazi vingi zaidi vijue heshima kubwa iliyotolewa na watu hawa wachache waliotangulia mbele ya haki?
Tukio lile lilikuwa na sifa kadhaa mabazo uilitakiwe liwe la kihistoria ila basi ni sisi wachache tu tuliolishuhudia ndio tuna kumbukumbu.
(1) Ilikuwa ni ndege ya kwanza ya kivita kuanguka mbele ya umati wa watanzania tena wakati wa sherehe.
(2) Ilikuwa ni tukio mara tu baada ya vita pekee ambayo jeshi letu lilikuwa limetekeleza jukumu lake la la kulinda na kutetea mipata yetu: Vita ya Kagera
(3) Ni ajali iliyotokea mbele ya macho ya amiri jeshi mkuu
(4) Kipindi hicho tulikuwa na marubani wachache sana wenye ujuzi wa ndege za kivita, hivyo kupoteza marubani waiwili lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa jeshi letu la anga ambalo lilikuwa bado changa.
Binafsi nilikuwa mwanafunzi wa form 6 wakati huo, na nilikuwa Dar kwa dharura fupi nikatumia nafasi hiyo kwenda uwanja wa taifa kujionea ndege zile kwa vile niliwahi kuziona kwenye mazoezi. Kwa bahati mbaya, ilikuwa ni experience mbaya sana kwangu kwani ilibadilisha nisipende tena kazi ya urubani niliyokuwa naota kwa PGM yangu. Mara ya mwisho nilipoondoka Dar es Salaama, sikuwahi kuona kumbukumbu yoyote ya tukio hilo. Wakati nikiwa JKT Mgulani nakumbuka kusikia mradi wa mnara huo lakini sina uhakika kama kweli ulijengwa wakati huo. To the best, wangeweka vipande (debris) vya ndege hiyo kule jumba la makumbusho ya taifa.