Nakuja Dar es Salaam kwa mara ya kwanza, nipeni muongozo huu

Umesoma Ndanda mimi Songea Boys,ushauri wangu ni huo fanya Research,lakini Biashara hizi za mazao hasa kwa Kariakoo ni kwamba unafikisha mzigo unamkabidhi Dalali unaondoka,unaanza kuwasiliana na dalali kwa simu kumuuliza Biashara inaendaje(kwa kifupi unakuwa kama unamnyenyekea/unajipendekeza)kumuomba aupe first priority mzigo wako maana unapomkabidhi utamkuta ana mzigo wa watu wengine kama wako nao wanahitaji awauzie,hivyo ukiwa na sehemu ya kuuweka mzigo wako tena ya bure,kisha ukawa Supplier mwenyewe kwa wauzaji wa masoko ya mitaani utafanikiwa,muhimu uwe na bei nzuri chini ya ile ya wauzaji wa Kariakoo
Ilo ndilo lengu langu Mkubwa, ukweli ni kwamba Nina access ya kupata hata million 5 anytime lakini nimeona nianze kama underdog niangalie soko lilivyo nione biashara inaendaje nikishaanza kuona mafanikio na nikijua njia zote za biashara basi naweza nikaingiza mtaji woote.
 
Kaka nitakusaidia kwa uchache saaana maana Mimi pia nimekuja dar nikitokea kanda ya ziwa mkoa wa Geita, baba yangu pia ni mvuvi wa dagaa ziwa ziwa Victoria upande wa kasamwa butundwe, nitakupa mwongozo na changamoto nilizo kutana nazo Mimi kijana mwenzako. ni PM
Ungeweka Waz mambo pm unaficha nn wakat hapa ni sawa na darasa!
 
Temeke lipo soko kubwa linaitwa stereo, lipo karibu na hositali ya wilaya ya Temeke, Mwembe Yanga na chuo cha bandari.
Shukrani mkuu, nikija nitazunguka poote nione afadhali hiko wapi lengo langu ni kama alivyosema broo hapo juu nataka niuze mwenyewe na kuwapa wale wafanya biashara sokoni (niwe supplier) nikisema nimpe dalali nitabaki kuumia tu mzigo mwenyewe ni ndogo sio Mkubwa.
 
Wavivu Summary:

Kijana wa Kisukuma, hajawahi kufika Dar, ni graduate wa Education, ana Million 1 taslim, anataka kuja Dar kutafuta maisha6.

Kwa kuanza angependa kuuza Dagaa wakavu (dagaa kauzu), anachoomba mumtafutie (1) nyumba ya kupanga maenye nyumba anapokea kodi kwa mwezi (2) mahala pa kuuzia dagaa (meza)
WONDERFUL
 
Tafuta godoro na chandarua,nitakupa chumba cha kuishi bure kipo Madale,ni nyumba yangu bado sijaikamilisha,unaweza kujibana hapo kwa muda mpambanaji
Watu wenye moyo kama wako wapo wachache sana, nakuombea uzidi kubarikiwa mkuu.
 
Good idea. Dagaa zinatoka sana sehemu za uswazi. Huku Masaki wanakula dagaa wa kopo from India..
Hata hao wa masaki wananunuwa dagaa hao wa ziwa Victoria waliosafishwa vizuri na kukaangwa na kupack kwenye vifungashio utawakuta super market.

Ukishakaa vizuri kwenye hii biashara na kujuwa namna ya kulobby unapata tender ya kusupply supermarket na pia dagaa wana soko kubwa ulaya, hili linahitaji connection tu.
 
Wakuu habari!

Mimi ni mtanzania kijana nilie graduate chuo mwaka huu nikitokea mkoani kanda ya ziwa, kwanza niweke wazi kutokana na trend ya ajira ilivyo nchini nimeamua kupambana na kuhangaika mwenyewe katika nyanja ya kujiajiri maana nikitegemea ajira ya serikali naweza kufa njaa na ndoto zangu zisitimie maana umri pia unaenda, nimesoma education (science) naelewa ajira zitakuja lakini nataka niweke vyeti kabatini nipambane ajira zitanikuta mbele ya safari huko.

Katika maisha yangu ya kusoma ndoto yangu kubwa ni kufanya biashara ili niweze kujikwamua kiuchumi japo naelewa kwa sisi watoto wa maskini safari ni ndefu saana, nilipokua chuo nimefanikiwa kusave boom langu kwa kujibana saana nimefikisha 1 million. Najua kwa watu wengi hii Pesa ni ndogo na ni matumizi ya week tu au mwezi lakini kwangu ina maana kubwa sana maana naelewa inaenda kunikomboa.


Japo pia naelewa "safari ya maili 1000 uanza na step moja"

Idea yangu kuja kufanya dar ni hipi?

Naelewa Dar ni mji Mkubwa hata mzunguko kwa biashara ni Mkubwa pia, ninayo access ya kupata dagaa wakavu (dagaa kauzu) kutoka gosber kisiwani so idea yangu ni kuleta dagaa huko Dar ninao mtaji wa kuanza na gunia 10. Japo lengo langu kubwa ni kuleta nafaka zote pamoja na mafuta ya alizet though mtaji wangu ni mdogo nataka nijikite kwenye dagaa kwanza then mwangaza wa asubui ukishaonekana basi naweza fungua ofisi kubwa nianze kuleta hivyo vitu.

Nilitaka nifike dar kwanza nifanye research nizunguke kwenye masoko mbali mbali nataka niuze jumla kwa madalali na rejareja NIKIPATA MEZA SOKONI ITAKUA VIZURI (japo sijui nitapataje).

WAKUU KWA SABABU MTAJI WANGU NI MDOGO NA CHANGAMOTO YA DAR NI SEHEMU YA KUKAA NA KUKAA KWA MTU NI NGUMU KUTOKANA NA HALI YA MAISHA YALIVYO (kila mtu anashida zake)

Next week nakuja kufanya research ya maeneo kuongea na madalali na kutafuta eneo langu la kufanya kazi.

Nilikua natafuta chumba sehemu ya kujishikiza (sio kufikia kwa mtu) ambapo mwenye nyumba atanikubalia kulipa kodi ya Mwezi mmoja huku Mimi nikiendelea kufanya research zangu kuhusu hiyo biashara endapo nikipata godoro nitashukuru sana.

Asanteni.

Natumaini wewe ni Me, karibu mjini wazo zuri sana ila ukija utuoe mrejesho
 
pakia dagaa gunia zako 10 shusha bungoni sokoni dk zitachukuliwa na madalali...ili safari isiwe ya kuja tu bure ukiuza rudi ukiwa umeacha connections ata ukiwa kanda ya ziwa unatuma dagaa zako
 
pakia dagaa gunia zako 10 shusha bungoni sokoni dk zitachukuliwa na madalali...ili safari isiwe ya kuja tu bure ukiuza rudi ukiwa umeacha connections ata ukiwa kanda ya ziwa unatuma dagaa z
Shukrani mkuu lakini Nina swali kidogo hapo bungoni ni wapi? (Eneo ambalo ni maarufu mfano temeke, kariakoo n.k) then hapo bungoni hao madalali watanipatia Pesa baada ya mda gani? Au ni kusubiri week 2-3 kama kaka alivyoniambia hapo juu kuhusu wafanyabiashara wa kariakoo?.

Asante
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Shukrani mkuu lakini Nina swali kidogo hapo bungoni ni wapi? (Eneo ambalo ni maarufu mfano temeke, kariakoo n.k) then hapo bungoni hao madalali watanipatia Pesa baada ya mda gani? Au ni kusubiri week 2-3 kama kaka alivyoniambia hapo juu kuhusu wafanyabiashara wa kariakoo?.

Asante
sorry sio bungoni ni ilala boma (ilala) japo naweza kuwa nimekosea jina ila inshort ni ilala sokoni ni pazuri zaidi kuliko Tandika ,(temeke) ..wanaweza kukupa pesa cash au wengine wenye mizigo mkubwa wanapewa kwa mda mliokubaliana
 
Ongera kijana kwa kumaliza hiyo degree yako. Lakin ongera kubwa Sana kwa kuwa na mtazamo mwingine mbadala wa ajira tofauti na kuzunguka na bahasha mjin. nafurah Sana mtu anayewaza Kama wewe.

Pamoja na kukupongeza naomba nikuchalenge kidogo na kukupa ushaur kidogo. Ukitaka ushauri zaid nitakupa hapa live Sina aja ya PM.

Kijana mwanza inafursa nyingi Sana,kwann wewe umewaza biashara ya dagaa tu?

Kwann umewaza kuleta dagaa kuuza dar esalaam tu hakuna mikoa mingine zaidi ya dar? Hujui watu wengi wanaleta bidhaaa dar na hivyo wakat mwingine supply kuwa kubwa na price kushuka?

Kijana visiwa ulivyotaja kupata dagaa, kwann hukuwaza kuja dar kuchukua mzgo mdogo Kama urembo na nguo za kike kuleta uko mwz visiwan uko Goziba, Ghana n.k na kuuza bei kubwa?

Sasa kwa kuwa moyo wako umependa dagaa, wacha na mm nikushauri kwa upande huo wa kidagaa dagaa Zaid.

1.Ukija dar kutafuta soko la dagaa usije na sample moja. Njoo na sample 3 za dagaa maana kati ya hz 3, lazma moja itatiki vizuri.

1.Sample ya kwanza njoo na dagaa wakavu uliyo sema. Lakin kwa dar, jitahidi kununua dagaa walio anikwa kwenye buti au mwamba. Usilete walio anikwa kwenye mchanga, kwa dar unaweza kupata wateja wachache Ila kwa mikoa mingine Kama songea Haina shida.

2.Sample ya pili, njoo na dagaa walio kaangwa kwa mafuta. Wana anikwa kwenye vichanja, then wanakaangwa. Kwa dar utapata wateja, Ila kwa njombe, mbeya, makambako wateja ndo wengi wa sample no 2.

3. Sample ya 3, njoo na dagaa wa chakula cha kuku. Ukiwa dar kwsbb mtaji wako ni mdogo, tafuta masoko kwenye maduka ya vyakula vya kuku au kwa wafugaji wenyewe. Usiende viwandani.

Kwenye sample hizo, ukiwa na comtment na kumtanguliza Mungu. Mtaji utapanda. Ukiitaji kujua ni jinsi gan unaweza kutuma ata gunia 5, kutoka mwanza hadi dar bila ata wewe kusafiri utaniuliza...

Kwenye sample no 3, ya chakula ya kuku, ongeza na uduvi, njoo na uduvi utapata soko.

Kuhusu kupanga chumba, usikubali kupewa chumba au nyumba bure na mtu yeyote. Mwambie mkubaliane ata umlipe helf 10 kwa mwz lakin si bure. Itapendeza ukilipa miez 3 maana mpaka inaisha, utakuwa umepata muelekeo ya biashara na kuona je ni dar kweli au siyo na je ni dagaa kwel au fursa nyingine.

Kwa dar si lazma huishi karibu na mjin, wee hishi pale ambapo bidhaa zako zinaweza kuuzika zaidi. Mfano Kama pale banana, gongo la mboto, mbagara pale rang 3 na kwingineko. Yaan penye changanyiken....

Kuhusu vibali vya serikali.
Hili dagaa zako zitoke mwanza kwenda mkoa wowote tz. Unatakiwa uwe na nyaraka kuu 4. Kwanza Lesen ya kukusanya samaki na mazao ya samaki. Gharama yake shs 30,000.unalipia na kupata tu hakuna mashart.

2. Lesen ya biashara, hii inatolewa na halmashauri. Gharama yake haizid 80,000 kwa biashara Kama yako.Na hawasumbui kuipata.

3.Cheti cha mlipa kod (tn) certificate, so utaenda TR na kupata tn bure. Na kwa mtaji wako, ukienda Kama mwezi huuu, watakupa TN tu na kukwambia mwakan January uende lasm kukadiriwa kodi..
Usiogope T.R.A ni waelewa Sana haswa pale na wewe ukiwa mkweli

Baada ya hapo, utalipia ushuru, wa dagaa zako. hapa sijui bei yake kwa gunia lakin ni kati ya shs 1000 had 2000 inategemeana na halimashauri.
Ukisha lipia ushuru, afisa uvuv atakupa kibali Cha kusafirisha nzgo wako. Na kibali hicho ni bure.

Kuzipata nyaraka hz ni rahis Sana na ni bei ngodo usiogope.

Kwa upande wa masoko kwa dar, umesema unataka kupata meza. Ni vizuri lakin pia unaweza kupata wateja wako wa viduka vidogo vidogo wa kuchukua gunia moja n.k.

Kuwa Makin Sana na madalal haswa wa pale ilala, na tandika.

Kwa upande wa dagaa na dar, ngoja niishie hapo kwanza nimekushauru kidagaa dagaa zaidi, Kama utakuwa na swali karibu mkuu.
 
Aise be careful,
Hiyo million yaweza kuingia mikononi mwa matapeli ukalia milele.

Usimwamini mtu hata mkono wako wa pili usiuamini.

Naweza kukuunga pa kufikia maeneo ya mbezi if you will not mind
 
Back
Top Bottom