Nakufa naombeni msaada

Afadhari wewe unapenda udongo wa dukani, mke wangu yeye alikua anapenda ule udongo wa mchwa.... akikuta mti una mchwa basi atakwangua udongo hadi namuonea huruma.
 
Unaupungufu wa madini chuma meza dawa inaitwa fefo utaacha kula udongo
 
Asante kama ukihitaji ushaur wa haraka na wewe tafuta attention kama mie ili watu waukimbilie Uzi wakobila kichwa cha habari usingesoma ,hongera Kwa kukwazika panapo makaaliwa nikishusha mzigo ntakuPM utume permpers
Pole mama kijacho ila inaonekana clinic haukuhudhuria tokea awali.
Hapo ilitakiwa uwe unatumia folic acid kila siku..ila maadam ulishaenda na umepatiwa dawa basi jitahidi kuzitumia sawasawa. Bila shaka hako itakuwa ni ka baby girl
 
Habari wanajukwaa hili la JF,

Mimi ni mjamzito na ni ujauzito wangu wa kwanza, wakati ipo changa nilikua nasumbuliwa sana na morning stickiness hata maji nilikua sinywi, natema mate tu na kutapika harufu mbaya mbaya yani nilikonda sana kiasi nilikua naumwa Hadi mwanaume wangu akawa anaogopa akawa ananiambia kama haitaweza kuhandle situation tuitoe hakusema Kwa nia mbaya kwakua wote tulimuomba na kumdhamiria hichi kiumbe nafikiri ni kwakua umri wetu na wote hatujawahi kuwa na mtoto, mtoto wetu wa kwanza kwetu sote.

Nisiwachoshe kilichonifanya niandike ni hiki 2nd semester nikawa na ahueni angalau nakula matunda na chakula kiasi nadokoa dokoa hv hv Ila mate yalikua bado nilikua na kopo kabisa special ghafla nikaanza kupata hamu ya Udongo nikamwambia mwenzangu akaenda nitafutia (sipo nyumbani Tanzania ilibidi nigoogle akautafute masokoni lol) akaupata Ila mweupe na nikaridhika nao.

Tatizo likaanza nikishakula chakula udongo ndy kama tunda langu naushushia yani hata dk 5aimalizi toka nile nataka udongo na nnaula hasa hadi najihirumia nikawa Hadi nauficha na kujaribu kujiwekea limit lakin nafail nakumbuka Kuna siku uliisha nikasema nitajikaza na sitakula tena chakula Hadi kesho mana nikila lazima nile udongo else najitskia hovyo hamuwezi amin nilipata shida nilizunguka nyumba mzima usiku wa manane Hadi nilipopiga jicho jikoni kulikua na viazi vitamu vibichi yale maganda yake yanaudongo nikawa nabandua udongo nakula.

Mwezi ujao M/Mungu akijaalia ntajifungua InshaAllah Ila tangu juzi kiukweli najskia hovyo na nahisi kabisa na akili yangu inaniambia ni udongo nikila au nisipokula hali Sawa Ila nashindwa kuacha mwili unakosa nguvu na najua fika nimeula mwingi sana naombeni kujua kama ndy sababu ya kuhisi hovyo na je madhara ya Udongo ingawaje kesho InshaAllah nimepanga kama hali itakua hii niende hospital.

Asante I naombeni kujua madoctor

Sent from my Nokia 7.2 using JamiiForums mobile app
Wataalam watakuja kuelezea zaid ila kwa Mama mzazi au mjamzito...kuna hivi wanaitwa virutubisho..(hivi sio dawa ni virutubisho))... Vinasaidiaa sana wanaita MULTI-VITAMINS…..(complex).. Maana kutokana na nature ya mimba unaweza kuta unapenda kula chakula kisicho na vitamins sana na kukataa chakula chenye faida (sababu ya mabadiliko ya mwili) kwahiyo KUNYWA MULTI VITAMINS hizo shida zitaisha sana.,..ukienda kwa daktar NA kwennda pharmacy itasaidia sana.

Mungu wetu wote
 
Wakuu mimi nauliza endapo mama mjamzito hatopata vile vidonge vya mwanzo kabisa..kutakuwa na madhara yeyote kwa mtoto na kwake? Au akichelewa kupata hivyo vidonge.
 
Ujauzito wa mke wangu alikuwa anapenda Sana harufu ya moshi wa gari hivyo kila saa nikitoka kwenye ishu zangu anawasha gari anachukua mkeka then anakaa nyuma kwenye exoz .
 
Mkuu na huko nje ya nchi ( Ulaya) kuna udongo kumbe......
Ila mnatabu mpaka mgoogle, poleni sana wakuu.
Ukijifungua mtoto aje, kwa wajomba zake huku bongo.
 
Jaman dalili za mimba huonekana
Baada ya mda gani tangu mmetoka
6*6
 
Mwambie Yesu amejulika sana, hayupo rafiki kama Yesu
Mwambie Yesu sasax2
 
Back
Top Bottom