Nakaribisha maswali yote kuhusu tohara ya mwanaume

muhamar Gadaf

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
1,049
991
nakaribisha maswali yote kuhusu tohara ya mwanaume.



Tohara ya mwanaume ya kitaalamu ni upasuaji mdogo wa kukata na kuondoa ngozi inayo funika kichwa cha uume.

kazi hii hufanywa na wataalam wa afya walio pata mafunzo maalum ya kufanya tohara kwa mwanaume na watoto wachanga.



Tafiti zinaonyesha tohara ya mwanaume inapunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya HIV kwa asilimia 60%


karibu kwa maswali na ufafanuzi zaidi kuhusu tohara ya mwanaume
 
Upi ni umri sahihi wa kutahiri mtoto..

Kuna madhara yeyote kumtahiri mtoto akiwa mdogo tuseme labda chini ya miaka mitatu..?
 
Ukitahiri ukiwa mkubwa au mdogo sana yepi madhara mtu anaweza pata ni umri gani sahihi wa kutahiri ambao hautafanya mboro kuwa kibamia!!??
 
asante kwa swali zuri.

ndugu zangu mtu anapofanyiwa tohara inayo ondolewa ni ngozi inayofunika kichwa cha uume ,
ngozi hii haina mahusiano yoyote na ukuaji wa uume .



hakuna madhara yoyote zaidi ya faida anayo weza kupata mtu aliye fanyiwa tohara.



umri sahihi wa mtu kufanyiwa tohara ni kuanzia masaa 24 toka mtoto amezaliwa na kuondelea.




faida za kuwafanyia watoto ni kuondokana na uwezekano wa kupata magonjwa ya kujirudia ya njia ya mkojo al maarufu kama UTI


kuanzia miaka 10 na zaidi husaidia kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya virusi vya HIV kwa asilimia 60%


hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya zinaa kama kaswende na pangusa kwa asilimia kubwa


hupunguza uwezekano wa kupata kansa ya uume


hupunguza uwezekano wa mke wako kupata kansa ya shingo ya kizazi.
Upi ni umri sahihi wa kutahiri mtoto..

Kuna madhara yeyote kumtahiri mtoto akiwa mdogo tuseme labda chini ya miaka mitatu..?
 
Ukitahiri kwenye umri mdogo ubakuwa na 90% ya kuwa na kibamia
hii sio kweli mkuu.

hii ni imani zilizo jengeka miongoni mwetu sisi lakini hazina kweli wowote


kwenye tohara ya mwanaume na mtoto mdogo , kinacho katwa paleni ngozi inayo funika kichwa cha uume.


hatukati kichwa cha uume mkuu !



karibu tene kwa swali lingine


wasalaaam
 
Ukitahiri ukiwa mkubwa au mdogo sana yepi madhara mtu anaweza pata ni umri gani sahihi wa kutahiri ambao hautafanya mboro kuwa kibamia!!??
madhara ya kuchelewa kufanyiwa tohara


1. uwezekano wa wakubwa kupata maambukizi ya HIV na magonjwa ya zinaa ninkwa asilimia kubwa.



kwa watoto husaidia kupunguza uwezekano wa kuvimba ngozi inayofunika uume ( phimosis) kwa asilimia kubwa.


husaidia kuzuia magonjwa ya UTI zinazo jirudia rudia kwa watoto.

nk
 
Back
Top Bottom