Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Rafiki yangu anaugonjwa wakuanguka anakuwa kama kazimia alafu anahema kwa kasi nakifua kinapanda sana litakuwa ni tatizo gani?
 
Hospitali wamempima wanasema hawaoni tatizo lolote. MORIO15
*UFAHAMU UGONJWA WA KIFAFA NA TIBA YAKE*

Huu ni ugonjwa ambao unasabababishwa na seli zilizopo katika mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa umeme[impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili, na kusababisha mtu kupata dalili kama vile kuishiwa nguvu, kichwa kuuma, kuchanganyikiwa, mwili kukakamaa na hata kupoteza fahamu. Hali hii hujirudia mara kwa mara.

Ifahamike kuwa, aina ya kifafainayojulikana sana mitaani ni ile ambayo mtu anakakamaa na kupoteza fahamu, japokuwa kuna aina za kifafa ambazo mtu hakakamai wala kupoteza fahamu, kama tutakavyoona hapo baadae.

Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua zaidi ya watu laki moja duniani, 80% wakiwa waafrika.

Mgonjwa huyu huweza kuanguka mara kadhaa kwa mwezi lakini anaweza asianguke kabisa kama anafuata masharti na utaratibu mzuri wa matibabu…

Chanzo cha ugonjwa wa kifafa ni nini?

chanzo kikuu cha ugonjwa huu kwa watu wengi hua hakifahamiki lakini baadhi ya hiz ni moja ya sababu za kuugua kifafa.

Kurithi; familia na koo zingine zinakua na ugonjwa huu hivyo watoto na wajukuu huzaliwa tayari na ugonjwa huu.

Kuumia kichwa: ajali zinazohusisha kuumia kwa kichwa huweza kusababisha kuumia kwa mishipa ya fahamu na mtu kuugua kifafa.

Magonjwa mengine; kuna magonjwa mtu akiugua maishani mwake baadae huweza kupata kifafa kwasababu magonjwa hayo yanavyoharibu mfumo wa ubongo.. mfano homa ya uti wa mgongo kitaalamu kama meningitis.

Uvimbe kwenye ubongo: matatizo ya uvimbe kwenye ubongo kama kansa huweza kusababisha mtu kuugua kifafa.

Kiharusi; huu ni ugonjwa ambao husababishwa na damu kushindwa kupita vizuri kwenye ubongo au kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo hali hii husababisha mtu kupooza nusu ya mwili wake na huweza kuugua kifafa baadae.

Matatizo wakati wa kuzaliwa: wakati mwingine mtoto huzaliwa kwa shida sana kwa njia ya kawaida kiasi kwamba kichwa chake hubanwa sana wakati wa kupita na hali hii huweza kumsababishia kifafa kwanzia utotoni.

Matatizo ya utengenezaji wa mtoto tumboni; wakati mwingine ile miezi mitatu ya kwanza ambayo mtoto ndio anapata viungo tumboni huweza kutokea kasoro kwenye mfumo wa fahamu za kwenye ubongo na kumfanya apate kifafa akizaliwa.

Magonjwa ya uzee yanayoathiri ubongo; kuna magonjwa huharibu ubongo wakati wa uzee na magonjwa haya huweza kusababisha kifafa kipindi hicho.

Kuna aina mbili kubwa za kifafa…

1)Primarymarygeneralized seizures

Hii ndio aina ya kifafa ambayo inafahamika sana mitaani; na inahusisha mgonjwa kukamaa, na kupoteza fahamu, pamoja na dalili zingine kama vile kutoa povu mdomoni, na kujisaidia haja kubwa na/au ndogo bila kujitambua akishikwa na hali hiyo.

Pia wengine hupatwa kama na wazimu au kuchanganyikiwa kwa muda kabla au baada ya kushikwa na hali hiyo.

2)Partial seizures

Aina hii ya kifafa ni ile ambayo haihusishi muhusika kupoteza fahamu na kukakamaa!! Bali hushikwa na hali fulani kama ya bumbuwazi kwa dakika kadhaa; Wengine huwa na dalili zisizoeleweka za mara kwa mara kama vile kusihiwa nguvu, kizungu zungu, kichwa kuuma sana (bila sababu ya kiafya inayojulikana), na kadhalika. Aina hizi za kifafa ziko nyingi, na dalili hutofautiana kwa kadri ya aina ya kifafa!!

Vipimo vinavyofanyika kugundua kifafa

Ugonjwa huu unaweza kutambulika kwa daktari kuchukua historia ya dalili zinazomkabili muhusika tu(hakuna kipimo ambacho kinaweza kutambua kifafa kwa asilimia 100); Kuna kipimo kinachopima jinsi ubongo unavyotoa taarifa za umeme (ELECTROENCEPHALOGRAM-EEG), ambacho kinaweza kutambua kifafa, lakini kipimo hiki kinaweza kikaonekana kuwa hakina shida, na bado mtu akawa na tatizo hilo la kifafa. Hivyo basi, kifafa ni moja kati ya magonjwa machache ambayo kutambulika kwake kunategemea sana ujuzi na utaalamu wa daktari katika kuunganisha dalili za mgonjwa kuliko vipimo!!

Hata hivyo, mara nyingi nyingi mgonjwa hupimwa vipimo tofauti ili kuweza kujua chanzo cha ugonjwa… mfano

• Uwezo wa kufanya kazi figo

• Uwezo wa kufanya kazi maini

• Kupima maji ya uti wa mgongo

• Kupima Kaswende

• Picha ya ubongo mfano CT SCAN.

mambo yanayofanya kupata degedege za kifafa mara kwa mara..

• Kukosa usingizi kwa muda mrefu

• Mianga na miale ya disko

• Unywaji wa pombe

• Kuishiwa sukari mwilini wakati wa akisikia njaa kali.

• Kutomeza dawa kama ilivyoelekezwa

Matibabu yasiyo ya dawa wakati mgonjwa amekamatwa na kifafa:{non pharmacological treatment}yaani HUDUMA YA KWANZA

• Mzuie mgonjwa asijiumize kwa kuweka kitu laini chini ya kichwa chake, ondoa vitu vikali karibu yake kama kisu, sindano au vyuma.

• Usilazimishe kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa.

• Usimshike kuzuia mizunguko yake

• Weka kichwa alale anaangalia upande mmoja ili kutoa mate mdomoni.

• Kaa na mgonjwa mpaka degedege ziishe

• Usiweke chochote mdomoni kwa mgonjwa kama dawa au chakula mpaka apate fahamu zake.

Mtu mwenye kifafa hali hii ya kukamatwa na degedege za kifafa sio ya ajabu sana ila ukiona dalili hizi mkimbize hospitali..

• Degedege za kifafa zaidi ya dakika kumi

• Kutapika sana

• Kushindwa kuona vizuri

• Kupoteza fahamu

• Kichwa kuuma sana.

MATIBABU YA UGONJWA

Kama kawaida chanzo cha ugonjwa kikipatikana mgonjwa huanzishiwa matibabu lakini kama mgonjwa alikua tayari ameshapata madhara kwenye ubongo kulingana na chanzo husika ataendelea kua na kifafa.

Ugonjwa wa kifafa hauponi kabisa kwa 100% hospitali, ukishaambiwa una kifafa au mgonjwa wako ana kifafa basi utapewa utaratibu wa matibabu yaani kumeza dawa siku zote za maisha yako na kufuata baadhi ya masharti na utaishi maisha ya kawaida kabisa.
ANNA DALILI HIZI
 
Mkuu nimeshindwa kuelewa yeye ni wakundi lipi hapo naomba nikuelezee inavyomtokea.Inapenda kumtokea sehemu yenye watu wengi,anaanguka gafla anazimia alafu anakuwa anahema kwa kasi nakifua kinapanda sana juu. kuna kipindi alizimia zaidi ya saa moja ikabidi awahishwe hospitali.lakini siku zakaribuni kaanguka kaamka ndani ya dk 10. hali hii inaniumiza sana maana kuna wakati anakata tamaa ananiambia bora afe.anateseka sana.

MORIO15
 
Mkuu nimeshindwa kuelewa yeye ni wakundi lipi hapo naomba nikuelezee inavyomtokea.Inapenda kumtokea sehemu yenye watu wengi,anaanguka gafla anazimia alafu anakuwa anahema kwa kasi nakifua kinapanda sana juu. kuna kipindi alizimia zaidi ya saa moja ikabidi awahishwe hospitali.lakini siku zakaribuni kaanguka kaamka ndani ya dk 10. hali hii inaniumiza sana maana kuna wakati anakata tamaa ananiambia bora afe.anateseka sana.

MORIO15
Anakuwa kama kachanganyikiwa akizinduka? Akizimia anazinduka baada ya muda gani? Na je ni kifua tu kinapanda? Hatikisiki au kukakamaa miguu na mikono? Macho kugeuka, kujingata? Habadiliki rangi? Kuna sababu tofauti zinazoweza kusababisha mtu kuzirai ukiachilia kifafa, mfano hypoxia(low level of oxygen) /syncope, hypoglycemia(low level of sugar) n.k
 
Hakakamai na akizinduka anakuwa na masikitiko anafunika uso nafikiri analiaga pia.hatikisiki na anakuwa kafumba macho anahema tuu.anazinduka baada ya dk 5 hadi 10 na habadiliki rangi.
 
Hakakamai na akizinduka anakuwa na masikitiko anafunika uso nafikiri analiaga pia.hatikisiki na anakuwa kafumba macho anahema tuu.anazinduka baada ya dk 5 hadi 10 na habadiliki rangi.

HYPOTENSION : Low Blood Pressure
Ifahamu Presha ya kushuka

Nini presha ya kushuka ?

Hypotension ndio jina alinalotumika kuelezea presha ya kushuka (90/60 mm Hg) ambayo huonekana kutokuwa na sababu iliyoifanya itokee.Kipimo cha presha huwa na namba mbili. Namba moja huwa juu na nyengine huwa chini.

Hypotension (haipo juu). Kwa watu wengi presha hii huwatia kizunguzungu na kuwaangusha. Presha hii ikiwa ya muda mrefu husababisha mtu kupata maradhi ya mshtuko.Watu wenye afya nzuri, hasa wakimbiaji, presha ya kushuka huwa ni dalili ya uzima kwao.
Si rahisi kuziona dalili kwa mtu mwenye presha ya kushuka hata kama imedumu kwa muda mrefu. Mara nyingi matatizo ya kiafya huwa ni

dalili ya presha ya koshuka pale mtu presha yake inaposhuka ghafla. Wakati huo wa matatizo ya kiafya, damu kidogo hufika katika ubongo. Hali hii humfanya mtu awe na kizunguzungu au kuumwa na kichwa kusiko kuwa kukubwa. Kushuka ghafla kwa presha mara nyingi humtokezea mtu pale anapofanya jambo la haraka kama mtu aliyekaa na kutaka kusimama mara moja. Kitaalamu presha hii inajulikana

kama postural hypotension, orthostatic hypotension, au neurally mediated orthostatic hypotension.
Postural hypotension inachukuliwa ni hali ile ya kushindwa kwa mfumo wa mawasilianao unaojiendesha wenyewe mwilini kufanya kazi yake kikamilifu (autonomic nervous system). Mfumo huu huendesha na kuongoza vitendo visivyo vya hiari (involuntary vital actions), kama vile

mapigo ya moyo kubadilika kutokana na jambo lililotokea kwa wakati uleopo. Kwa kawaida unapoinuka, kiwango fulani cha damu yako kinakuwa kimebaki sehemu ya chini (miguuni). Kukiwa hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa na mwili wako, hali hii itasababisha presha yako kushuka. Katika hali hii mwili wako unafanya nini ?

Mwili wako unapeleka taarifa kwenye moyo na kuamuru uongeze usukumaji wa damu ambao utaizidi mishipa yako na kuifanya kuwa membamba hali itakayopelekea kuifanya presha yako kubakia ileile. Ikiwa jambo hili halikufanyika au limaefanyika polepole sana, presha yako itashuka ghafla. Hapa ndipo mtu unapomuona anaguka ghafla.

Kwa ufupi athari ya maradhi ya presha ya kushuka na ya juu huongezeka kadri mtu anapokuwa na umri mkubwa na pia kubadilikabadilika kadri umri unavyoongezeka. Jambo jengine la kufahamu ni kuwa, ufikaji wa damu kikawaida kwenye ubungo unapungua kadri umri unavyoongezeka. Inakisiwa kiasi cha asilimia 10 mpaka 20 ya watu wenye umri unaozidi miaka 65, wanapata tatizo la presha yao kushuka.

Ni kiwango gani cha presha kinapofika ndio huwa maradhi ?
Hakuna kiwango maalum kinachojulikana ambacho ni sawasawa kwa watu wote kikifika ndio kinaitwa maradhi. Kiwango ambacho kwako ndio uzima, basi huenda kwa mwenzako ikawa ni maradhi. Katika presha ya kushuka, madaktari wengi huchukulia kuwa tayari mtu ana

maradhi pale aambapo kiwango chake cha presha kinafuatana na dali za maradhi yenyewe.
Hata hivyo, baadhi ya wataalamu wanachukulia tayari mtu ana maradhi ya presha ya kushika pale vipimo vinapoonyesha kiwango hichi 90/60 mm Hg. Tufahamu kuwa kiwango cha namba inayosomwa chini katika kipimo cha presha ( /60 mm Hg ), hichi huonyesha tayari mtu huyu

anapresha ya chini hata kama kile cha juu ( 90/mm Hg) kina namba iliyozidi 100. Mfano ikiwa umepimwa presha na ukapata kipimo hichi 115/60 mm Hg, presha yako itakuwa ipo chini. Na kama umepata kipimo hichi 115/50 mm Hg, sio kwamba presha yako itakuwa ipo chini tu, bali presha hii itakuwa si ya kawaida.

Dalili za maradhi

Kama nilivyokwisha tangulia kusema, presha inaweza kuwa sawa kati ya watu wawili lakini ikawa na matokeo tofauti. Presha hiyo inayoweza kuwa sawa na ikawa na matokeo tofauti si yenye kipimo hichi 120/80 mm Hg. Presha yenye kipimo hichi 120/80 mm Hg, ndiyo nzuri na watu wenye presha hii wanakuwa na afya nzuri. Kitu muhimu ni kujua, mabadiliko gani yanaleta tatizo katika presha hata inapelekea kuwa si ya kawaida.

Presha nyingi za watu wanapopimwa huwa zinakuwa kati ya 90/60 mm Hg (presha iliyo chini) mpaka 130/80 mm Hg (presha iliyo juu). Mabadiliko ya kushuka presha upande wa chini, hata kama kidogo kiasi cha 20 mm Hg, hupelekea matatizo kwa baadhi ya watu ( hasa watu wasiofanya mazoezi kila siku).

Mtu mwenye mazoezi ambae presha yake nzuri (120/80 mm Hg) akapimwa presha na kupata kipimo hichi, 110/60 mm au 120/70 mm Hg, mtu huyu hatakuwa na tatizo lolote la presha
Kuna aina tatu za presha ya kushuka :

 Orthostatic sambamba na postprandial orthostatic (Orthostatic hypotension, including postprandial orthostatic hypotension)
Orthostatic, hii ni aina ya kwanza ya presha inayosababishwa na kubadili mazingira uliyonayo kwa ghafla, maranyingi hutokea kwa mtu anayesimama kutoka alipolala. Presha hii haidumu muda mrefu, kiasi cha sekunde chache mpaka dakika moja. Ikiwa presha hii itatokezea

baada ya kula, basi itakuwa ni hatua ya pili(postprandial orthostatic) .Hatua hii ya pili huwapata zaidi wazee na wenye presha ya juu.
 Neurally mediated hypotension (NMH)
NMH kama ilivyo kifupisho cha presha aina ya pili, huwapata zaidi vijana na watoto. Presha hii hutokea pale mtu anaposimama kwa muda mrefu. Maranyingi huwapata sana watoto.

Aina hii ya pili ya presha ya kushuka maranyingi husababishwa na hali zifuatazo :
Utumiaji wa pombe
Utumiaji wa dawa za kutibu presah ya juu.
Utumiaji wa dawa za kumtoa fahamu mtu wakati wa kufanyiwa upasuaji

Mambo mengine yanayosababisha presha kushuka ni pamoja na :
Ugonjwa wa Kusukari
Mtu kula kitu kinachomdhuru
Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida
Maradhi ya kuharisha
Kuzimia
Maradhi ya moyo
Maradhi ya kustuka
 
Hakakamai na akizinduka anakuwa na masikitiko anafunika uso nafikiri analiaga pia.hatikisiki na anakuwa kafumba macho anahema tuu.anazinduka baada ya dk 5 hadi 10 na habadiliki rangi.
Kama hospitali hawajaona kitu ana tatizo linaloitwa SYNCOPE linasababishwa kushuka kwa msukumo wa damu kwenye ubongo,tukio ambalo linasababisha kupoteza fahamu na hata uwezo wa kudhibiti misuli.Kitendo hiko kinasababisha mtu kuanguka ambapo damu inaruhusiwa kusukumwa kwenye ubongo ikisha mtu fahamu humrudia.Mara nyingi hili tatizo linakuwa linadumu kwa sekunde hata dakika kadhaa.
Ugonjwa huu unaweza unasababishwa na vitu kadhaa:
  • Kushuka kwa presha au mishipa ya damu ilotanuka
  • Kubadilikabadilika kwa mapigo ya moyo
  • Kusimama kwa muda mrefu
  • Stress
  • Ujauzito
  • Kukosa maji ya kutosha mwilini
  • Kitendo cha kusimama haraka
  • Uoga
  • Uchovu
Ndio maana kuna baadhi ya watu wakiona damu wanazirai.Tatizo hili linaweza kuchochewa na vitu tofauti vinaavyomzunguka mtu.

DALILI NA ISHARA zinazoonesha kwamba unaweza kuzirai
  • Kichefuchefu
  • Kubadilika kwa mapigo ya moyo
  • Kutoka kwa jasho ghafla/mabadiliko ya hewa kuhisi joto au baridi ghafla
  • Kufa ganzi
  • Kizunguzungu
  • Kuumwa na kichwa/kichwa kuwa chepesi
  • Kuchoka
  • Kutetemeka
  • Mabadiliko kwenye kuona
  1. Ukiona dalili zozote nilizozitaja hapo juu inabidi uacha unachofanya na uketi chini
  2. Jaribu kulala chini na kuweka miguu juu au keti chini na weka kichwa katikati ya miguu hii itasaidia msukumo wa damu uende kwenye ubongo.Na hata ukizirai ukiwa umelala itakuepushia majeraha au ajali
  3. Jaribu vilevile kutambua vichocheo vinavyosababisha ukazirai
  4. Ni muhimu ukapime presha,EKG na MRI ya ubongo,kisukari ili kuhakiksha hakuna tatizo lolote jingine linaloweza kuchochea kupoteza fahamu.
Kila la kheri
 
Nimeonaga wagonjwa wakifafa wakiwa wamezimia lakini kwa huyu ni tofauti kabisa dah.



Vipi iyo low level of sugar inatibiwaje na je kunauwezekano wa hali hii kumuisha kabisa?

Mm shida yangu ilikuwa kutafuta namna yakumsaidia kimatibabu wakuu.
 
Nimeonaga wagonjwa wakifafa wakiwa wamezimia lakini kwa huyu ni tofauti kabisa dah.



Vipi iyo low level of sugar inatibiwaje na je kunauwezekano wa hali hii kumuisha kabisa?

Mm shida yangu ilikuwa kutafuta namna yakumsaidia kimatibabu wakuu.
Si kila ugonjwa una tiba ya dawa. Kisukari anaweza kupima hosp na tiba zipo aina tofauti!
 
Hi! Mimi huwa nasumbuliwa na tatizo kwenye mguu wa kushoto kwenye maungio kati ya nyonga na mfupa wa mguu unauma kuanzia kwenye nyonga mpaka kukaribia goti haya maumivu huwa yanaanza pale tu nikifanya kazi za kudeki au kubeba vitu vizito vinavyohusisha kuinama inama,..Hili tatizo lilianza nilivokuwa na ujauzito wa miez 7 mpaka sasa mtoto ana umri wa miaka 2 na miez 8 na jinsi mda unavokwenda ndo maumivu yanazidi mda mwingine nashindwa hata kusimama vizur, naomba msaada wa kujua shida ni nn na tiba yake, asanten.
 
Hellow wapendwa,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu dawa zozote zenye active ingredients (DRUGS). Kama una maswali kuhusu matumizi yake, matumizi yake pamoja na dawa nyingine, vyakula (interactions), athari zake (side effects) au hata kama unataka kujuzwa jinsi dawa inavyofanya kazi kutibu ugonjwa!!

Karibuni sana.

A



B


C


D


E



F
 
Hi! Mimi huwa nasumbuliwa na tatizo kwenye mguu wa kushoto kwenye maungio kati ya nyonga na mfupa wa mguu unauma kuanzia kwenye nyonga mpaka kukaribia goti haya maumivu huwa yanaanza pale tu nikifanya kazi za kudeki au kubeba vitu vizito vinavyohusisha kuinama inama,..Hili tatizo lilianza nilivokuwa na ujauzito wa miez 7 mpaka sasa mtoto ana umri wa miaka 2 na miez 8 na jinsi mda unavokwenda ndo maumivu yanazidi mda mwingine nashindwa hata kusimama vizur, naomba msaada wa kujua shida ni nn na tiba yake, asanten.
 
Ndg yangu anasumbuliwa na uvimbe kwenye njia ya haja kubwa, kwa ndani kidogo imayomletea maumivu japo sio sana, aliwahi patiwa Anusol vidonge vya kuweka ndani ya njia ya haja kubwa lkn baadae ya mda ikamrudia,,, je ni dawa ipi sahihi ya kutumia na nasikia kuna dawa za asili, ni zipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndg yangu anasumbuliwa na uvimbe kwenye njia ya haja kubwa, kwa ndani kidogo imayomletea maumivu japo sio sana, aliwahi patiwa Anusol vidonge vya kuweka ndani ya njia ya haja kubwa lkn baadae ya mda ikamrudia,,, je ni dawa ipi sahihi ya kutumia na nasikia kuna dawa za asili, ni zipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Dawa alotumia ni sahihi.Ana tatizo la bawasili. Anaweza kutumia upya dawa ya kuweka kwenye njia ya hajakubwa yenye prednisolon/hydrocortisone. Ni muhimu pia ajaribu kuepuka hali hio isitokee tena kwa kufanya yafuatayo
  1. Afanye mazoezi
  2. Aepuke kuwa na choo kigumu(constipated) kwa kunywa maji ya kutosha, kula vyakula vyenye fibers nyingi kama mboga na matunda
  3. Alifunze tumbo kwenda haja kwa wakati maalumu mfano baada ya kifungua kinywa au chakula cha mchana
  4. Aepuke kukaa muda mrefu akijaribu kusukuma hajakubwa.
 
Hi! Mimi huwa nasumbuliwa na tatizo kwenye mguu wa kushoto kwenye maungio kati ya nyonga na mfupa wa mguu unauma kuanzia kwenye nyonga mpaka kukaribia goti haya maumivu huwa yanaanza pale tu nikifanya kazi za kudeki au kubeba vitu vizito vinavyohusisha kuinama inama,..Hili tatizo lilianza nilivokuwa na ujauzito wa miez 7 mpaka sasa mtoto ana umri wa miaka 2 na miez 8 na jinsi mda unavokwenda ndo maumivu yanazidi mda mwingine nashindwa hata kusimama vizur, naomba msaada wa kujua shida ni nn na tiba yake, asanten.
Nakushauri uende ukachekiwa kuhusu ugonjwa unaoitwa PERIPHERAL VASCULAR DISEASE.Ni tatizo linalosababisha blockage kwenye mshipa wa damu(artery) kutokana na atheloscleorosis.
 
Back
Top Bottom