Nakumbuka Mtani wangu alilalama kumpikia chai Nchimbi akakimbilia CHADEMA

Mnambua

JF-Expert Member
Jan 6, 2020
246
250
Msifikiri kuwa Waitara Mwita (Naibu Waziri TAMISEMI) kaanza leo kuropoka ropoka (off-course pengine hajaropoka kaongea ukweli), ameanza siku nyingi na ndiyo tabia yake hiyo. Huyu jamaa miaka ya nyuma alikuwa ni Mwanachama wa CCM na kwa sababu hufanya siasa kama biashara akakimbilia CHADEMA kwa ajili ya kunufaika kwa business hiyo. Alipokuwa CHADEMA akapewa madaraka akawa analipwa vizuri na mpaka pale waliposambaratishwa kwenye mpango wao wa kimapinduzi ndani ya CHADEMA (zZtto, Kitila Mkumbo na Mwigamba) kiasi akawa mnyonge na CCM akawa hana msuli wa kuwarudia kwa wakati huo kwa sababu hakuwa amekipata alichokusudia na CCM aliondoka kwa maneno ya kejeli sana.

Leo mie naongelea tu hulka ya huyu bwana. Huyu Bwana anawachora sana watu wa Musoma ambao hawana tabia za kijinga jinga kama yeye. Ukweli watu wa Musoma ambao ni watani na sisi Wanyiramba nimefanya nao sana kazi nikiwa Dar maeneo ya Ukonga na ni hawana tabia za kijinga hivyo. Huyu jamaa haaminiki kabisa. Kiutaratibu duniani hamna taasisi ambayo huwa haina mapungufu - hata Marekani yenyewe Serikali ya Donald Trump ina mapungufu lkn hatokei mtu wa Donald Trump akaanza kuelezea mapungufu hayo hadharani hata wakitofautiana. Ikitokea hilo ni hali mbaya. Waitara ndiyo tabia yake hiyo - anawasema wenzake lkn hata yeye angekuwa hakatwi hizo hela angenyamaza tu kimya. Waitara hiyo tabia inawezekana ni ya kuzaliwa nayo.

Kama mtakumbuaka wakati akihamia CHADEMA aliwasema sana wenzake WanaCCM kuwa walikuwa wanamnyanyasa - akadai yeye na bachelor degree yake ya Ualimu akaajiriwa kumpikia Nchimbi chai pale Lumumba - yaani akawa kama mhudumu wa Ofisi ya Nchimbi - enzi hizo Nchimbi akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana. Siku hizo pia aliongea maneno mengi sana na akatoa siri nyingi sana za Chama chetu cha CCM. Huyu bwana maneno hayo yakawakosha CHADEMA na wakamchukua. Miaka ikaenda mara yeye na Kitila, Zito na Mwigamba wakapanga mkakati wa mapinduzi ndani ya CHADEMA lkn kwa kuwa ni mnafiki akawalipua wenzake kisirisiri na Mbowe akamhonga fedha nyingi sana (ushahidi ninao) na kumfanya mtu wake wa karibu na ndiyo maana kati yao wanne ni yeye tu alibaki CHADEMA.

Baada ya kupata mradi wake CHADEMA basi CCM kwa kuwa wanamjua ni mfanyabiashara kwenye siasa wakamhaidi nafasi ya Uwaziri (ingawa ahadi haijatimia akapewa unaibu kwanza) ili ahamie huko na akalipwa kiasi cha shilingi milioni 278 ili kuhakikisha CHADEMA inapoteza Dar-es-Salaam. Katika kiasi hicho cha fedha alitakiwa pia ahakikishe madiwani wasipongua 10 wanaondoka CHADEMA au CUF lakini hilo hajafanikiwa na ndiyo maana mpaka sasa hajapewa Uwaziri - ingawa ameahidiwa kama ameshindwa hilo basi ahakikishe anamtoa Heche na pia atasaidiwa na dola kutimiza hilo. Tayari mipango hiyo inajulikana.

Labda tu nimalizie kwa kusema - huyu Waitara kwa hayo yote aliyofanyiwa na CCM iwapo itatokea hajatekelezewa na yale aliyoahidiwa huko baadaye basi mjue atakuja kulipuka tena dhidi ya CCM kama alivyofanya sasa dhidi ya CHADEMA. Kitakachowaokoa CCM ni iwapo itatokea akashindwa ubunge basi wakampa ubalozi au ukuu wa mkoa hapo itakuwa nafuu yao. Lakini ikitokea CCM wakashindwa kwenye Uchaguzi kikachukua CHADEMA au hao NCCR Mageuzi basi ujue ni lazima Waitara ataenda tena huko na tabia yake ya taarabu dhidi ya CCM itaendelea hivyo hivyo.

Namalizia tu kusema kuwa huyu mtani wangu hafai - tena hafai haswa. JPM mwone kwa jicho la ziada huyu jamaa - ni mfanyabiashara wa kisiasa - tena ukimpa Uwaziri ni wale wa aina ya Lugola atakupamba pamba sana na kukupendezesha wakati yeye kwake siasa ni income na wala sio kuwatumikia wananchi.
 
Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,600
2,000
Huko ni kutapatapa, kama mlijua ni mropokaji kwa nn mlimpa dhamana kubwa. Mwambieni Mbowe aachie ngazi ili chama kiimarike, siyo kuja na hoja dhaifu dhaifu eti Mbowe ni mwamba, ndiye nguzo ya chama wakati ukweli ni kwamba amekidhoofisha Chadema. Mbadhirifu wa fedha za chama nk
 
Mhujumu Uchumi

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
1,307
2,000
PIA KWA WALIE KARIBU NAE NAOMBENI MUMSHAURI ASIWE ANALEWA SANA HADI KUTOKUJITAMBUA, DUNIA INA MENGI NA IMEHARIBIKA
Nikimkuta na hali kama niliyomkuta nayo juzi nam-"0713" huku namrekodi, hawezi kupiga larger mpaka kutojitambua kiasi kile, anatuaibisha wanywaji, wote tunaonekana hatujui kunywa,tunajifunza, yeye ndo ana degree
 
balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
9,244
2,000
Msifikiri kuwa Waitara Mwita (Naibu Waziri TAMISEMI) kaanza leo kuropoka ropoka (off-course pengine hajaropoka kaongea ukweli), ameanza siku nyingi na ndiyo tabia yake hiyo. Huyu jamaa miaka ya nyuma alikuwa ni Mwanachama wa CCM na kwa sababu hufanya siasa kama biashara akakimbilia CHADEMA kwa ajili ya kunufaika kwa business hiyo. Alipokuwa CHADEMA akapewa madaraka akawa analipwa vizuri na mpaka pale waliposambaratishwa kwenye mpango wao wa kimapinduzi ndani ya CHADEMA (zZtto, Kitila Mkumbo na Mwigamba) kiasi akawa mnyonge na CCM akawa hana msuli wa kuwarudia kwa wakati huo kwa sababu hakuwa amekipata alichokusudia na CCM aliondoka kwa maneno ya kejeli sana.

Leo mie naongelea tu hulka ya huyu bwana. Huyu Bwana anawachora sana watu wa Musoma ambao hawana tabia za kijinga jinga kama yeye. Ukweli watu wa Musoma ambao ni watani na sisi Wanyiramba nimefanya nao sana kazi nikiwa Dar maeneo ya Ukonga na ni hawana tabia za kijinga hivyo. Huyu jamaa haaminiki kabisa. Kiutaratibu duniani hamna taasisi ambayo huwa haina mapungufu - hata Marekani yenyewe Serikali ya Donald Trump ina mapungufu lkn hatokei mtu wa Donald Trump akaanza kuelezea mapungufu hayo hadharani hata wakitofautiana. Ikitokea hilo ni hali mbaya. Waitara ndiyo tabia yake hiyo - anawasema wenzake lkn hata yeye angekuwa hakatwi hizo hela angenyamaza tu kimya. Waitara hiyo tabia inawezekana ni ya kuzaliwa nayo.

Kama mtakumbuaka wakati akihamia CHADEMA aliwasema sana wenzake WanaCCM kuwa walikuwa wanamnyanyasa - akadai yeye na bachelor degree yake ya Ualimu akaajiriwa kumpikia Nchimbi chai pale Lumumba - yaani akawa kama mhudumu wa Ofisi ya Nchimbi - enzi hizo Nchimbi akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana. Siku hizo pia aliongea maneno mengi sana na akatoa siri nyingi sana za Chama chetu cha CCM. Huyu bwana maneno hayo yakawakosha CHADEMA na wakamchukua. Miaka ikaenda mara yeye na Kitila, Zito na Mwigamba wakapanga mkakati wa mapinduzi ndani ya CHADEMA lkn kwa kuwa ni mnafiki akawalipua wenzake kisirisiri na Mbowe akamhonga fedha nyingi sana (ushahidi ninao) na kumfanya mtu wake wa karibu na ndiyo maana kati yao wanne ni yeye tu alibaki CHADEMA.

Baada ya kupata mradi wake CHADEMA basi CCM kwa kuwa wanamjua ni mfanyabiashara kwenye siasa wakamhaidi nafasi ya Uwaziri (ingawa ahadi haijatimia akapewa unaibu kwanza) ili ahamie huko na akalipwa kiasi cha shilingi milioni 278 ili kuhakikisha CHADEMA inapoteza Dar-es-Salaam. Katika kiasi hicho cha fedha alitakiwa pia ahakikishe madiwani wasipongua 10 wanaondoka CHADEMA au CUF lakini hilo hajafanikiwa na ndiyo maana mpaka sasa hajapewa Uwaziri - ingawa ameahidiwa kama ameshindwa hilo basi ahakikishe anamtoa Heche na pia atasaidiwa na dola kutimiza hilo. Tayari mipango hiyo inajulikana.

Labda tu nimalizie kwa kusema - huyu Waitara kwa hayo yote aliyofanyiwa na CCM iwapo itatokea hajatekelezewa na yale aliyoahidiwa huko baadaye basi mjue atakuja kulipuka tena dhidi ya CCM kama alivyofanya sasa dhidi ya CHADEMA. Kitakachowaokoa CCM ni iwapo itatokea akashindwa ubunge basi wakampa ubalozi au ukuu wa mkoa hapo itakuwa nafuu yao. Lakini ikitokea CCM wakashindwa kwenye Uchaguzi kikachukua CHADEMA au hao NCCR Mageuzi basi ujue ni lazima Waitara ataenda tena huko na tabia yake ya taarabu dhidi ya CCM itaendelea hivyo hivyo.

Namalizia tu kusema kuwa huyu mtani wangu hafai - tena hafai haswa. JPM mwone kwa jicho la ziada huyu jamaa - ni mfanyabiashara wa kisiasa - tena ukimpa Uwaziri ni wale wa aina ya Lugola atakupamba pamba sana na kukupendezesha wakati yeye kwake siasa ni income na wala sio kuwatumikia wananchi.
We kunywa bia barabara itakusaidia nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnambua

JF-Expert Member
Jan 6, 2020
246
250
Huko ni kutapatapa, kama mlijua ni mropokaji kwa nn mlimpa dhamana kubwa. Mwambieni Mbowe aachie ngazi ili chama kiimarike, siyo kuja na hoja dhaifu dhaifu eti Mbowe ni mwamba, ndiye nguzo ya chama wakati ukweli ni kwamba amekidhoofisha Chadema. Mbadhirifu wa fedha za chama nk
Baada ya Uchaguzi wa mwaka huu utaona CHADEMA watakavyokuwa wameimarika.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom