Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,978
- 5,025
Elimu yetu ilipokuwa bora! Huko wilayani tulikuwa tunasoma na watoto wa wakuu wa wilaya, wakurugenzi, maafisa mbali mbali. Mnakaa dawati moja na kushare vitabu na vifaa mbali mbali. Japokuwa walikuwa wakitetwa na magari ya serikali tulikuwa tunaona ni kawaida kwani nao walijiona wako sawa na sisi watoto wa wakulima. Ni wachache sana waliojiona ni zaidi lakini walikuwa watupu darasani hivyo kuwafanya wawe kimya. Kitu kikipungua shuleni mf madawati viongozi walifanya active participation ya kuhakikisha yanapatikana, hata vitabu pia walihakikisha vinafuatiliwa bohari kuu na kuletwa kwa gharama za halmashauri. Walimu walikuwa wanafundisha kwa moyo na kujituma kwani shule inayofaulisha sana walikuwa wanapewa zawadi. Nakumbuka tulifurahi tulipoambiwa hakuna kufanya kazi za watu binafsi baada ya mkuu wa wilaya kutuona tukiwa tumebeba kuni kupeleka mtaani. Ilitolewa amri wote wanaonunua vitu vya miradi ya shule wakasombe wenyewe wilaya nzima. Tulifurahi sana!.. Hii siyo mbali ni kipindi cha mwisho cha mwinyi na mwanzoni mwa mkapa. Lakini siku hizi, loh! Mkuu wa wilaya hakai wilayani au anaishi kama senior bachelor, mkurugenzi na waajiriwa wengine hata watoto wao huwezi kuwafahamu. Hukuti wakisoma au kushirikiana na watoto wa kawaida. Ukiuliza unaambiwa wanasoma nje. Kwa mshahara gani?! Wameua kiwango cha elimu shule za msingi ili watoto wao waendelee kuvuma ndani ya mfumo wa nchi hii. Imefikia hatua shule inakosa hata choo! Choo? Madwati yatakuwepo? Vitabu je? Walimu ndo kabisa, bora liende, sijui tunakoelekea. Tumefikia hatua ambayo kama ni uharibifu ni usiorekebishika! Tunahitaji kuanza upya. Elimu yetu inatia uchungu, hakuna sera ya taifa, kila anayekuja na madudu yake anayatekeleza na kuondoka. Toa maoni yako kwenye katiba kama watayafanyia kazi, tunahitaji kuwa na sera ya taifa ya elimu ambayo kila mmoja ataitekeleza.