Nakiri Ole Sabaya kunishinda ujanja na kuweza kunidanganya. Nilimuona mzalendo kweli kweli

abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
1,386
2,000
Habar watanzania poleni kwa majukumu

Mpaka Sasa kichwa changu naona kipo tu kama mzigo sababu ubongo ulishindwa kuelewa chochote maana Sabaya nilimuona mzalendo Sana Mpaka nilimkingia kifua Mbele za watu kumbe nilikua namtetea Mwizi na mnyang’anyi

Pia, Sabaya katika watu 5 nilio waona wazalendo kweli kweli kumbe ndio walio kuwa hatari kwa ustawi wa nchi hii

Sabaya hajaweza kunidanganya mimi peke yangu am sure ni wengi tuliodanganyika na lawama zetu zote tunazipeleka kwa Wabunge tuliowachagua kushiriki hii Dhambi

Yani kila nikikaa mwenyewe nafikiria how niliruhusu kuwa mjinga kiasi kile pia Sabaya kanifungua kuwa huenda hata wale wazalendo wengine wa 4 nao walitudanganya

Nakiri kuwa sijawahi kuona watu waongo dunian zaid ya Hawa watu wa 5 pia wote mlio kuwa mnasema mkuu hakua mwanasiasa eo naomba niwapinge sababu hamna mwanasiasa kama yeye Tanzania sababu yeye pekee ndio kafanikiwa kudanganya watu kwa kiasi kikubwa

Hongera jeshi la Polisi pia ningependa kuwashaur usalama wa taifa kua next time kuwen Makin sababu ikija kutokea kiongoz mwenye propaganda kali Zaid ya izi zilizo pita am sure nch tutaipoteza sababu propaganda hizi tu zilizo pita zilinifanya niwe tayar kuingia hata Barabaran na sio mimi tu vijana wengi walikua tayar
 

King Bill

JF-Expert Member
Feb 8, 2021
685
1,000
Wewe ni kijana muungwana. Binadamu anayekiri mapungufu yake hadharani ni mtu anayejiami. Nakupongrza kwa hatua hii.

Ushauri wangu kwako,na watu wengine ambao mliingia kwenye mtego wa viongozi laghai kwa kutekwa na propaganda zao...anza kusaka ukweli(truth) ili ufanye informed judgement.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,278
2,000
"Vetting" kwa viongozi pale wateuliwapo ni mchakato muhimu sana, na unapaswa kufanyika kabla kiongozi mteule kuapishwa na kukabidhiwa ofisi za umma. Mamlaka za uteuzi huweza kufanya makosa na kumteua mtu kwa sababu za kimaslahi wanazozijua wao wenyewe nje ya vigezo stahili vya ushindani, weledi, stadi, ujuzi, elimu na uzoefu wa muhusika.

Mchakato huu unapaswa kuwekwa kiaheria, ili jopo la majaji liundwe na kuweza kujiridhisha juu ya sifa za kimaadili na kiuadilifu za kiongozi mteule. Kwa kufanya hivyo tutaepuka kupata viongozi ndezi kama huyu Lengai ole Sabaya.

Kwa masikitiko makubwa na kwa mara nyingine tena tunazidi kushuhudia na kutilia mashaka umakini katika teuzi dhaifu za mwendake hasa kwa viongozi vijana. Aliwadekeza mno wengine wakifanya matendo ya kifedhuli mbele ya macho yake huku yeye akifurahia.

Kwake wale waliowachapa watu viboko sawa! Waliowa waweka watu kolokoloni Kwa masaa 48 sawa! Kundi la watu wasiojulikana sawa! Waliotoa lugha za matusi na sizizokuwa za staha sawa! Kuharibu mali za watu sawa! Na mengine mengi yenye kufanana na haya.

Mwendazake! Mwendazake! Mwendazake! Kweli ulijaribu, kuthubutu ama hata kutamani kubadilisha katiba ya nchi na kuondoa ukomo wa uongozi!? Acha tu zibaki kuwa ni tetesi.
 

santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
2,154
2,000
Mkuu siyo Sabaya na hao mahero wako wanne tu, system na ccm yoooooote, ni hivyo ulivyo Sema!
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,583
2,000
IMG-20210604-WA0119.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom