Najuta: nilioa mke kwa kuvutiwa sura na umbo lake

Headless Person

JF-Expert Member
Nov 30, 2012
307
0
Habari zenu wanajamvi.

Nilidhani nimepata kumbe nimepatikana! Mwaka jana mwezi wa tatu nilifunga ndoa na mke wangu. Tumejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume. Kitu kikubwa kilichosababisha nikamuoa ni sura yake ya kuvutia, sauti yake tamu pamoja na umbile lake kwa ujumla. Kiukweli ameumbika sana.

Tatizo alilo nalo mke wangu ni kwamba kwa sasa hakamatiki! Hatulii. Anatembea hadi na marafiki zangu. Kibaya zaidi ni kwamba siku hizi kila nikitaka kufanya naye mapenzi ananiambia hajisikii kufanya hivyo.

Ameanza kunidharau na kuniona mimi sina hadhi kwake. Inaniuma sana.

Wazazi wa pande zote mbili wamejaribu kulitatua hili bila mafanikio.

Sasa nimeona kabla ya kuchukua maamuzi mengine mazito nimeamua niwashirikishe mnipe ushauri wenu. Nisaidieni kuokoa ndoa yangu jamani.
 

Suprise

JF-Expert Member
Nov 2, 2012
2,697
2,000
mlilie bana uwe ka bushoke akuone huwezi ishi bila yeye, wanawake tumeumbiwa huruma ipo siku atarudi kwako mazima
 

georgeallen

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
3,762
2,000
Habari zenu wanajamvi. Nilidhani nimepata kumbe nimepatikana! Mwaka jana mwezi wa tatu nilifunga ndoa na mke wangu. Tumejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume. Kitu kikubwa kilichosababisha nikamuoa ni sura yake ya kuvutia, sauti yake tamu pamoja na umbile lake kwa ujumla. Kiukweli ameumbika sana. Tatizo alilonalo mke wangu ni kwamba kwa sasa hakamati! Hatulii. Anatembea hadi na marafiki zangu. Kibaya zaidi ni kwamba siku hizi kila nikitaka kufanya naye mapenzi ananiambia hajisikii kufanya hivyo. Ameanza kunidharau na kuniona mimi sina hadhi kwake. Inaniuma sana. Wazazi wa pande zote mbili wamejaribu kulitatua hili bila mafanikio. Sasa nimeona kabla ya kuchukua maamuzi mengine mazito nimeamua niwashirikishe mnipe ushauri wenu. Nisaidieni kuokoa ndoa yangu jamani.
Headless person???? Mambo yatakuwa mazuri ukibadilisha hili jina
 

prianka

JF-Expert Member
Aug 29, 2012
684
195
kama wazazi pande zote mbili wamegonga miamba na tena huwa kunamsemo unasema wazazi ndo mungu wa duniani kama yeye kakataa kuwasikiliza unategemea nini? ok jaribu kwenda hata huko mliko fungia ndoa wanaweza kubadilisha kiroho ikishindikana achana naye maana maisha yenyewe mafupi na tena ya tabu c ndo utazidi kuchanganyikiwa looo pole sana
 

bhikola

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,130
2,000
Mi nafikiria kwa mitazamo miwili,
Kwanza ni username yako, kama ina reflect personality yako, then no wonder its that way. so endelea kuwa headless person maana hapa kikubwa ninacho kiona ni wewe kuacha kichwa cha chini ki over-ride kichwa chenye ubongo, tumia mbongo yako mtoto wa kiume
Ishu ya pili ni kutojua hasa tatizo ni nini?! mi siamini kama mke kabisa anaweza anza tu abruptly kuwa namna hiyo, na kama kweli ni hivyo baasi kazi unayo. otherwise kaa chini, au nenda vacation mkae huko hata kwa mwezi mmoja, zaidi ukitafakari yaliyopita kuliko yanayotokea naamini utajua kiini cha tatizo na hapo ndo penye utulivu na saburi. ki msingi Vunja Ukimya dude
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom