Nakuja Dar es Salaam kwa mara ya kwanza, nipeni muongozo huu

Optimists

JF-Expert Member
Oct 17, 2021
278
686
Wakuu habari!

Mimi ni mtanzania kijana nilie graduate chuo mwaka huu nikitokea mkoani kanda ya ziwa, kwanza niweke wazi kutokana na trend ya ajira ilivyo nchini nimeamua kupambana na kuhangaika mwenyewe katika nyanja ya kujiajiri maana nikitegemea ajira ya serikali naweza kufa njaa na ndoto zangu zisitimie maana umri pia unaenda, nimesoma education (science) naelewa ajira zitakuja lakini nataka niweke vyeti kabatini nipambane ajira zitanikuta mbele ya safari huko.

Katika maisha yangu ya kusoma ndoto yangu kubwa ni kufanya biashara ili niweze kujikwamua kiuchumi japo naelewa kwa sisi watoto wa maskini safari ni ndefu saana, nilipokua chuo nimefanikiwa kusave boom langu kwa kujibana saana nimefikisha 1 million. Najua kwa watu wengi hii Pesa ni ndogo na ni matumizi ya week tu au mwezi lakini kwangu ina maana kubwa sana maana naelewa inaenda kunikomboa.


Japo pia naelewa "safari ya maili 1000 uanza na step moja"

Idea yangu kuja kufanya dar ni hipi?

Naelewa Dar ni mji Mkubwa hata mzunguko kwa biashara ni Mkubwa pia, ninayo access ya kupata dagaa wakavu (dagaa kauzu) kutoka gosber kisiwani so idea yangu ni kuleta dagaa huko Dar ninao mtaji wa kuanza na gunia 10. Japo lengo langu kubwa ni kuleta nafaka zote pamoja na mafuta ya alizet though mtaji wangu ni mdogo nataka nijikite kwenye dagaa kwanza then mwangaza wa asubui ukishaonekana basi naweza fungua ofisi kubwa nianze kuleta hivyo vitu.

Nilitaka nifike dar kwanza nifanye research nizunguke kwenye masoko mbali mbali nataka niuze jumla kwa madalali na rejareja NIKIPATA MEZA SOKONI ITAKUA VIZURI (japo sijui nitapataje).

WAKUU KWA SABABU MTAJI WANGU NI MDOGO NA CHANGAMOTO YA DAR NI SEHEMU YA KUKAA NA KUKAA KWA MTU NI NGUMU KUTOKANA NA HALI YA MAISHA YALIVYO (kila mtu anashida zake)

Next week nakuja kufanya research ya maeneo kuongea na madalali na kutafuta eneo langu la kufanya kazi.

Nilikua natafuta chumba sehemu ya kujishikiza (sio kufikia kwa mtu) ambapo mwenye nyumba atanikubalia kulipa kodi ya Mwezi mmoja huku Mimi nikiendelea kufanya research zangu kuhusu hiyo biashara endapo nikipata godoro nitashukuru sana.

Asanteni.

FB_IMG_1624375535315.jpg


UPDATE

Wakuu nimefanikiwa kuingia jijini dar as salaam Nina kama week mbili hivi nimefikia kwa rafiki yangu kibaha...
Kama nilivyokua nimeeleza hapo awali niliingia kutafuta masoko ya Dagaa, nimefanikiwa kuzunguka masoko yoote makubwa hapa kuanzia mabibo, tandale Sokoni , stereo temeke, tandika pamoja na mbagala n.k

Changamoto

Changamoto kubwa nilioipata huku ni kwamba wafanyabiashara wa huku wengi wanachukulia Mzigo yao huko visiwani option pekee iliyokuepo ni kutafuta meza na Mimi pia kuuza kwa jumla na rejareja.
Sio rahisi maana pale mabibo walinambia nilipie meza kodi 70,000 per month na wanahitaji miezi 3, kule ilala sokoni meza zinafika mpaka laki moja kwa mwezi nikaangalia ujazo wangu(mtaji wangu) nikaona hapa sitatoboa.

Katika harakati za kuzunguka zunguka huku nikijiandaa kurudi home nikazunguka pale tandale Sokoni nikapata wazo jipya kuhusu biashara ya nafaka.

Japo mtaji wangu ni mdogo lakini pale sihitaji meza, wala mizani n.k na wazo nililolipata ni kuhusu biashara ya Mchele kwamba unachukua mashambani then unawapa madalali wanakuzia wanakupa hela (wanakuuzia)..

Japo faida yake ni ndogo nikaona sio busara kwanza kukimbia mji nifanye kujishikiza hapo nione.....waku kwa ground mambo sio mepesi kihivyo haswa kwa sisi graduate ambao hatuna mitaji sometimes unafikiri kukata tamaa lakini unajiuliza hata ukikata tamaa unamkatia nani?...

Let say umenunua mzigo mbeya kwa 1300 plans zako unafikiri uuze 1600/1700 hata urudishe mtaji wako ukifika Sokoni unakuta watu wanakwambia huu tunakupa 1400 tu so inakua ni changamoto.

Kwa sababu ya mtaji ni mdogo issue ninayoifanya ni delivery nimechukua mzigo ambao sio super saana bei yake ni moderate tu.
IMG-20211101-WA0029.jpg


Kwa ambaye anahitaji Mchele kutoka mbeya kwa bei ya 1800 around dsm nitafikisha popote pale pia maongezi yapo kwa atakaechukua nyingi.
Unaweza nitext normal au WhatsApp kwa 0757590836

Asanteni
 
Wavivu Summary:

Kijana wa Kisukuma, hajawahi kufika Dar, ni graduate wa Education, ana Million 1 taslim, anataka kuja Dar kutafuta maisha.

Kwa kuanza angependa kuuza Dagaa wakavu (dagaa kauzu), anachoomba mumtafutie (1) nyumba ya kupanga maenye nyumba anapokea kodi kwa mwezi (2) mahala pa kuuzia dagaa (meza)
 
Wavivu Summary:

Kijana wa Kisukuma, hajawahi kufika Dar, ni graduate wa Education, ana Million 1 taslim, anataka kuja Dar kutafuta maisha.

Kwa kuanza angependa kuuza Dagaa wakavu (dagaa kauzu), anachoomba mumtafutie (1) nyumba ya kupanga maenye nyumba anapokea kodi kwa mwezi (2) mahala pa kuuzia dagaa (meza)
umeturahisishia sana
 
Kil la heri,

Naamini utafanikiwa ktk lengo lako hilo,

Ila kabla hujaingia ktk hiyo biashara ya dagaa,umetafiti soko la bidhaa lako likoje na vipindi vipi bei inakuwa nzuri au mbaya ili usiingie kichwakichwa. Maana yake inawezekana kwa sasa bei ikawa chini ukaua mtaji. Hilo ni angalizo tu
 
Mimi nipo Dar, nakushauri hicho chumba usichukuwe kilometers nyingi kufika city center.

Tena kutoka kwenye chumba kwenda city center iwe ni daladala moja na nauli isizidi sh 400/=

Chumba cha kawaida jiandae cha sh 30,000/= kwa mwezi, wengi wanataka miezi mitatu ulipe kwa pamoja then ikiisha hiyo miezi mitatu ndio unaweza kulipa mwezi mmoja mmoja.

Nadhani hapo umepata mwanga kidogo, ukiitaji maelezo zaidi karibu sana.
 
Kaka nitakusaidia kwa uchache saaana maana Mimi pia nimekuja dar nikitokea kanda ya ziwa mkoa wa Geita, baba yangu pia ni mvuvi wa dagaa ziwa ziwa Victoria upande wa kasamwa butundwe, nitakupa mwongozo na changamoto nilizo kutana nazo Mimi kijana mwenzako. ni PM
Hakuna member asiyekuwa na pm humu, tunaandika hadharani kwa faida ya wengine.

Pm ni baadaye mtu akijiridhisha nani wa kumsaidia, hizi pm zimeshaumiza watu humuhumu.
 
Achimwene wa Makete usiwe mpumbavu,sihitaji Mlinzi maana pale site hakuna kitu kinachoweza kuibiwa,lakini kama kuna mhitaji anayetaka kujibanza panafaa,na usafiri wa kufika Tegeta Kibaoni ni rahisi
Huyu jamaa inaonekana hajakutana na shida ya kukosa hifadhi, yeye Kama anasehem nzuri ya kulala ni Bora akae kimya Kuna watu huenda sehem wakiwa hawana ndugu na hata sent tano mfukoni na wanaishia kulala vibarazani kwa maduka ya watu. Tena nimemuomba sio kila comment anajibu niyingine awe anakaa kmya.
 
Back
Top Bottom