Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

bright platnumz

bright platnumz

JF-Expert Member
2,750
2,000
Naomba kujua jinsi ya kulainisha kidevu kilicho momaa kwa kunyoa ndevu
 
Asclepius

Asclepius

JF-Expert Member
692
1,000
Nasumbuliwa na gono mwezi wa tatu sasahivi nilienda clinic nikachoma sindano usaha ukawa hautoki tena, nikawa fresh kabisa baada ya wiki mbili nikafanya mapenzi nilitumia condom fresh kabisa, asubuhi nilipo amka nikawa naisi maumivu sehemu zangu za pumbo nikavumilia kama siku mbili nikaenda tena clinic MR Doctor akanipa tena doz ya sindano na vidonge, baada ya wiki mbili nikajihisi nimepona kama kawaida nikafanya tena mapenzi nilitumia condom sema asubuhi nilipo amka nikawanaona kitu kama maji maji mazito meupe yanatoka kwenye ume wangu nikaenda tena clinic nikachoma sindano mpaka leo hii maji maji bado yanatoka Tu.
Me nadhani kuna haja ya kumaliza dozi na pia ukienda hospitali waambie ufanye kitu kinaitwa culture and sensitivity itasaidia kujua huyo mdudu dawa gani inamuondoa kwa asilimia zote
 
Asclepius

Asclepius

JF-Expert Member
692
1,000
naomba kujua dawa effective ya kutoa mimba ya wiki 3-4
gharama zake na zinapatikana wapi
Wiki tatu mpaka nne misoprostol inaweza kutoa
Ila jiulize kwann utoe mkuu fikiri mara mbili mpaka tatu
 
Asclepius

Asclepius

JF-Expert Member
692
1,000
Vidonda via tumbo dawa yake ni Nini dr please reply
Vidonda vya tumbo mara nyingi havitibiki ila inategemea na kisababishi chake kama ni bacteria utapewa dawa zitakazomuondoa huyo mdudu na kukupa afadhali pia kuna dawa za kupunduza acid na kadha wa kadha
Cha muhimu fuata management ulopewa na daktari wako ili vidonda visizidi kuongezeka ukubwa
 
Asclepius

Asclepius

JF-Expert Member
692
1,000
Habari yako,

Nina tatizo la kuwashwa kwa korodani miaka mitatu na nusu sasa.

Nimetumia dawa creams za hospital, pils za anti fungal, dawa za asili nyingi mno sijapona..

Nimemuambukiza kipenzi mke wangu pia.

Sijawahi kuchepuka na sijui chanzo ni nini.

Ugonjwa nilianza kuupata nilipokwenda safarini dsm mwaka 2016 February..

Nifanye nini niweze kupona kabisa????
Kafanye culture and sensitivity wanaweza jua dawa gani ni effective
Na kutokana na kua umetumia dawa nyingi za kila aina pengine wadudu wamekua sugu na dawa
And by the way anza na either flucanozole au griseofulvini wakati unaendelea kufanya hiyo test niliyokuambia
 
Asclepius

Asclepius

JF-Expert Member
692
1,000
Hello habari yako...

Pole sana na majukumu..

Nipo hapa kuwasilisha tatizo langu.
Nimeamka asubuhi naenda chooni haja kubwa najisaidia choose cheusi. Najiandaa kwenda kazini najihisi kizunguzungu. Natoka nyumbani nafika njiani napata kizunguzungu macho yanaona giza naishiwa nguvu na kutapika maji kama meusi hivi. Na sometimes kila nikitapika holaa.

Mkuu mpaka hapo tatizo nini...
Naomba muongozo kiongozi
Kutakua na tatizo kwenye mfumo wako wa umeng’enyaji nenda hospitali kwa maelezo zaidi
 
zere

zere

Senior Member
122
225
Polen na majukum wakuu . Ninatatizo la pre-mature ejaculation & nakumbhka o-level nlikuwa mwanachama wa chaputa 6years ago sasa ni victim wa pre-ejaculation naomba msaada. Mazoez nafanya sana
 
Tomasi Sankara

Tomasi Sankara

Member
95
125
Hellow wapendwa,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu dawa zozote zenye active ingredients (DRUGS). Kama una maswali kuhusu matumizi yake, matumizi yake pamoja na dawa nyingine, vyakula (interactions), athari zake (side effects) au hata kama unataka kujuzwa jinsi dawa inavyofanya kazi kutibu ugonjwa!!

Karibuni sana.

AB


C


D


EF
Naomba msaada niliumia mkono kwenye maungio nikafungwa p.o.p kwa wiki 4 sasa Jana wametoa lakini mkono bado auko vizuli naomba kama kuna dawA naweza kutumia picha apo chini za X ray na mkono ulivyo sasa
 
Mjina Mrefu

Mjina Mrefu

JF-Expert Member
2,835
2,000
Kafanye culture and sensitivity wanaweza jua dawa gani ni effective
Na kutokana na kua umetumia dawa nyingi za kila aina pengine wadudu wamekua sugu na dawa
And by the way anza na either flucanozole au griseofulvini wakati unaendelea kufanya hiyo test niliyokuambia
griseofulvin nimeitumia miezi miwili but hamna mabadiliko
 
Mjina Mrefu

Mjina Mrefu

JF-Expert Member
2,835
2,000
Kafanye culture and sensitivity wanaweza jua dawa gani ni effective
Na kutokana na kua umetumia dawa nyingi za kila aina pengine wadudu wamekua sugu na dawa
And by the way anza na either flucanozole au griseofulvini wakati unaendelea kufanya hiyo test niliyokuambia
Mkuu sifahamu Culture and sensitivity ni nini....nipe maelezo zaidi
 
Munamuge

Munamuge

JF-Expert Member
531
500
griseofulvin nimeitumia miezi miwili but hamna mabadiliko
Unapoitumia hakikisha unakula vyakula vyenye mafuta kwa wingi ili iweze kufanya kazi, vinginevyo utakua unaitumia kama kiburudisho tu. Kama hayo yote umezingatia na haijasaidia basi inaweza tatizo lako lisiwe fungal infection
 
Mjina Mrefu

Mjina Mrefu

JF-Expert Member
2,835
2,000
Unapoitumia hakikisha unakula vyakula vyenye mafuta kwa wingi ili iweze kufanya kazi, vinginevyo utakua unaitumia kama kiburudisho tu. Kama hayo yote umezingatia na haijasaidia basi inaweza tatizo lako lisiwe fungal infection
Mkuu, Naweza kupima hii kitu? vipimo gani? Maana nimeenda kwa Dermatologist Muhimbili, haja propose kuhusu vipimo, ananipa dawa tu hizo cream
 
Scoko

Scoko

Senior Member
165
250
Mtoto wangu wa mwaka mmoja na nusu
akilia ama kwa hasira au kwa mstuko
hukakamaa na kupindua macho na kupoteza fahamu kwa muda.
Je hii ni degedege?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pablo

Pablo

JF-Expert Member
2,442
2,000
Nikila chakula naskia kutapika. Ingawa nimeshawahi tapika mara 3 Tuu hizo nyingine najizuia na hali hii hutokea wakati wa kula tuu iwe asubuh,mchana au jioni.

Nilienda hospital nikapewa dawa za minyoo lakini hakuna mafanikio, ni mwezi wa sita sasa hii hali ipo kwangu.

Mwenye uwezo wakunisaidia nini tatizo anisaidie au kama kuna mtu aliewahi kumbana na tatizo kama hili pia anaweza akashare na mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
D

DsmicSound

JF-Expert Member
1,474
2,000
Ninaharisha tu maji maji bila tumbo kuuma...sasa nimetumia 'loperamide' wakati huo huo nina dose ya kifua ya Koflyn(Diphenhydramine) pamoja na amoxlyn(Antibiotics)...

Sasa naona mafua yameanza mpaka macho yanauma nikifumbua sana...na kifua ndio kama kawaida...sasa nahofia kunywa hiyo dose yangu...nikihofia REACTION itakayotokea...na diclofenac ya maumivu pia nimepewa...

Sasa ninafanyaje...maana dawa ni nyingi sana...je hakuna madhara yoyote yatakayotokea...?

NB: NI JANA NIMETOKA KITUO CHA AFYA WAMEPIMA MALERIA UTI HAKUNA SASA...WAKANAMBIA NIRUDI WACHECK LABDA NA TYPHOID...ILA KIFUA TU NDIO WAKANIANDIKIA HIZO DAWA(wakati huo kuharisha kulikuwa bado...maana kumeanza usiku huu).

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics


Threads
1,424,521

Messages
35,065,802

Members
538,008
Top Bottom