Nakufa mwenzenu. Tafadhali nisaidieni dawa ya uvimbe puani

Kig

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
1,076
456
Tafadhali nisaidieni jamani. Nina uvimbe puani kwa muda wa miaka 3 hasa Shimo la kulia la pua yangu.

Huu uvimbe ndani ya siku moja unaweza badilika hadi mara tatu. yaani kuna muda unaziba pua kabisa. kuna muda unapungua unakua mdogo halafu unajirudia na kuwa mkubwa.

Zamani nilikuwa sipati maumivu ila sasa nahisi maumivu kiasi. Nimekwenda hospitali mara nyingi lakini naambiwa eti ni hali ya kawaida. mara naambiwa ni alergy ingawa huwa siamini kama nina alergy yoyote. dawa ninazopewa ni za ku-spray ndani ya pua. nikispray uvimbe unapungua kiasi lakini baada ya muda unajirudia tena.

Naomba wataalamu mnisadie jamani ugonjwa huu unasababishwa na nini? tiba/ dawa yake ni ipi? Je inaweza kuwa kansa. Kama ni dalili ya kansa tafadhali nielekezeni jinsi ya kuushughulikia.

Duniani tuna dhiki, tusaidiane kimawazo na tutiane moyo.

Natanguliza shukrani.
 
Unahitaji kuonwa na ENT (Ear, Nose and Throat specialist) na sio daktari wa kawaida.
Pole sana ndugu
 
Mkuu pole sana naomba nikulize ulishawai kutoboa poa na kuweka hereni???
 
Hizo ni nasal polyps,siyo cancer unaweza kutolewa kwa operation na madaktari specialist wa ENT au unaweza kutumia dawa za kuunyausha na unapotea kabisa,njia ya pili ni kama siyo mkubwa sana na haukuletei matatizo makubwa.kama unaziba kabisa pua operation ndo njia sahihi .njoo kcmc tukutoe andaa laki 315 uingizwe kwenye fast track,dakika chache tu mambo yanakuwa safi.
 
hyo ni allergy tu. mi ninazo na nilishawah kwenda hosp wakasema ni allergy. so dawa ninazotumia ni antihistamine. pia OLBAS OIL ni nzuri. but go to the hospital.pole sana
 
Unahitaji kuonwa na ENT (Ear, Nose and Throat specialist) na sio daktari wa kawaida.
Pole sana ndugu


Nimeonana na nose specialist ndio aliniambia hili ni tatizo la kawaida na akasema niendelee kutumia dawa ya ku - spray. lakini bado tatizo lipo palepale na nahisi linaongezeka
 
Nimeonana na nose specialist ndio aliniambia hili ni tatizo la kawaida na akasema niendelee kutumia dawa ya ku - spray. lakini bado tatizo lipo palepale na nahisi linaongezeka

Kama una hakika ni ENT, tafuta second opinion kwa ENT mwingine na umueleze umeonana na mwingine na unataka kujihakikishia. Umsikie atasemaje. Otherwise, relax nauwaamini utashangaa utakuwa hujisikii tena. Itakuwa busara wakikuambia una allergy ya kitu gani ili uweze kukiepuka kamainawezekana.

Pole sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom