Nakula lakini sipati choo, nkipata nikidoogo tena baada ya siku mbili.

Apr 6, 2012
97
34
Jamani naombeni msaada wa haraka, chakula nakula kama kawaida ila choo sipati, nikipata nikidogo sana halafu kinatoa harufu na upatikanaji wenyewe ni washida tena baada ya siku mbili. Nilikwenda hospital wakapima choo wakaniambia ninaminyoo, nikapewa albendazone doze, nimemaliza lakini hakuna ahueni. Msaada please!
 
Pole kaka... Kula mapapai ya kutosha, maji na mboga za majani fanya kama diet kwa siku kadhaa! Bt unahitaji kuonwa na mtaalam coz constipation ni zaidi yakuwa na minyoo sometimes! Maziwa ya mgando huwa yanasaidia sana!
 
Jamani naombeni msaada wa haraka, chakula nakula kama kawaida ila choo sipati, nikipata nikidogo sana halafu kinatoa harufu na upatikanaji wenyewe ni washida tena baada ya siku mbili. Nilikwenda hospital wakapima choo wakaniambia ninaminyoo, nikapewa albendazone doze, nimemaliza lakini hakuna ahueni. Msaada please!

Mkuu dawa yao ni ndogo sana kama upo dar fika katika maduka ya madawa ya kienyeji ukifika uliza kitu kinaitwa habat muluk hizi ni aina ya nuts ukubwa wake ni kubwa kidogo zaid ya punje ya ngano nzima na dozi yake ikiwezekana ikate mara nne halafu anza na kipande kimoja ila chukuwa ii tahadhari mara ulapo hii kitu usirande rande mitaani pendelea kula usiku ama week end ukiwa umetulia nyumbani bila kusahau unatafuna tu kama karanga halafu unasukumia na maji , tatizo lako litakwisha mkuu utaharisha mpaka mpaka basi na kawaida haichukuwi muda utaona matokeo yake.

usije ukadharau ukaona ni chembe ndogo ukasema unakula yote utakuja lala chooni. mkuu utasafisha tumbo lote pia kunywa maji mengi kidogo kwani shughuli yake inakua kubwa.
 
Mkuu altaaf Dawa hiyo ya Habat mulku unataka aharishe sana siku anayotaka kunywa hiyo Dawa?Na ikiwezekana anywe hiyo Dawa Habat mulku aitwange kisha achemshe na maziwaya moto anywe lakini asiwe mbali Toilet choo maana anaweza kujiharishia mwilini mwake.

Mkuu.@SEMBE WA LUSANGA Ninakupa dawa ya kupata choo na njia Rahisi tu fanya hivi

Kwa Mtu Mgonjwa wa Maradhi yoyote inatakikana uwe unakunywa maji moto umoto wa chai au Maji ya ya Uvuguvugu unapo amka Asubuhi kabla ya kupiga mswaki anywe Glasi 2 za Maji ya moto na baada ya kupiga Mswaki anywe glasi 1 au 2 na kabla ya kunywa chai anywe Glasi moja ya maji moto kila siku afanye hivyo kwa wakati wa asubuhi.

Na Wakati wa mchana Dakika 15 au dakika 30 kabla ya kula chakula cha mchana unywe maji ya moto au Maji ya Uvuguvugu Glasi 1.

Na Wakati wa chakula cha Usiku unatakiwa unywe Maji ya moto au ya Uvuguvugu Glasi 2 kabla ya kula chakula cha usiku.

na unywe Maji ya moto au Ya Uvuguvugu Glasi 1 kabla ya kwenda kulala usiku. Na kila usiku unapo taka kulala kula tunda moja tu la Apple kwa kiswahili linaitwa Tufaha litakusaidia kufunguwa hicho choo chako Tumia hiyo dawa kisha uje hapa unipe feedback.
1282852892989866508apple-grn.jpg

Pole sana ndg, kila tatizo hapa duniani lina suluhisho lake, kma bado ni tatizo basi waweza pata chai ya TIENS( TIENS antilipemic lipid management tea) kazi yake mwilini ni:-
- husaidia kuponya magonjwa mengi sana
- husasafisha tumbo na kusaidia chakula kusagwa vizuri
- inazuia saratani ya tumbo
- kuondoa mafuta mabaya mwilini.
- huponya vidonda, maumivu na huondoa uchafu
- humaliza magonjwa ya ini
- inaongeza nguvu kupigana na magonjwa
- ni nzuri kwaupunguza mwili
- huwasaidia watu wenye matatizo ya kukosa usingizi
- nzuri sana kwa watu wenye UPUNGUFU WA KINGA MWILINI( UKIMWI)
- Nzuri kwa akina mama wenye matatizo ya hedhi( mzunguko kutoeleweka, fungus,maumivu ya tumbo nk)

NB: JITAHIDI KULA MATUNDA ANGALAU DK 15 KABLA YA KULA, MAHINDI YA KUCHOMWA, JUICE NA MBOGA ZA MAJANI KWA WINGI, EPUKA ULAJI WA SEMBE KWAN NI MAKAPI TU.

kwa tatizo lolote twaweza wasiliana nami kwa private message au kwa :-
TIENS HEALTH CONSULTANT AND DISTRIBUTOR
TEL NO. +255755569494
E-mail: ruhazwentaki@yahoo.com, ruhazwentaki@gmail.com
or visit: http://www.tiens.com, http://www.aftiens.com
 
Pole sana mkuu Ila kama walikushauri wenzangu ni sawa kabisa.

Chakuongezea Kuwa (natumia lugha nyepesi ili kila mtu aelewe):

Kutopata choo kunasababishwa na mambo mengi yafutayo:-
1. Mfumo na aina ya vyakula unavyokula
2. Mfumo na aina ya vinywaji unavyokunywa
3. Je unakula Mlo kamili kwa maana ya balanced diet?
4. Je unakunywa maji ya kutosha? 5. Je unafanya mazoezi?

Siamin sana ktk madawa ya kisasa na ninashauri yafuatayo:-
1. Hakikisha unakula aina tofauti tofauti za matunda mf papai na tango, parachichi, etc.
2. Hakikisha unakula vyakula na nafaka venye nyuzinyuzi (fibre) tena viwe vya kuchemsha mf; mihogo, magimbi, viazi, karanga, 3. Usile ugali uliopikwa kwa unga uliokobolewa.
4. Tumia Herbal tea na asali mf; Tangy KAZI yake mwilini ni kulainisha choo na ku ongeza mumeng'enyo wa chakula.
5. Hakikisha kila siku walau mala moja unapata mboga mboga za kutosha na isipikwe ikaiva sana na isiungwe kwa mafuta na vikorombwezo kibao, chukuchuku ni nzuri zaidi ukishindwa basi pika mboga yako (nyama au samaki) ikiisha iva Tia ktk hotpot then weka mboga yako (iliyosafishwa na kukatakatwa) juu ya mboga iliyoiva then vunga hotpot yako na acha kwa muda iive humo humo ndani ya hotpot (mchicha, spinach, Chinese, etc) mboga laini tu usije ukaweka Matembele au majani ya kunde hahahaha

Mwisho kabisa fanya mazoezi maana yatakusaidia kunya maji mengi najua ni tatizo la wengi ila jizoeze kuwa unakunywa kidogo kidogo na hakikisha uko nayo karibu pia sio mazoezi ya kukumiza mwili la hasha, unaweza hata kutembea tu kwa mwendo wa nusu Saa na kurudi.
 
Mimi na Tatizo hilo na nime gundua sababu 1

1. Punguza kula wali -Mchele si mzuri sana kwa choo na uzito unabaki sana tumboni.
2. Kula matunda mengi yenye fiber Mananasi, maembe na maganda yake, n,k
3. Tumia Ole Vera kidogo tu kila siku inasaida sana kwenye choo. Tumia kidogo tu lakini kila siku asubuhi zinauzwa madukani achan na za kienyeji.
4. Yote yakikataa inabidi uanze na majani ya chai ya kichina yanaitwa green tea diaters nenda kwenye store za kichina utapata haya yatakurekebisha lakini anza na vitu vya asili kwanza
 
Back
Top Bottom