Nakula kiasi kidogo cha chakula, sipendi nataka kula sana nifanyaje?

Oct 9, 2010
13
3
Kwa muda mrefu sasa nakula chakula kidogo sana matokeo yake sinenepi, kama unanijua uwezi kunitofausha wakati nipo shule na sasa ninavyofanya kazi naomba kusaidiwa mawazo.
 
Unajitafutia shida ya kiafya ndugu yangu?

Unene unautafuta wa nini wakati wengine tunatafuta kuupoteza bila mafanikio?
 
We mwenyewe umeshasema unakula kidogo sana, sasa unategemea kunenepa? Kama unataka kunenepa kula ipasavyo.
 
kapime minyoo na hasa minyoo aina ya gardia..... nilikua na tatizo kama lako lakin baada ya tiba ni mwendo wa kula kama kiwavi
 
Kweli unachekesha.wenzio wanatamani wapungue wewe unautafuta unene? kwani unaumwa ukiwa mwembamba?
 
Kwa muda mrefu sasa nakula chakula kidogo sana matokeo yake sinenepi, kama unanijua uwezi kunitofausha wakati nipo shule na sasa ninavyofanya kazi naomba kusaidiwa mawazo.

Hahhahahaha, usilolijua ni sawa na usiku wa giza.

Kwanza shukuru kwa jinsi ulivyo kama unataka kuongezeka utaongezeka wala usilazimishe. Ukinenepa apetite inakua juuu hakuna
mfano ukitaka kupunguza kula ama unene gharama yake ni kubwa sana.

lala vya kutosha, kunywa maji mengi, kula matunda na fanya mazoezi mwili utanawiri mashavu yatakaa vema. USITAKE UNENE
 
Back
Top Bottom