Nakosa hamu ya kuoa matukio ninayoshuhudia kwa macho yangu ama kusimuliwa

kinundu

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
2,029
2,129
Wakuu swala la mapenzi kwa kizazi cha sasa imekua giza nene mno. Juzi nilienda mitaa flani ya mwenge kumtembelea ndugu yangu kwake.

Lakini mtu hakunyimi maneno anakunyima pesa akanidokeza ndugu yangu humu ndani kuna jamaa anakaa na mkewe lakini shughuli zote anafanya mwanaume.

Kufua chupi za msichana wake, brazia, taiti na vitu vingi na bila aibu jamaa anavianika nje kabisa, na akianza kufua anafulia nje.

Cha ajabu binti mwenyewe ni mdogo kabisa, jamaa mwenyewe ni kijana tena wote wanafanya kazi kampuni moja ya mawasiliao kama customer care.

Cha kushangaza asubuhi kuamka jamaa anakua wa kwanza yeye ataoga yeye na kumtengea maji mwanamke wake mi nilishikwa na butwaa iweje kijana mdogo hv aendeshwe na msichana mwenye rika kama lake?

AMA NDIO MAPENZI YA KISASA? WATAALAM FUNGUKENI.

Hivi ni;
1.Ushamba wa mapenzi?
2.Jamaa kupigwa match hajui vizuri?
3.Kawekewa limbwata?
4.Jamaa anakibamia?
 
Fatilia mambo yako mkuu, dunia hii haishi misongamano ukifatilia ya watu utadata.

Pia kumuwazia mwanaume mwenzio kwamba ana kibamia sio dalili nzuri huenda ipo siku utahitaji utafiti zaidi ili ujue undani kuhusu maumbile yake.
Kiukweli macho hayana pazia.. Bado kuna mabrother nimepanga kwao.. Wao waliowa wote wawili mtu na Mdogo wake lkipind hicho walikua napesa sanaa .

Bahati mbaya mkubwa huyo akatengenezewa zengwe kazi akaachishwa pesa ikapukutika na kubaki na kudunduriza bac mkewe akamkimbia... Now yupo yeye na mwanae tü... Hvyo hvyo kwa Mdogo wake... Napata ukakasi kwakweli
 
Unakosa hamu kwa sababu ya shida za wengine???

Hamna wenye raha??? Why wenye raha wasiwe ndio role model wako???

Ukijua sababu ya kuoa, utaoa tuu
Wenye raha kwakweli ni Wale wenye umri mkubwa kuliko sisi vijana... Ila karibia wengi wananipa simulizi ya mambo waliyokutana nayo.. Na kukimbiwa... Baada ya kipato kupukutika
 
Ukiendelea kuangalia mapenz ya watu na kuyafanyia mtihani daima hautaoa
Hakika ndiko ninako elekea maana ata bibi mmoja alinipa husia mjukuu wangu kwa sasa ukiona kuna wanawake 10 bac mmoja ndio wakuowa wengine takataka... Ndoa zilikuaga kwao ndio maana hadi leo nipo na babu yako...

Kwasasa labda mtakacho pata ni maradhi tuu... Kwakweli alizidi niongeze msongo wa mawazo
 
Hivi wanawake tulijisahau wapi hadi wanaume wamevamia fani yetu ya umbea kiasi hiki.
Huo sio umbea ni namna ya kubadirishana mawazo na jinsi ya kujinasua.... Ni jambo linalo tisha..... Tufanyeje tumsaidie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom