Nakubaliana na Spika wa Bunge Job Yustino Ndugai lakini si katika yote aliyoyasema jana

Ukitaka kuwa wa hovyo jiunganishe na kauli za mtu huyu.
Nilibahatika kufuatilia mkutano wa Spika Ndugai na Waandishi wa Habari alioufanya jana jijini Dar es Salaam. Nilifuatilia kuanzia maelezo yake;maswali aliyoulizwa;majibu yake na maswali aliyowauliza wauliza maswali.

Lipo jambo la kikatiba ambalo Spika Ndugai amelizungumza ili kujenga hoja yake kuwa kauli ya Prof. Assad juu ya udhaifu wa Bunge imemgusa hadi Rais Magufuli. Spika alisema kuwa Rais ni sehemu ya Bunge. Hilo nakubaliana na Spika Ndugai.

Lakini, katika utendaji wa Bunge, Rais huwa sehemu ya Bunge katika masuala mawili tu: katika utungaji wa Sheria na katika masuala ya kibajeti. Katika masuala mengine kama kuisimamia Serikali, Rais 'si' sehemu ya Bunge. Rais hawezi 'kujisimamia' mwenyewe akiwa sehemu ya Bunge na mkuu wa Serikali kwa upande mwingine.

Kauli ya Prof. Assad, kwa uelewa wangu, ililenga kwenye wajibu wa Bunge katika kuisimamia Serikali hasa katika kuhakikisha matumizi yanakuwa sawa na ufisadi unadhibitiwa. Katika hilo, Rais hawi sehemu ya Bunge. Hivyobasi, kauli ya Prof. Assad haikumhusu Rais Magufuli kama Spika Ndugai anavyotaka kutuaminisha.

Nasema tena kuwa kauli ya Prof. Assad haikumhusu Rais, Waziri Mkuu au Baraza la Mawaziri. Ililihusu Bunge katika muktadha na sura ya kuisimamia Serikali kwa kuisimamia na kutekeleza mapendekezo ya CAG kwenye Ripoti zake.

Si vyema kumleta Rais, Waziri Mkuu na Mawaziri kwenye sakata hili ili ionekane kuwa Prof. Assad amewakosea hata wakuu wake. Halafu, lugha ya staha iwe inatumika wakati wa kuipinga lugha inayodaiwa kuwa ni ya kuudhi. Vijembe na kejeli hazijengi.

Hakukuwa na haja ya kumshauri Prof. Assad kujiuzulu au kwenda kwa Rais kuzungumza naye kwa sababu mbili. Kwanza, azimio la Bunge limeshamwadhibu kwa kutofanya naye kazi na si kumshauri ajiuzulu. Pili, Prof. Assad hana mgogoro wowote na Rais ili akazungumze naye kwa kuomba radhi. Katika kuisimamia Serikali,Rais 'si' sehemu ya Bunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu japo bunge ni dhaifu na spika ni dhaifu sana lakini kwenye hoja ya kumwingiza Rais, hajakosea wala hakumwingiza kwa bahati mbaya. Hivi jambo kama hili lingeweza tokea kipindi cha Mwl JK? Hivi jambo kama hili lingetokea wakati wa Ben? Conflict kama hizi zinatokea sasa kwa sababu ni wakati wake kwa kuwa mazingira yana mbolea!
 
Kwa ukweli sioni kinacho sababisha malumbano haya yote, kwani mwisho wa siku bunge litajadili report hiyo ya CAG! either bunge linashikiana na Assad au la.
 
Mkuu japo bunge ni dhaifu na spika ni dhaifu sana lakini kwenye hoja ya kumwingiza Rais, hajakosea wala hakumwingiza kwa bahati mbaya. Hivi jambo kama hili lingeweza tokea kipindi cha Mwl JK? Hivi jambo kama hili lingetokea wakati wa Ben? Conflict kama hizi zinatokea sasa kwa sababu ni wakati wake kwa kuwa mazingira yana mbolea!
Si kweli Rais ni sehemu ya Bunge ila si mbunge..sasa CAG alifanya kazi ya sehem ya Rais ila si vinginevyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugai anahangaika kama kuku anayetaka kutaga. Hana lolote. Hii yote ni frustration ya kulamba matapishi yake maana aliapa "kutopokea report ya CAG'' yenye sign ya Prof. Alhaji Mussa Juma Assad.
 
Kabudi yupo upande wa Ndugai, Dr. Mahiga yupo zake kimya alivyo na busara atasimama upande wa Prof Assad kimoyo moyo
 
Mimi nadhani huyu subhover kawekwa mbele na mafisadi na huenda naye ni mmojawao! Haiwezekani rais anayeongoza kuupiga vita ufisadi kwa nguvu zake zote aburuzwe na subhover eti amchukie cag anayemsaidia kupigana vita hiyo!
Kumtumbukiza rais kwenye udhaifu wake ni udhaifu wa kiutendaji unaotakiwa kupigiwa kelele! Anatakiwa asithubutu hata kulitaja jina la rais kwani hamsaidii kupambana na mafisadi zaidi ya kuyalea! Kama ameshindwa kuongoza mjadala juu ya ripoti ya cag awaachie kina chenge na yeye akajifiche india kuupisha upepo huu mbaya!
Na ikimpendeza amwone rais akiwa na barua ya kuuachia usubhover mkononi aone kama rais atajiuliza mara mbili!
Aondoke tu aepushe mkanganyiko wa kikatiba anaouratibu kidhaifu!
 
Back
Top Bottom