Albedo
JF-Expert Member
- Feb 24, 2008
- 5,559
- 1,452
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26 sasa, nimehitimu elimu yangu ya juu kwenye moja kati ya vyuo vikuu vilivyopo hapa mjini.
Nimelelewa kwenye familia ya wafanyakazi waajiriwa wa serikalini ambao ni maaskari polisi, hivyo basi maisha yangu yote nimeishi kwenye nyumba za laini za jeshi la polisi.
Kutokana na kuishi watu wengi kwenye eneo dogo, niliiga tabia za watoto wenzangu, tulikuwa tunaamka usiku na kuanza kupipita kwenye nyumba za majirani huku tukiangalia ni nyumba gani ambayo baba na mama mwenye nyumba wamelala usingizi wa wakubwa.
Nilikuwa mahiri sana wa kupiga deo hadi nikapewa jina la koziman.
Nimeendelea na tabia hiyo sugu kwa kipindi chote hicho tanghu nikiwa darasa la tatu hadi jana nilipofumaniwa kwa kuanguaka kutoka darini kwa mpangaji mwenzangu ambako nilipanda juu ya dari ili niwafaidi vizuri wakikamuana.
Baada ya kushtushwa na kishindo nikawa nimeumbuka kiasi kwamba leo naogopa kurudi jioni.
Naiomba mnisaidie ili niweze kuiacha kabisa tabia hii ambayo inanivunjia heshima kwenye jamii...
Nimejaribu nimeshindwa, ukifika tu usiku usingizi huwa unaniruka hadi nione watu wakilana mambo.
Nisaidieni mwana jamvi mwenzenu ili nipate kupona.
Nimeongea ukweli mtupu kutoka moyoni mwangu kwani mficha maradhi kifo kitamuumbua.
Naogopa nsije nkauawa kwa kupiga deo
Pole Mkuu Bujubuji tafuta hobie mkuu kama kuangalia Movie nk.
Tahadhari: Angalia wasije wakakutoboa macho ukafikiri wamezima Taa