Nakuja na swali kwa dada zangu 40+

Joel360

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
981
631
Habari za muda huu wanachama wenzangu wa Jamiiforums.

Mimi kuna jambo huwa linanitatiza SANA. Huwa linanitatiza kiasi cha kunipa maswali mengi sana kichwani. Na leo naomba niwaulize dada zangu wa 45+.

Unakuta kuna mama/dada wa miaka zaidi ya 40 au 45 au pengine hata miaka 50 anajaribu kuanzisha mahusiano na kijana au pengine mtu mzima mwenzie. Of course sio mbaya kuanzisha mahusiano kama una nia njema ya kufunga ndoa.

Lakini kwa mwanamke wa umri huo(45 mpaka 50 na kuendelea) huwa anatafuta nini hasa kwenye suala la mahusiano/ndoa ?

Kwanini nimeuliza hivyo ? Kwa sababu.
i. Mwanamke wa umri huo wengi wao huwa hawapati tena hedhi hivyo hawawezi kuzaa lakini pia hata hamu ya ngono unakuta hana tena kutokana na kukoma kwa hedhi.

Sasa anaanzisha mahusiano ya kazi gani ?

ii. Wanawake wa umri huo wengi unakuta TAYARI ana watoto. Mimi nnachokijua ni kuwa mtoto anachukua nafasi ya kwanza kwa mwanamke. Tayari ana mtoto/watoto sasa anataka nini kingine ?

Ukichukua sababu hii ukijumlisha na kukoma kwa hedhi kunakofanya kukosa hamu ya ngono ndo kunaponipa maswali; Sasa mwanamke wa umri huo unataka mahusiano ya nini ?
Hedhi hupati. (Huwezi kuzaa tena)
Hamu ya ngono huna(sidhani kama ngono itakufurahisha).
Watoto yawezekana tayari unao. Kama huna sidhani kama utapata baada ya hedhi kukoma.

Sasa niambie wewe unataka mahusiano ya nini ?
Utakuwa umenielimisha pakubwa sana.

Nashukuru sana kwa watakaonijibu. Mniwie radhi kama nimetumia lugha kali sana, nimeamua kuwa muwazi kwa sababu nataka kujua kwanini hasa unakuta mwanamke mtu mzima anakutongoza au kukutega.
 
Muheshimiwa, Mahusiano ya Mwanaume na Mwanamke ni zaidi ya kupata watoto japo jambo la msingi kijamii na kiutamaduni ni kuongeza familia, lakini baada ya hapo kuna upweke na hali hii huanza hasa watoto wanapokuwa wakubwa na kuondoka nyumbani kwenda kuanza maisha yao iwe kuoa ama kuolewa.

Lakini pia siyo wanawake wote wanakoma hedhi baada ya kufikisha 45+ , pia siyo lazima edhi inapokoma kwamba na hamu inaisha (haya ni mambo mawili tofauti) ndiyo maana kuna wanawake bado wanakwenda edhini lakini hawana hamu ya tendo kutegemea na yepi yamemsibu (hii hujumuisha magonjwa na sarakasi katika mahusiano yaliyopita na yaliyopo)

Hivyo basi jambo la kuzingatia ni kuwa sisi wanaume na wanawake tunahitajiana sana, ukisikia mtu anasema hana haja ya kuwa na mwenzi tambua kuwa hicho ni kiburi cha uzima na afya. Akifika uzeeni akaanza kuhisi upweke ndipo ataona haja ya kuwa na mwenzake.

Sasa usishangae kusikia mama wa miaka 60 kaolewa, wanatafuta kampani kushinda upweke maana hata kama ana watoto wapo makwao (wanajitegemea).
 
Nafikiri lisikutatize, ukizingatia halikuhusu. Mahitaji ya wanadamu yako pale pale.
Linanihusu ndugu. Kuna sister mmoja namzungusha toka last week. Nikiangalia age yake najiuliza maswali mengi sana
 
Linanihusu ndugu. Kuna sister mmoja namzungusha toka last week. Nikiangalia age yake najiuliza maswali mengi sana
Una umri huo nawe? Wanadamu wana mahitaji, sio lazima hayo unayoyafikiria wewe. La kama ni kuzaa, kuna mama anaitwa Janet Jackson, alianza kuzaa akiwa na miaka 50.
 
Mkuu....
Sio kila mahusiano yana maanisha kunyanduana.
Kuna mengi mazuri na faraja kwenye mahusiano, zaidi ya mjegejo.
Naomba nikukumbushe kwamba, upweke pia ni jambo linalo watafuna wamama/wababa wengi hasa wanapo kosa wenza. And by nature, mwanamke ni kiumbe ambae lazima aongozwe na mwanamume.
Mkuu, haujawai kuona mama mtumzima pengine amekwenda kusalimi wanawe huko mkoa wa mbali, then baada ya muda kidogo utamsikia anasema anataka kurudi nyumbani kwake(kwa mume wake)..?? Hiyo ni moja ya sababu za kiasili kwamba hawezi kukaa pekeyake.
Anyway, hata ivyo naona kama nakupa majibu makubwa yaliokupita umri, na swali lako limeegemeza akili yako kwenye kungonoka zaidi.
 
Uko darasa la ngapi??
So akija Bibi yako kukuambia amepata mchumba anaolewa ..
Utasema mchumba wa nini??
 
Nimeambiwa na baadhi ya wanawake wenyewe. Hamu ya ngono hukoma baada ya hedhi

Wamekudanganya siku hizi na technology hedhi inaenda mpk 70 years halafu nikutaarifu tu above 40s ndio wana hamu sana. Kama wewe ni mwanaume huwezi jua haya mambo na ndio maana ni rahisi kukutana mama wa 40s ana cheat coz kipindi hiki mme ndio ukute ana maradhi nyemelezi kama kisukari sasa kwa nini mama asitafute dogo dogo.
Kuna mbaba alikimbia mke mwenye 45 kisa ana hamu sana kua uyaone mwanangu.
Hao wanaokuambia waangalie vizuri lishe yao na maisha yao utapata majibu.
Kula vizuri, test vizuri be stress free hamu iko hata ukiwa na 60s
 
Mkuu....
Sio kila mahusiano yana maanisha kunyanduana.
Kuna mengi mazuri na faraja kwenye mahusiano, zaidi ya mjegejo.
Naomba nikukumbushe kwamba, upweke pia ni jambo linalo watafuna wamama/wababa wengi hasa wanapo kosa wenza. And by nature, mwanamke ni kiumbe ambae lazima aongozwe na mwanamume.
Mkuu, haujawai kuona mama mtumzima pengine amekwenda kusalimi wanawe huko mkoa wa mbali, then baada ya muda kidogo utamsikia anasema anataka kurudi nyumbani kwake(kwa mume wake)..?? Hiyo ni moja ya sababu za kiasili kwamba hawezi kukaa pekeyake.
Anyway, hata ivyo naona kama nakupa majibu makubwa yaliokupita umri, na swali lako limeegemeza akili yako kwenye kungonoka zaidi.
Asante kwa kunielewesha.
 
Uko darasa la ngapi??
So akija Bibi yako kukuambia amepata mchumba anaolewa ..
Utasema mchumba wa nini??
Mimi nimemaliza chuo mda mrefu sana. Kama miaka 9 iliyopita. Sasa hilo la nipo darasa la ngapi sijui unamaanisha nini.
 
Back
Top Bottom