Nakubaliana na Waziri Simbachawene na mtangazaji Maulid Kitenge kuwa Mwamposa ametukosea sana kama Taifa kwa kukimbia baada ya tukio kule Moshi

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,196
25,516
Asubuhi ya leo (kwa mara ya kwanza), nilisikia taarifa ya kusikitisha ya vifo vya watu takribani 20 vilivyotokea kule Moshi, mkoani Kilimanjaro kwenye shughuli ya kukanyaga mafuta kwenye kongamano la kidini lililoandaliwa na kuratibiwa na Mtume Mwamposa almaarufu kama Bulldozer. Inasemekana kuwa watu hao walifariki kutokana na kukanyagana.

Nimemsikia Waziri mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani, Mhe. George Simbachawene akizungumzia kukamatwa kwa Mtume Mwamposa. Amesema kuwa Mtume huyo Mwamposa amekamatwa Dar es Salaam baada ya kusakwa kwa muda. Waziri akaeleza, pamoja na mambo mengine, kuwa mipango inafanywa kumsafirisha Mwamposa kwenda Moshi kwa mahojiano. Amesema vitendo vyake vinaashiria kuwa alihusika na tukio lile.

Habari hii pia imegusiwa kwenye kipindi cha uchambuzi wa magazeti kwenye Redio ya Wasafi kinachoongozwa na Mtangazaji nguli Maulid Kitenge. Kitenge amesikika akisema, kutokana na Mwamposa kukimbia baada ya tukio badala ya kubaki na kushughulikia suala lile, Mwamposa ametukosea sana. Nakubaliana naye. Kwanini akimbie na hata kusakwa baada ya tukio lililomhusu moja kwa moja? Kwanini asingebaki na kumaliza jambo lile akishirikiana na vyombo vya dola?

Kuna jambo la kutazamwa kwenye makongamano ya aina ile. Kama Taifa, tuna jambo la kujifunza kutokana na vifo vile vya wapendwa wetu. Rest in peace wapendwa wetu!
 
Back
Top Bottom