Nakataa Hakuna mpasuko wa kidini!!

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
614
wana JF napinga kwa nguvu zote kuwa kuna mpasuko wa kidini katika nchi hii.!! tokea matokeo yatangazwe kuna visingizio vingi vinavyotolewa kutafuta mchawi aliyesabababisha Vyama fulani vidhani kuwa chanzo cha kukosa kura za kutosha ni sababu za kidini. Mimi hili nalikataa na nawaomba viongozi wanoeneza jambo hili waliache mara moja maana linapandikiza mbegu ambayo kama ikichipua na kumea na kwa bahati mbaya wanachi wakajichanganya kwa sababu yoyote wakaitafuna itakuwa hatari sana

Watanzania niwamoja na hatudhani kabisa kuwa tunatatizo hilo, shida yetu sisi ni kuona taifa hili likipiga hatua mbele si vinginevyo. aidha tanzania ya Enzi za mwalimu sio hii jamani watu wengi wanafahamu siasa ni nini, niko chini ya miguu yenu msitupeleke huko tafadhalini sana. toeni sababu zingine lakini hili la mpasuko wa kidini jamani halipo ila nyie ndio mnaotaka mlilete!!!!!!!
 
cheap politics ya ccm kwa kuwa background ya Slaa ni upadri, hawaangalii hata muundo wa chama kiuongozi. Kama ni udini cuf na ccm ndiyo wadini kupindukia? rejea mdahalo wa juzi ambapo hamad rashid na ndesa walijoke masuala ya udini wakiwa bungeni lakini hamad rashid kaichukua kama ajenda.

Sijui hofu yao ni nini wasio wa dini yao wakiwa active kwenye politics.
 
Religious sentiments origin zake sio grassroots; na sio Chadema, ni mbinu za wakubwa katika kutapatapa kwa kuwa waliona kuwa Dr. Slaa ni mwanasiasa na mwenye uelewa mkubwa na kwamba anapendeka na wananchi. Anayesemea wengine ni wachawi actually hao hao ndio wachawi, so wale waliosema Chadema kuna udini, hao hao ndio wanaoleta hizo religious sentiments na hata katika kutapatapa ili kupata kura za Waislamu mkuu akaahidi Waislamu ahadi ambazo ndizo zimeongeza kwa kasi hizo sentiments; na kwa sababu anajua kuwa kampeni zake zilijaa udini; ndipo siku ya hotuba yake kwa bunge "akajitetea" eti kuna udini, kumbe wao ndio waanzilishi, sasa anatafuta mchawi yupi tena? Shida ni kwamba CCM inafikiria Watanzania ni wale wa zama la kale; wa yes lord, yes master....nope, Watanzania tumefunguka na kwa sehemu kubwa we owe it to Chadema and Dr. Slaa
 
Hisia za kidini mie naziona hapa JF kuliko hata mitaani!JF kuna kejeli sana za kidini !
 
hisia za kidini mie naziona hapa jf kuliko hata mitaani!jf kuna kejeli sana za kidini !
mkuu baba mwenyenyumba ndo alisema udini upoo toka kipindi cha kampeni mapaka amepata uraisi, kisa slaa alikuwa padre.
Cdm inawakosesha usingizi ccm! Na waliumia sana wabunge walipotoka bungeni wanatabasamu lakini hawana furaha kabisa! Tabasam la mbwa!
 
Udini kwa maana ya watu kubaguana kwa misingi hiyo haupo,lakini mbegu aliyopanda JK na timu yake ya kampeni inaaza kuota na muda si mrefu itaanza kumea, hivi sasa CUF ndiyo wanaimwagilia maji ili ichipue vizuri. Lakini kama Mungu aishivyo wote waliohusika kumwaga sumu hii wataangamia.
 
Tena cha kusikitisha zaidi wanadai wanaoleta udini eti ni wakatoliki, wakati historia ya wakatoliki haisemi hivyo, maana hawa ndiyo waliojenga mahospitali mengi kuwahudumia watanzania wote( Bugando, Peramiho, Ndanda just tyo mention few), ndio waliojenga shule za kati na sekondari na kuwawezesha watanzania akiwemo JK kusoma bila kubaguliwa au kubadilishwa dini.Ndiyo leo wanafungua vyuo vikuu kila kona zikipewa jina la ST.Augustine( Mwanza, Mtwara, iRINGA, Ruvuma n.k) ambapo leo watanzania wote wanafaidibila ubaguzi. Ndio hao leo wanafungua bank ya mkombozi inayohudumia watanzania wote bila kubagua.

Historia ya wakatoliki haiko hivyo hapa Tanzania, waseme mengineeeeeeee!!!!!!!!!!.Lakini JK huyo aliwahi kusema kuwa bila wakatoliki leo angekuwa muuza Korosho chalinze, iweje leo awazushie wamisionari hawa kuwa wanaeneza udini wakati wamempa elimu bila kuingilia uhuru wake wa kuabudu??????.Watanzania tumsaidie kikwete kumkumbusha yawezekana anapotoshwa ama amesahau alikotoka
JK muogope mungu wako
 
udini upo, umeonekana na hata haufichiki . kwanini hao wanaojifanya wanauchungu na nchi hii huanza kelele wakiona rais ni muislam tu?

Haa hizo ni tafsiri potofu, watu wanapiga kelele iwapo Rais atekelezi vema majukumu yake, siyo kwa sababu ya dini yake. Na wanaokemea ni watanzania wote bila kujali dini zao. Mfano mzee Mwinyi alikemea pale Rais alipotoa vitisho kwa wafanyakazi
 
Tatizo vyuo vimefunguliwa na siku hizi kuna net vyuoni basi tabu tupu! Forum imejaa vitoto vya shule.
 
Inawezekana ukawepo ila ni kwa ngazi ipi? kwetu huku kwa walala njaa hatuna udini tunaazimana mboga kama kawaida na hata kwenye kushiriki kwenye mkubwa wa meza hakuna shida yeyote
 
Anold ASANTE SANA nakuunga mkono. Malaria sugu ni sawa tu wewe ni mdini sana huna tofauti na babu yako JK ambaye anazungumzia udini wakati Watu wa dini zote wamemwingiza madarakani sasa udini umetoka wapi? Ila CCT wakikemea utetezi wa mafisadi inageuka udini hatuwezi kukubaliana na siasa za chuki za kidini katika nchi hii. Nendeni Somalia au Arabuni wanakoishi na kula kwa misingi ya kidini.
 
wana JF napinga kwa nguvu zote kuwa kuna mpasuko wa kidini katika nchi hii.!! tokea matokeo yatangazwe kuna visingizio vingi vinavyotolewa kutafuta mchawi aliyesabababisha Vyama fulani vidhani kuwa chanzo cha kukosa kura za kutosha ni sababu za kidini. Mimi hili nalikataa na nawaomba viongozi wanoeneza jambo hili waliache mara moja maana linapandikiza mbegu ambayo kama ikichipua na kumea na kwa bahati mbaya wanachi wakajichanganya kwa sababu yoyote wakaitafuna itakuwa hatari sana

Watanzania niwamoja na hatudhani kabisa kuwa tunatatizo hilo, shida yetu sisi ni kuona taifa hili likipiga hatua mbele si vinginevyo. aidha tanzania ya Enzi za mwalimu sio hii jamani watu wengi wanafahamu siasa ni nini, niko chini ya miguu yenu msitupeleke huko tafadhalini sana. toeni sababu zingine lakini hili la mpasuko wa kidini jamani halipo ila nyie ndio mnaotaka mlilete!!!!!!!

Aliyesema ana vyanzo vingi vya taarifa.
 
tusirizarau inashangaza chama cha ccm kuingiza mahakama yakadhi kwenye iraniyauchaguzi sijajuwa kama hikichama kinataka kuwa chama chakiisiram rinarosemwa ripo ninashidwa kuerewa tunaperekwa wapi?
 
Anold ASANTE SANA nakuunga mkono. Malaria sugu ni sawa tu wewe ni mdini sana huna tofauti na babu yako JK ambaye anazungumzia udini wakati Watu wa dini zote wamemwingiza madarakani sasa udini umetoka wapi? Ila CCT wakikemea utetezi wa mafisadi inageuka udini hatuwezi kukubaliana na siasa za chuki za kidini katika nchi hii. Nendeni Somalia au Arabuni wanakoishi na kula kwa misingi ya kidini.

Mchango wako wenyewe umejaa udini alafu unajifanya hakuna udini.
 
udini upo, umeonekana na hata haufichiki . kwanini hao wanaojifanya wanauchungu na nchi hii huanza kelele wakiona rais ni muislam tu?

Usirahisishe mambo. JK alipogombea 2005 aliungwa mkono na wakristo wengi sana (nikiwa mmojawapo) kwa matumaini kwamba ataondoa mizizi ya ufisadi, jeuri na kibri ya CCM vilivyoneemeshwa chini ya Mkapa (Mkristo). Wengine walivuka mpaka na kumuita chaguo la Mungu (Naamini waislam wengi walielekea CUF iliyokuwa na nguvu zaidi wakati huo) Hotuba yake ya kwanza ilizidi kutupa matumaini kwa tuliyoamini. Kumbe anatupiga kipapai.

Kwenye vita ya ufisadi JK amelaumiwa kwa kutowachukulia hatua wahusika wa Richmond kama akina EL, Mwanyika, Mwakapugi na Hosea. Hao ni waislamu? Kwenye kashfa hiyo pamoja na EPA, meremeta, n.k. wamo wakristo na waislam. Dk. Slaa na hata "wapambanaji" ndani ya CCM hawajachagua dini ya mtu katika kushusha nondo. Ndio maana hata JK alipomnadi Mramba kama mtu safi hakueleweka. Aidha, Pinda alipompigia chapuo Rostam kule Igunga alitushangaza.

Hii kuona ni waislamu ndio wanaandamwa itakuwa kama Ole Naiko wa TIC alivyoanzisha kilio kwamba wana-Monduli wanaadamwa baada ya kulaumiwa kuhusu madudu yanayofanyika TIC kwa kisingizio cha kuvutia uwekezaji. That's too cheap and extremely dangerous. Ni muhimu kwa watu wa dini zote kukemea uovu bila kujali autendaye ni wa dini ipi. Mkichagua kuwatetea wapuuzi kwa sababu ni wa dini yenu mjue kuwa hamuwatendei haki walio wasafi katika dini hiyo na zingine - labda kama lenu na mafisadi ni moja.

NDIO MAANA SISI WENGINE TUNASISITIZA HAKUNA MPASUKO WA KIDINI TANZANIA! JK NA MASHABIKI WAKE WANAPANDA MBEGU YA HATARI NCHINI MWETU - TUKATAE.
 
Udini hauonekani kuwako lakini umekuwako toka enzi zilee... za yule babu alipomuita yule babu kuwa ni mdini na yule babu mwingine akamsema yule babu kuwa si mwenzetu ni mdini.... Tokea hapo udini umekuwepo chini kwa chini... na udini huo uliendelea mpaka pale Prof. Kighoma Malima alipoupunguza makali akiwa waziri wa elimu kwa kuleta mfumo mpya wa namba badala ya majina.... udini upo upo, na hautaacha kuwepo mpaka pale mashaka ya wadini yatakapokuwa hayapo... otherwise tuendelee kufunika moshi mpaka wakati moto utakapolipuka rasmi :teeth:
 
Dubo kanusha kwa misingi inayoonekana na iliyo wazi. Kwani Somalia au Arabuni hakuna hayo jamani tuseme ukweli. Ukifika Saudia waulizwa je mwenzetu u dini gani hilo ni la kwanza, la pili utaulizwa unatoka wapi sasa hayo si kweli? Hapa Tanzania hakuna kitu kama hicho. Tulipomchagua JK 2005 kwa kishindo mie nikiwa mmojawapo hatukujali udini bali utendaji au hao 80%+ waliomchagua wakati huo walikuwa ni Waislamu peke yao si pamoja na Wakristo? Sasa hivi mie sikumpenda siyo kwa sababu ni Mwislamu bali mwenendo wake wa kiutendaji ni kutochukua hatua kwa mafisadi? Hilo la kutomchagua tutalifanya hata kama Rais atakuwa Mkristo. Kwa hiyo nakataa watu hawana udini ila wanataka maendeleo na si upuuzi mwingineo mmojawapo mie.
 
Hata mimi siamini kama kuna udini, ila kuna watu waliupandikiza ili wagombea wengine wasipate kura. Na kama kuna mgombea hakuchaguliwa basi ni kwa sababu utendaji wake ni mbovu. Ukiwa kama kiongozi na wenzako i mean wa dini yako wakakashifu dini nyingine na wewe ukakaa kimya basi nawe ni mdini, kwa mfano, Mikutano ya hadhara ya kuchambua biblia. Viongozi wapo kimya utafikiri hawasikii au hawaoni, nyumba za ibada zinachomwa moto nk. Ingekuwa kinyume chake nchi isingekalika.
 
Back
Top Bottom