Najuuta kuusikiliza ushauri wa mama watoto

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,673
9,988
Kabla hatujaoana nilikuwa nafanya sana mazoezi kwa ajili ya kujiweka fit na ili niwe na mivuto hasa kwa wasichana na wavulana wavivu wanaotamani miili ya wenzao wafanya mazoezi huku wao wakijiachia na vitambi.

Siku zote nilivichukia sana vitambi na mchumba wangu wa kipindi hicho ambaye sasa ni mke wangu alilijua hilo.
Muda wa honeymoon sikuweza kabisa kufanya mazoezi, wiki tatu za fungate nikaanza kuhisi mabadiliko mwilini mwangu.

Wife akanishauri nijaribu valeur inapunguza mafuta. Nilicho kipata sasa ni kwamba sina tena uwezo wa kufanya mazoezi, valuer ziinanifanya nile sana, nimekuwa na kitambi kama mimba.

Pia nimekuwa mlevi na mtumwa wa pombe, nisipogida silali. Yaani bora nisingesikiliza ushauri
 
"ulevi ni noma" muone daktari akushauri namna gan unaweza acha pombe na kurudia enzi zako za SEX BODY na kuukimbia Upolygon ulionao kwa sasa.ASANTE
 
Mkuu...wiki tatu hazitoshi kukufanya ubadilike mwili kiasi hicho kama wewe ni mtu wa mazoezi...
Acha pombe anza mazoezi upya.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kama unakunywa sana jaribu kuhamia kwenye bia, baadhi ya watu (mimi mmojawapo) nkishatandika za kutosha nakuwa sina hamu na msosi, itakusaidia kutokula sana.
 
hapa naona kuna mambo mawili; kupunguza pombe na kupunguza mwili.

1. kupunguza mwili; ishi ya mwili kama ulivyosema ni kufanya mazoezi sana pale unapopata nafasi. endeleza zoezi hasa kwa mida ya alfajiri.

2. kupunguza unywaji; katika hili ukianza kufanya zoezi utapunguza pia iweke akilini kwamba unataka kupunguza pombe. na pia jua kwamba kunywa pombe kunaleta njaa inayokufanya ule sana na pia mfano bia ukinywa nyingi ikiingia mwilini inabadilishwa kuwa fat na ndo maana wengi wanaokunywa sana wanakuwa na vitambi vikubwa.

So, kuacha pombe si ishu, ishu usi addict bana. At least uwe unapitisha siku 3 au nne ndo unapiga japo bia 2 si mbaya. ila usizime yaani mibia mingi kwanza hata pesa itaisha bwana.

conclusively; zoezi + punguza wanga(ugali, wali, viazi etc) +maji mengi(at least 3litres per day) + mboga mboga
 
Jamani suala hapa sio kushuriwa na mkewe. Suala ni kitambi... Hili ni tatizo kubwa sio tu kwa afya ya mapenzi, bali hata kwa maisha yako...
 
pole sana, nadhani usimhukumu mkeo
fuata ushauri unaopewa na wadau na utapona tu
amua kuacha pombe na hautakufa
mazoezi ni muhimu kwa kitambi
balance milo yako
 
Jamani suala hapa sio kushuriwa na mkewe. Suala ni kitambi... Hili ni tatizo kubwa sio tu kwa afya ya mapenzi, bali hata kwa maisha yako...

kunywa kile kinywaji jamaa aliyenyanyua mikono!! akiishusha mikono na ww kitambi kwishinei.
 
.....kinachokushinda kufanya mazoezi nini?mwambie wife adiliti ushauri wamwanzo,akupe wakufanya mazoezi na kwa vile wamsikiliza sana uatafanya!ukishindwa kabisa,kunywa sanaaaaa pombe,sanaaaaaa afya yako itaporomoka then utarudia mwili wako wa kawaida
 
Kama unakunywa sana jaribu kuhamia kwenye bia, baadhi ya watu (mimi mmojawapo) nkishatandika za kutosha nakuwa sina hamu na msosi, itakusaidia kutokula sana.

Ya nini kuingia gharama za bure? Ajaribu GONGO aka CHANG'AA aka SUPU YA MAWE aka MACHOZI YA MAMBA etc. Pombe yenye thamani ya bia moja tu inatosha kumsahaulisha msosi kama kweli atafanikiwa kuimaliza.
 
mtoa mada bila shaka nyumba yako umeizindika, tena kabla hujaenda hospitali unapitia kwanza kwa mganga wa kienyeji. Ukitaka kufanya kitu ni lazma upige ramli kwanza. Yaani naona tu, hata ukikwapuliwa simu na vibaka unaenda kwa mganga mwenye tv ya asili.
Ukijikwaa unarudi nyumbani kuanza upya safari, ukiamini kwamba uliianza na mkosi.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom