Nakiri nimemkosea mwanaume mwenzangu

Habari wanajamii, poleni kwa majukumu ya kutwa nzima ya leo.

Jamani naombeni mnisaidie nini cha kufanya nana roho inaniuma sana kwa jambo hili. Kuna ndugu yangu naishi nae mtaa mmoja ila yeye ameo na ana watoto wawili. Mara nyingi huwa nakwenda kwake nahasa shemeji yeye huwa anata niende kula chakula kwake pindi ninapotoka kazini kwa kuwa mimi bado sijaoa so ananionea huruma kujipikia mwenyewe.

Sasa pale kwa huyu ndugu yangu kuna mpangaji ambaye anawatoto wawili mmoja ni binti mkuwa wa miaka 21 na mwingine ana miaka 13 kiujumla maisha yao si mazuri kila kitu wanamtegemea mama yao. Huyu binti mdogo anasoma form one pamoja na mtoto wa ndugu yangu.

Hawa watoto wamenizoea sana. Nikajikuta namhurumia sana huyu mtoto wa jirani wakati mwingine anakosa hata vifaa vya shule kutokana na hali yao ya kimaisha basi nikaamua kumnunulia baadhi ya vitu pia na hata pesa za tution namlipia mimi. Mama yake pamoja na dada yake wakanishukuru sana.

Sasa ikawa kila siku dadayake akaanza kuwa karibu na mimi na hatimaye tukawa marafiki wakubwa tu hadi kwangu akawa anakuja kilichokuwa kikimleta ni CD huwa anapenda sana kuangalia seasons kama mimi so anakuja kuchukuaga kwangu. Ila hatukuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi hata siku moja Mungu wangu ni shahidi.

Kumbe huyu dada alitolewa mahari na bwana mmoja hapa mtaani mimi sikufahamu hilo na wala yeye hakunambia. Mara nikamuona huyu dada akiwa mjamzito sikuhoji kitu na sikuwa na sababu ya kuhoji kwa hilo.

Kumbe likawa kosa kubwa sana mchumba wake akawa analalamika kuwa mimi natembea na mchumba wake mimi sikuwa na habari kwasababu mimi si mkaaji wa vijiweni mimi nikiingia nimeingia nikitoka nimetoka ukibahatika basi utanikuta kwa shemeji yangu so story za mitaani zikawa zinanipita.

Imefika wakati huyu dada kajifungua tena kwa oparetion na siku chache kabla ya kujifungua alikuja kwangu tuliongea sana kama kawaida yetu. Kilichotokea jamaa kamkataa mtoto anadai sio wake ni wangu mimi na hii leo ni siku ya 6 tangu ajifungue jamaa hajaenda kumuona mwanae. Dada wa watu analia anaomba nimsaidie kumwambia ukweli huyo jamaa. Shemeji ndo amenambia kila kitu kuhusu huyu jamaa.

Kinacho niuma zaidi mtu mwenyewe ni mlemavu masikini naumia sana moyoni sikutembea nae mimi hata mara moja jamini. Nitafanya nini ili niaminike wakati watu walikuwa wanamuona akija nyumbani kwangu?

NITAELEZA NINI MIMI WAPENDWA. NAJIONA MKOSAJI HASA MTU MWENYEWE KILEMA NITAANZIA WAPI KUMWAMBIA UKWELI .
NISAIDIENI MAWAZO YENU NDUGU ZANGU NIMEKWAMA HAPA.
mlemavu wa nini?
 
Mtafute huyo Baba wa mtoto kaa nae na mweleze Ukweli. Asikie kutoka kwako. Akubali au akatae ww haikuhusu. Na pia Mtoto alikua anaweza kuchukua Muonekano wa Baba yake halisi. Na jamaa akiona atajirud...

Inawezekana pia jamaa alikuwa hamtaki mwanamke na pia anakwepa Majukumu ya ubaba.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom