Nakuja Dar es Salaam kwa mara ya kwanza, nipeni muongozo huu

Wavivu Summary:

Kijana wa Kisukuma, hajawahi kufika Dar, ni graduate wa Education, ana Million 1 taslim, anataka kuja Dar kutafuta maisha.

Kwa kuanza angependa kuuza Dagaa wakavu (dagaa kauzu), anachoomba mumtafutie (1) nyumba ya kupanga maenye nyumba anapokea kodi kwa mwezi (2) mahala pa kuuzia dagaa (meza)
Ahsante sana mkuu....

Kumbe ni hivi tu ndo akaamua kutuchapishia gazeti?
 
Kil la heri,

Naamini utafanikiwa ktk lengo lako hilo,

Ila kabla hujaingia ktk hiyo biashara ya dagaa,umetafiti soko la bidhaa lako likoje na vipindi vipi bei inakuwa nzuri au mbaya ili usiingie kichwakichwa. Maana yake inawezekana kwa sasa bei ikawa chini ukaua mtaji. Hilo ni angalizo tu
Ndio mkuu nimeshafanya utafiti kwa kusikia kwa watu nimeona haitoshi ndio maana nataka nije mwenyewe nione na nikishapata meza yangu itakua rahisi kuona biashara ilivyo.
 
Usisahau kujipanga kishirikina pia maana Dar imekua kama ile mikoa iliyosifika kwa uchawi mathalani Kigoma, Sumbawanga na Tanga sasa wachawi na washirikina woote wamehamia Dar.
Uchawi hupo kila mahali tu, naelewa duniani kuna nguvu mbili zinazo operate nuru pamoja na Giza ina depend umesimama wapi...Nina mifano mingi ya watu waliofanikiwa bila ya ushirikina lakini asante.
 
Tatizo la watu unamsogeza baada ya mda anakubadilikia una kuta na nyumba kaiuza na kapotelea kisiojulikana, binaadamu shida sanaa.
Unahisi mkuu Mimi ni moja wapo wa watu wa hivyo? Si kweli ndio maana nimesema Pesa ya kodi kwa kuanzia ninayo labda godoro tu ndio itanigharimu.
 
Wala siyo uongo mkuu
Tutegemee kuona mabango ya KUTANA DR MALUMA KUTOKA KIGOMA ANATIBU......
katka Jiji la London

Mkuu uongo zambi wakazi wa Dar wanaendesha shughuri zao kwa kutegemea ushirikina na uchawi si wamaofisini Wala wafanyabiashara woote ni partcipant wakubwa wa waganga wa kienyeji inshort Dar inatisha kwa ushirikina, Mabinti wengi wanaroga ili wapendwe na watu wenye hela na Magari,

Mmmh naomba nisishushe nondo manaake hapa siyo mahala pake, tumuche kaka wawatu anaetaka kuja Dar kusaka ridhiki huenda kajipanga
Dar bila kujiimarisha kiwizard unaweza kuta we unafanyaga biashara ya kupoteza muda na pesa tu!

Kwanza lazma uonane na wataalamu unaona mtu anauza kiepe babkubwa unahisi kizembe vile kujaza kumbe watu wana michakato yao!

Ukikaa kizembe wanakukata upepo tu unashangaa gunia moja unakaa nalo mwezi mzima wakati mwenzio anashusha gunia 10 na kila siku anauza sio chini ya gunia 5
 
Mangole umeongea vema,kwanza pale Madale kuna soko japo sio kubwa,Tegeta,Bunju nk kuna masoko pia,wauzaji katika masoko na vibanda vya huko mitaani wote hufuata mzigo Kariakoo,hivyo huyu mtoa Mada anaweza akawa hata Supplier wao ili wasiende tena Kariakoo,tatizo la huyo wa Makete anawaza kila kitu Kariakoo tu,na tatizo la kupeleka mzigo Kariakoo ni lazima ukifika uukabidhi kwa dalali kisha akupe siku lini ukachukue pesa(nina uzoefu huo),dalali anaweza akakaa na mzigo wako wiki tatu anakwambia hajauza!!!hivyo ukiwa unauza mwenyewe kwa wauzaji wadogowadogo wa mtaani tena kwa bei ya chini ni vizuri kuliko kumuachia dalali
 
Hapo ndo vijana huwa wanafail unapata hela mkoa unakuja kuitumia dar hahahahah tuleteeee hyo hela tuongeze vipato
Mkuu umesoma mada kweli?...sileti hela au siji kula bata, naleta mzigo kutafuta hela sijaona utofauti wa dar na Mwanza kihivyo nimezaliwa Mwanza hapo sahara maisha yangu yote nimekua hapo, nimesoma ndanda high school nimepita dar safari zoote hizo kwahiyo naelewa principle zote za kuishi eneo lolote lile mkuu.
 
Pamoja na mengine ukija Dar achana na warembo au mashuga mammy wà Dar. Hao ndio wachawi wetu hapa mjini. Vumilia huu mwaka mmoja ndio umlete girlfriend wako huyo huyo uliyenae. Asije akakwambia mtu kwamba huyo Ni mshamba. After all Mimi naona k za washamba Ni tamu kuliko Hawa ma slay queen mumiani wanyonya damu.
Mkuu Mimi huko sipo kabisa, hahaha lengo ni moja tu kutafuta Pesa nimetoka mwanza mjini sio vijijini huko hao warembo na ma sugar mumy wapo tu
 
Mangole umeongea vema,kwanza pale Madale kuna soko japo sio kubwa,Tegeta,Bunju nk kuna masoko pia,wauzaji katika masoko na vibanda vya huko mitaani wote hufuata mzigo Kariakoo,hivyo huyu mtoa Mada anaweza akawa hata Supplier wao ili wasiende tena Kariakoo,tatizo la huyo wa Makete anawaza kila kitu Kariakoo tu,na tatizo la kupeleka mzigo Kariakoo ni lazima ukifika uukabidhi kwa dalali kisha akupe siku lini ukachukue pesa(nina uzoefu huo),dalali anaweza akakaa na mzigo wako wiki tatu anakwambia hajauza!!!hivyo ukiwa unauza mwenyewe kwa wauzaji wadogowadogo wa mtaani tena kwa bei ya chini ni vizuri kuliko kumuachia dalali
Exactly mkuu, nataka niuze mwenyewe jumla pamoja na rejareja kumuachia dalali mzigo wangu wa kwanza anaweza kunipiga nikaishia kulalamika tu ndio maana nataka nije nifanye research mwenyewe kuna washikaji zangu na wapo soko la temeke (japo sipajui) Mimi nakuja kuangalia upepo pengine naelewa dar masoko ni mengi.
 
O
Dar bila kujiimarisha kiwizard unaweza kuta we unafanyaga biashara ya kupoteza muda na pesa tu!

Kwanza lazma uonane na wataalamu unaona mtu anauza kiepe babkubwa unahisi kizembe vile kujaza kumbe watu wana michakato yao!

Ukikaa kizembe wanakukata upepo tu unashangaa gunia moja unakaa nalo mwezi mzima wakati mwenzio anashusha gunia 10 na kila siku anauza sio chini ya gunia 5
Unajua kwanini nataka niuze jumla na rejareja?...kwa jumla nitawapa hao unaosema ma wizard wanaotumia mziziology Mimi nauza kwa rejareja sio kwamba sielewi mambo ya wizard lakini naamini katika Mungu...kwani hao waliofanikiwa wooooote wameroga?..
 
Exactly mkuu, nataka niuze mwenyewe jumla pamoja na rejareja kumuachia dalali mzigo wangu wa kwanza anaweza kunipiga nikaishia kulalamika tu ndio maana nataka nije nifanye research mwenyewe kuna washikaji zangu na wapo soko la temeke (japo sipajui) Mimi nakuja kuangalia upepo pengine naelewa dar masoko ni mengi.
Temeke lipo soko kubwa linaitwa stereo, lipo karibu na hospitali ya wilaya ya Temeke, Mwembe Yanga na chuo cha bandari.
 
Umesoma Ndanda mimi Songea Boys,ushauri wangu ni huo fanya Research,lakini Biashara hizi za mazao hasa kwa Kariakoo ni kwamba unafikisha mzigo unamkabidhi Dalali unaondoka,unaanza kuwasiliana na dalali kwa simu kumuuliza Biashara inaendaje(kwa kifupi unakuwa kama unamnyenyekea/unajipendekeza)kumuomba aupe first priority mzigo wako maana unapomkabidhi utamkuta ana mzigo wa watu wengine kama wako nao wanahitaji awauzie,hivyo ukiwa na sehemu ya kuuweka mzigo wako tena ya bure,kisha ukawa Supplier mwenyewe kwa wauzaji wa masoko ya mitaani utafanikiwa,muhimu uwe na bei nzuri chini ya ile ya wauzaji wa Kariakoo
 
Ajira zitakuja mbele
Nani kakudanganya?
Hahaha mkuu nimepata ajira ya kufundisha japo malipo ni madogo lakini zipo nyingi nyiingi nimeona niachane nazo nipambane mwenyewe, nimesoma education physics, mathematics (PM)....magap yako na mimepata lakini naona nifate hobby yangu kwanza.
 
Fanya ivi kaka mpe mtoa mada chumba Cha kufikia Cha bure kilicho karibu na kariakoo. Au mpe hifadhi unapo ishi wewe tuachane na malumbano ya ajabu.
Unademka tu bure, hakuna sehemu kwenye maelezo yake mtoa mada alipoomba msaada wa chumba cha kufikia au kukaa kwa mtu.

Mtoa mada ni mtu anayejitambuwa kwenye maelezo yake, anahitaji kuwa independent, msaada anaotaka hapa ni connection tu.
 
Back
Top Bottom