Najuta kuwahi kuoa, mke wangu hanivutii tena

Nimeoa miaka nane iliyopita na nimepata watoto watatu. Ila sasa naona kama nilikosea kuchagua sababu huyu mke wangu tulianza mahusiano tukiwa shule tukaenda hadi Chuo kikuu pamoja.

Sasa naona wanawake wengine wazuri na wanaojipenda zaidi yake na nikiangalia yeye alivyo hajipodoi podoi yupo yupo tu na hana sexy body yaani havutii kabisa mpaka saa nyingine najisikia aibu.

Yaani nashindwa kujua nifanyeje kumwacha namwonea huruma sana.

Hakuna mwanamke mbaya au ambaye hana mvuto kabisa. Ni kweli kuwa kuna wengine wana mvuto kuliko wengine ila kwa ujumla wanawake wote wazuri. Nafikiri kinachotokea hapa ni kuwa umemzoea mke wako kwa hivyo unamchukulia poa, changamoto ambayo wanaume wengine tulio kwenye ndoa tunaweza kukumbana nayo!

Kwanza nikuambia kitu kimoja kama wewe ni mwanaume uliekamilika hutoacha kuona au kutamani wanawake wakali na wazuri hata kama umeoa. Huu ni ukweli ambao kuna wakati tunataka kuukataa ila hali ya wewe kama mwanaume kutamani au kuwaona wanawake wazuri itaendelea kuwepo.

Tofauti kati yako wewe mume wa mtu na kijana ambaye hajaoa ni kuwa kama mume wa mtu pengine utashindwa kufanyia kazi hayo matamanio, mimi huwa namshukuru Mungu kwa uumbaji maana macho nayo yanafurahi kuona wadada wazuri.

Sasa tujikite kwenye changamoto yako na ushauri wangu kwako. Napenda ukumbuke kuwa mwanamke mwenye watoto watatu, yaani mwanamke mama kama mkeo huwa anabadilika kidogo. Kama ungependa aendelee kubaki alivyokuwa binti basi suala la watoto ungeliacha, lakini kwa kuwa umechagua kuwa baba lazima kukubaliana na mabadiliko kwenye mwili wa mkeo.

Changamoto kwako hapa inakuwa matunzo. Je, unamhudumia mkeo katika namna ambayo inamsaidia kuendelea kubaki na mvuto? Kwa sababu mkeo mzuri, changamoto no huo mvuto ambao haitoshi tu kuoga na kuvaa nguo ndugu yangu.

MMimi nakushauri wekeza kwenye vitu vidogo vidogo. Kama mkeo ibabidi atengeneze nywele mkumbushe, muwezeshe, kapafyumu kidogo. Kama ameongezeka sana uzito baada ya kuwa mama fanya naye changamoto ya kupiga mazoezi na kubadili misosi ili apungue...yaani hata kama wewe huitaji kupungua uzito jitoe umsaidie yeye.

Halafu fanya mitoke na mkeo, mtoko sio kwenda kwenye sherehe za harusi na ubatizo tu. Toka nae mkeo. Ukiwa na hela kidogo kalale nae nje ya mji, yaani mfanye ajisikie unafanya jitihada basi naye atakuonesha mambo. Lakini ukiwa umezubaa naye anakuchukulia poa!

MMimi nakuhakikishia ukimuacha mkeo ataanza kupigwa miti na mtu ambaye anawajibika na utajuta. Tena kimsingi unaweza kumwacha na hao wanawake wakali wote wakapotea, usiwaone!

Furahia ndoa yako, fanya jitihada kuhakikisha mkeo anaendelea kuwa na mvuto kaka. Wajibika...usimpige mkeo makofi...mwanamke anapigwa kwa mavitenge, makanga, mapafyumu, MA-hairstyles na vitu vya namna hiyo.
 
Kama ulioa shape kaka hahahaa wewe leta wenge ukaokote mashaoe kama hatujashare mzigo wako...halafu urudi hapa utuambie... Hakuna rangi hutaona, siku hizi kupata mwanamke wa kuwa mke na kukaa na watoto na kukuheshimu na akatulia ni ndoto. kama ni hamu itakuja tu ili mradi usiwe mzinzi. Mara nyingi hamu ya mkeo hupungua kwasababu ya uzinzi unapiga piga nje. Tulia kula likizo kifuko kijae utashangaa utakavyolipuka anae.

Muhimu, tunza nguvu, pumzika vya kutosha kula mlo mzuri, usiguse nje halafu time siku zake za joto (ovulation). Hizo ndio siku kwa kawaida binadamu alipaswa kuhudumu nbdoa sio siku nyingine. Wanayama wote wana uwezo mzuri sana wa kutambua hizo siku aidha kwa tabia ya jike au kwa harufu na joto, wengine hunus ahata mkojo au harufu ya mwanamke tu inakusisimua. Binadamu sababu ya mapafyumu na maisha haya tumepoteza kabisa huo uwezo. Wanyama wengine wote hawampandi jike mpaka iwe siku na wakati muafaka haswa, na hapo wote mwanamke na mwanaume mnafaidi ndoa yenu.

Sijui kama ulimkuta baba yako akiwa na mama yako, au babu akiishi na bibi? maana hilo nalo huathiri mtizamo na namna unavyoelewa ndoa.
 
Kama umechoka ndoa fanya taratibu za kisheria uondoke zako. Achana na hawa waswahili wanaoishi kwenye maisha feki ya ndoa. Ndoa ni mkataba unaovunjwa muda wowote.
Usijaribu kumbadilisha mwanadamu ni mtu huru kama mkeo anafurahi kujiweka anavyojiweka siyo jambo la busara kumbadilisha, maisha yenyewe tunaishi mara moja, kuwa na furaha ni jambo la msingi sana kwenye maisha yetu mafupi.
Mkuu acha kuiga mambo ya wazungu si yote yanafaa kwa mila zetu za Tanzania na Afrika,unasema ndoa ni mkatata na unaweza kuvunjwa muda wowote,wewe wazazi wako walikuwa kwenye ndoa ya mkataba na wameuvunja?Mtu mwenye tabia ya ubinafsi wa hali ya juu ndiyo hao wanaosupport ndoa za jinsia moja hawana tofauti na wewe unayesema ndoa inaweza kuvunjwa muda wowote.Ok,mkivunja hiyo ndoa muda wowote na watoto manawavunja au?Mali nazo manazivunja?na kwa akili yako unadhani kesi za aina hii zinaisha haraka tu wiki moja mambo shwari unaedelea na ndoa mkataba nyingine?Wewe ungekua ukajikuta uko na wazazi wa kambo kisa wazazi wako walivunja mkataba kama unavyoshauri ungejisikiaje?Unajua madhara ya hizo ndoa za kuvunja muda wowote?
Ni kweli kuwa na furaha ni jambo la msingi lakini haimanishi upate furaha hata kwa kusababisha matatizo kwa jamii inayokuzunguka huo ni ubinafsi wa hali ya juu.Kama unataka mwanamke atakayekuvutia siku zote huyo huyo azae huyohuyo aonekane kama binti,huyohuyo awe ana kila kitu mwanamke wa aina hiyo ni wa kufikirika na kama unamwitaji weka order utengenezewe mdoli lakini hakuna mwanamke ambaye ataendelea kuwa kama alivyokuwa ten years ago hata kama ataenda gym na kujipamba kama watu wanavyoshauri.
Elimikeni,huwezi kupingana na "natural laws" siku zinavyosonga sura na mwonekano wa mtu hubadilika huwezi kuzui ila unaweza kuchelewesha na si kwa muda sana.
Wewe unaonyesha unatabia za kulaumu watu kwa matatizo unayopitia au kupata,unapokutana na tatizo kama mwanaume unatakiwa kupambana nalo hii wewe unaita kuishi maisha feki,umeonyesha wewe unatabia za kukimbia matatizo bila kutatua chanzo cha matatizo.Utahangaika sana kama hutabadilika.
 
Hamna kitu cha kipumbavu kama kuishi na mtu uliopoteza mapenzi naye kisa unagopa kuvunja ndoa, kuogopa jamii, kuogopa utashindwa kutunza watoto. Hivi mbona hamuogopi vitu vinavyotisha zaidi ambavyo vinaletwa na hizi ndoa zilizokosa upendo? Ulevi, Umalaya, Magonjwa ya zinaa, pressure, Domestic violence, Stress, Watoto wa nje ..etc. Siyo coincidence unakuta wake za watu wamejaa kanisani na waume zao wamejaa bar. It is not about being selfish ni suala la furaha yako. It's your life, it's your choice.
 
Hajipodoi sababu hana hela hao wenzake unaona wanapendeza wanagharamiwa. Mpe laki 3 kila mwezi mwambia unapenda asukie lace wgi, Ndo bei yake ikiwezekana nenda luluz hair kamnunulie mshushe saluni ashonwe Mpe laki kila mwezi atengeneze kucha. Mlipie gym 250,000 muwe mnaenda wote mwambie unataka mpendeze wote.. Anzeni diet za edmark ni nafuu elfu 99,000. Mpige shopping anunue nguo unazopenda wewe avae. Atapendeza tu. Hio ndio gharama ya mwanamke kupendeza. haishuki laki 5 kila mwezi. Akishavijua ...uwe unamwachia awe anaenda mwenyewe. Na mnunulie roses kila mara mwambie unampenda na akipendeza msifie haswaaaa. hadi kila siku atake kupendeza kwajili yako
Kama wewe ni mwanaume basi mwanamke wako ana bahati sana
 
Hamna kitu cha kipumbavu kama kuishi na mtu uliopoteza mapenzi naye kisa unagopa kuvunja ndoa, kuogopa jamii, kuogopa utashindwa kutunza watoto. Hivi mbona hamuogopi vitu vinavyotisha zaidi ambavyo vinaletwa na hizi ndoa zilizokosa upendo? Ulevi, Umalaya, Magonjwa ya zinaa, pressure, Domestic violence, Stress, Watoto wa nje ..etc. Siyo coincidence unakuta wake za watu wamejaa kanisani na waume zao wamejaa bar. It is not about being selfish ni suala la furaha yako. It's your life, it's your choice.
Umesema kuishi na mtu uliyepoteza mapenzi naye,sasa nikuulize nini kilifanya mapenzi yapotee?kama mwanzo yalikuwepo na sasa yamepotea maana yake unaweza ukayarudisha.hata ukikimbilia kwa mwingine na huko mapenzi yakipotyea utakimbilia tena kwa mwingine?Nikuulize vipi wazazi wako walipotezeana mapenzi au wako pamoja?Ndoa ni zaidi ya kufanya sex na mvuto wa mapenzi,mapenzi ni muhimu katika ndoa lakini ndoa si mapenzi pekee,shida yenu mnaingia kwenye ndoa mkiwa mmewaka tamaa tu the maximum,mnawaza sex na kusahau ndani ya ndoa ni zaidi ya sex.Wewe kama baba una wajibu wa kuitunza familia yako na kuilinda sasa wewe waza sex tu,matokeo yake mnakuja hapa mnalialia.Na hii inaonyesha vijana wengi siku hizi mnaingia kwenye ndoa bila kujua nini maana ya ndoa.
Ndoa inapokosa upendo kuna kitu kimesababisha,ndoa haileti ulevi wala ndoa haileti umalaya,mtu atalewa kwa sababu ya upumbavu wake ,unatatizo kwenye ndoa suluhisho siyo kutoka nje ya ndoa yako au kulewa.Hizo mnafanya hazisaidii kutatua tatizo lako bali unalikuza,kuna watu walitoka kwenye ndoa na wakapata watoto huko,baada ya muda matatizo ya kwenye ndoa yakaisha,ila mtoto wa nje anabaki,hapo unalakujibu kwa Mungu wako.
Magonjwa ya zinaa yanatoka wapi kwa wanandoa kama wakiwa waaminifu?Kama gonjwa litaingia maana yake kuna moja wa wanandoa hakuwa mwaminifu.Next time uandike vitu vya maana,ili utupe ugumu kukujipu.Samahani wewe uko kwenye ndoa?
Nakuona unasisitiza sana "furahja yako' hata mashoga nao wanataka ":furaha yako" sasa nikuulize wewe ni shoga?Je siku mmoja wa watoto wako akiwa shoga kwa sababu kama unayotupa hapa ya kupata 'furaha" wewe utajisikiaje?
Wewe si unasisitiza furaha ya mtu na mimi nilitahadhalisha kwamba furaha ya mtu ni muhimu ila asije akafanya mambo yatakayowadhulu wengine au yasiyo ya kimaadili kisa anataka furaha yake.
Kama watu watajaa makanisani na waume zao wamejaa baa hiyo ni shida ya aliye bar,na imani yake au dini yake huko anakoabudu.najua kuna watu wengi wanadini zao lakini wanaenda kuzimu kwa hiyo wao kujaa bar siyo issue kwangu.
Watenda kuzimu kwa sababu ni wanafiki,hawaishi vile ambavyo dini zao au imanni zao zinawafundisha kuishi.Wanatafuta kuwapendeza watu kuliko Mungu.
Hayo mambo ya ulevi,violence na mengine ukiwa ndani ya Yesu kwelikweli na si kwa unafiki huwa yanakufa natural death,karibu umpokee Yesu hutakuwa na komment za watu waliotekwa na tamaa za miili wakitumia akili zao badala ya kumwomba Mungu awaongoze katika maisha yao.
 
Nimeoa miaka nane iliyopita na nimepata watoto watatu. Ila sasa naona kama nilikosea kuchagua sababu huyu mke wangu tulianza mahusiano tukiwa shule tukaenda hadi Chuo kikuu pamoja.

Sasa naona wanawake wengine wazuri na wanaojipenda zaidi yake na nikiangalia yeye alivyo hajipodoi podoi yupo yupo tu na hana sexy body yaani havutii kabisa mpaka saa nyingine najisikia aibu.

Yaani nashindwa kujua nifanyeje kumwacha namwonea huruma sana.
Akili zako ni robo kilo aisee...
 
TULIA NA MKEO LEA WATOTOT ACHA UPUMBAVU WEWE,
WEWE MWENYEWE UNAONEKANA MSHAMBA TU .
 
Hongera umekuwa muwazi, wanaume wengi hilo linawaokea sana, pole sana, ila kwa mwanamke ukishazaa ile load ya kubeba mimba inaacha scar ya tumbo kubwa, especially kama mama alizaa kwa kisu au alilishwa vizuri alipokuwa amejifungua ama hakufunga tumbo. Kwa watoto watatu kuzaa peke yake kunaharibu tumbo. Umepata watoto at the expense of her loosing her attractive figure. Hiari yako uende kwa hapo wanaovutia (ama hawajazaa, au walizaa kwa kawaida, au kwa vyovyote vile ila weng wa wanaume wanaenda kimya kimya. Nendaga tu kimya kimya, ila umepata watoto kwa yeye kupoteza mvuto wake.
Wanaume hawakuumbiwa shida especially when they have got money, jiendeege tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom