Nakumbuka enzi hizo.

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,978
5,025
Elimu yetu ilipokuwa bora! Huko wilayani tulikuwa tunasoma na watoto wa wakuu wa wilaya, wakurugenzi, maafisa mbali mbali. Mnakaa dawati moja na kushare vitabu na vifaa mbali mbali. Japokuwa walikuwa wakitetwa na magari ya serikali tulikuwa tunaona ni kawaida kwani nao walijiona wako sawa na sisi watoto wa wakulima. Ni wachache sana waliojiona ni zaidi lakini walikuwa watupu darasani hivyo kuwafanya wawe kimya. Kitu kikipungua shuleni mf madawati viongozi walifanya active participation ya kuhakikisha yanapatikana, hata vitabu pia walihakikisha vinafuatiliwa bohari kuu na kuletwa kwa gharama za halmashauri. Walimu walikuwa wanafundisha kwa moyo na kujituma kwani shule inayofaulisha sana walikuwa wanapewa zawadi. Nakumbuka tulifurahi tulipoambiwa hakuna kufanya kazi za watu binafsi baada ya mkuu wa wilaya kutuona tukiwa tumebeba kuni kupeleka mtaani. Ilitolewa amri wote wanaonunua vitu vya miradi ya shule wakasombe wenyewe wilaya nzima. Tulifurahi sana!.. Hii siyo mbali ni kipindi cha mwisho cha mwinyi na mwanzoni mwa mkapa. Lakini siku hizi, loh! Mkuu wa wilaya hakai wilayani au anaishi kama senior bachelor, mkurugenzi na waajiriwa wengine hata watoto wao huwezi kuwafahamu. Hukuti wakisoma au kushirikiana na watoto wa kawaida. Ukiuliza unaambiwa wanasoma nje. Kwa mshahara gani?! Wameua kiwango cha elimu shule za msingi ili watoto wao waendelee kuvuma ndani ya mfumo wa nchi hii. Imefikia hatua shule inakosa hata choo! Choo? Madwati yatakuwepo? Vitabu je? Walimu ndo kabisa, bora liende, sijui tunakoelekea. Tumefikia hatua ambayo kama ni uharibifu ni usiorekebishika! Tunahitaji kuanza upya. Elimu yetu inatia uchungu, hakuna sera ya taifa, kila anayekuja na madudu yake anayatekeleza na kuondoka. Toa maoni yako kwenye katiba kama watayafanyia kazi, tunahitaji kuwa na sera ya taifa ya elimu ambayo kila mmoja ataitekeleza.
 
yaani mi huwa naangalia kila siku wanavyopiga kelele, tujenge shule! Wao watoto wao wanawapeleka hukoo... Huku kwenye shule zetu zisizo na maabara tunabaki sie na watoto wetu. Vitabu mashuleni siku hizi ni anasa sasa sijui hizo computer zitapatikanaje! We need a national policy ili tuachane na mambo ya kutekeleza sera za wahuni wachache wenye malengo ya watoto wao waendelee kupata na kunufaika na mfumo wa hovyo uliopo.
 
Last edited by a moderator:
Natamani kama ile enzi ingejirudia tena.
Zamani ulikuwa unaona sifa kuitaja sekondari unayosma japo iko huko wanakoita mikoa iliyosahaulika!
Sasa hivi bila kutaja Saint Fulani.., bado haijaonekana ni shule!
Kweli ya kale ni dhahabu...
 
shule za msingi sijui msalato, amani, iyunga, iwawa, vwawa, mwenge, chaugingi, mji mwema ukizitaja watoto wanashangaa. Wao wanataka kusiki xx english medium. Hii imesababisha hata wahuni kuanzisha vishule vya ajabu ajabu na kuvita english medium. Mtoto anafika la tatu orodha ya pili hajui ila ugandan english anaijua vizuri tu. Huu ni upuuzi unaofanywa na wizara ya elimu. Ukiangalia matokeo ya watoto karibu wote wamefeli hesabu, why?
 
Mkuu umenena vyema.., kwamtazamo wangu hata hizo tunazoziita inglish medium ni JANGA.
Mfano hai: Mtoto wa dada angu anaingia darasa la tano mwakani, anasoma the so called english medium lkn ukimpa gazeti la kiswahili hawezi kusoma.., ila kiswahili anaongea vizuri! Sasa unajiuliza wanafundisha hata kiswahili kwa mtindo wa kingereza au..??!
Pia mazingira ya nyingi ya hizo shule ni machafu.., kuanzia vyooni..., ukipita kwa nje utaziona zinapendeza ila ingia ndani utashangaa!!
Ni mfano tu waungwana msinitoe macho.
 
Back
Top Bottom