Najuta kuwa Raia Katika Nchi Ambayo Tambwe Hiza ni Raia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Najuta kuwa Raia Katika Nchi Ambayo Tambwe Hiza ni Raia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwanaharakati_msemahovyo, Mar 23, 2008.

 1. m

  mwanaharakati_msemahovyo Member

  #1
  Mar 23, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tambwe Hiza ni moja kati ya wananchi wa jamhuri hii waliowahi kuibaka siasa.Ni kinuka mito.Ni mwanasiasa mbinafsi aliyethubutu kuweka maslahi binafsi mbele na kuweka ya taifa kando.Binafsi ninajuta kuwa mwananchi katika nchi ambayo ndugu huyu Tambwe Hiza ni mwananchi pia.

  Tambwe ana hulka ya kuandika makala katika baadhi ya magazeti hapa nchini.Aina ya makala anayoyaandika huwa yana muelekeo wa kutaka kuonekana na wakubwa wa nchi hii ambao ni vigogo katika chama tawala ili mradi atupiwe mfupa na mkono wake uende kinywani.

  Ukimtafakari kwa kina huyu ndugu,utashawishika kwamba anaweza kuandika makala ambayo yatatetea mtu mkubwa katika chama tawala ili mradi atupiwe mfupa mnono.Hku ni kufilisika kimawazo na ni kiwango cha juu kabisa cha usaliti wa nchi na pia ni kutukana taaluma ya uandishi wa habari.

  Majuzi nilisoma makala yake ambayo alijaribu kuwashawishi watanzania ili Rais wa nchi atoe presidential decree kuwasamehe mafiadi walioiba fedha zetu BOT.Huyu ndugu amefikia kiasi cha kuchefua watanzania wenye uzalendo wa kweli na anajaribu kupandikiza mbegu ya ubaguzi na kutoheshimu utawala wa sheria nchini.

  Katiba ya jamhuri ya Tanzania inasisitiza kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria.Hakuna mtu awaye yeyote aliyeko juu ya sheria.Tambwe Hiza analeta siasa katika utawala wa sheria.Huyu ndugu ni wa kuogopwa kama ukoma.Uzalendo ndani ya Tambwe Hiza Hauko.Siasa anazoendesha ni ya kulinda tumbo lake hata kama akiuza nchi.Ni siasa chafu ambazo mwaliu alizikataa!!
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  This is not fair accusation. Kama una-mind kuwa na mwanasiasa ambaye ameweka maslahi yake mbele kama unavyomlaumu Tambwe, what abaout Majizi yanayokwapua hela zetu, what ambao wanaua kaka zetu na dada zetu, what about mafisadi, wauaji na wengine wengi ambao ni viongozi lakini ni wezi kuliko hata vibaka, hao je unaona wana afadhari kuliko Tambwe. Do you have anything personal with Tambwe???????????
   
 3. Allah's Slave

  Allah's Slave JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa naelewa kwa nini tumevamiwa hapa JF
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  NILIDHANI UTAJUTA KUHUSU MAFISADI KUWA RAIA WA NCHI HII,ROSTAM,MBOWE etc KUNA JINGINE ZAIDI YA TAMBWE KUANDIKA MAKALA YA KUTETEA MAFISADI?
  BUNGENI AKINA MASILINGI WALIKUWA SIDE YA AKINA ROSTAM......WAKATI WEWE UNAJUTA TAMBWE KUWA RAIA KUNA WATU WALIMKABIDHI MADARAKA MAKUBWA SANA KWENYE CHAMA CHAO.......WAO WALIJIVUINIA TAMBWE KUWA RAIA.....JE WALIKOSEA.....?
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  JF nako siku zingine kuna vituko. Nchi yoyote ina watu wa kila aina, kuanzia
  akili mpaka zuzu; vichaa mpaka wazima, sasa mwenzetu utaijutia nchi yako mara ngapi?

  Wewe timiza wajibu wako, nchi taratibu itabadilika. Ulichoandika hapo juu, kinakufanya usiwe tofauti sana na huyo Tambwe unayemsagia.

  Mkuki ni silaha nzuri sana, lakini angalia umeuelekeza wapi kabla ya kuanza kuurusha.
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Faida za pasaka.....
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nadhani mtoa mada alikuwa akiimanisha kuwa Tambwe ni hatari zaidi hana tofauti na mafisadi na mijizi ya cake ya taifa...ingependeza kama angesema anajuta kuwa raia wa Tanzania na Tambwe hiza Pamoja na akina Rostam et al (Lowassa, wezi wa EPA, majambazi, wazee wa unga)...
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huyu Tambwe nilishe sema habari zake .Si kwamba ni mwanasiasa na raia mwema hapana na ndiyo maana hakudumu kwenye upinzani maana kote alijulikana kwa fitina na tamaa ya madaraka .Majungu na uzinzi .Leo karudi CCM kesha pata kaeneo kake ka kula pale PTA kwenye external Trade nk .Yote haya nilisha yasema na yeye kama Makamba wote wanaongea kuzima uogo.He cannot be trusted na hawezi hata kubebeka .Kama huamini jiulize kwa nini alibebwa sana na Makamba kwa jina la Utanga na bado akamwagwa akiwa anaomba NEC , Uenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke na hata Ujumbe wa nyumba kumi kaukosa ?By nature amekuwa na biashara haramu kibao .
   
 9. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hivi kosa la mtoa mada ni lipi?Hivi kwa kuwa kuna ufisadi katika tarkiban kila eneo la nchi yetu then inakuwa dhambi kujadili eneo mojamoja eg hilo la Tambwe kuandika makala mufilisi?Mie nimeielewa vizuri sana hoja inayozungumziwa hapa na kwa hakika mtu yeyote mwenye akili timamu anapaswa kushangazwa na kauli za ajabu za Tambwe kutaka Rais awasamehe mafisadi.Baada ya jaribio lake kuingia NEC kushindikana sasa amegeuka kuwa political prostitute....

  Anyway,let's be fair to mtoa mada.It's a sensible arguement put forward in artistic way.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mlalahoi umesema maneno mazito hayo nakubaliana nawe .
   
 11. B

  Bakari Member

  #11
  Mar 25, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watetezi wa mafisadi wako wengi na t hiza ni 1 wao.shit
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,657
  Trophy Points: 280
  vibweka vya PASAKA
   
 13. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wangwe usimsahau kuwa ni miongoni mwa fisadi wa demokrasia
   
 14. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2008
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Tambwe anaonekana kwa kuwa wewe hauonekani ama unaogopa kuonekana......
   
Loading...