Najuta kupoteza muda wangu kuangalia Ujinga uliopo Kwenye series ya money heist

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
5,309
2,000
Kwa mara ya Kwanza toka 2009 nilipoanza kuchek series za 24 na prison break nilishamaliza kufananisha na series yeyote duniani nakumbuka mwaka 2010 nilichek pia series moja tamu Sana inatwa traveller,hii movie haikutoka tena na sielew sababu ya kushindwa kuchezwa mpaka leo..

Miaka mingi imepita bila kujichosha akili Yangu Kwa kuangalia UJINGA wa kile kinachoitwa series Kali mpaka mwaka huu nilipoamua kuchek series ya money heist (baada ya watu wengi kuifananisha na prison break na 24 hasa hapa jamiiforum).
Jumamosi iliyopita niliona Bora na Mimi nijiridhishe na hiyo movie kama kawaida nikaanza na season ya Kwanza nikaona holaaa!!! Sioni cha kutumia akili wala nini!! Nikajipa moyo nikamaliza Ila kikubwa nilichokuta ndani ya hiyo movie ni upumbavu na upuuzi tu.

Season 1: jamaa wameingia ndani ya bank na kinachofanyika humo ndani ni mapenzi Tu badala ya kupanga namna ya kuondoka na pesa hawa wezi wanaanza kuchagua kila mmoja na hostage pia kuna mdada mmoja Kwenye hii movie anaitwa Tokyo huyu muda wote anapigwa miti Tu na kusagana(movie imejaa ngono kama porn)

Season 2: huku nako hamna kitu kabisaaa nilishangaa kuona hawa wezi hawana hata mpango wowote wanaofanya ili watoroke zaidizaid ni hizo mishe za kitoto za professor za kumtongoza inspector...
Tukirudi Kwa professor ambae wadau wanamfananisha na jack Bauer au Michael Scofield ni bure kabisa Hana lolote la maana, huyu lofa(professor) kazi yake ni kujifungia ndani Kwenye chumba cha Siri na kupiga simu ndani ya bank na kuwapa mbinu za kutoroka Kwa kifupi Hana tofauti na operator wa tigo .

Season 3 nayo hakuna maajabu zaidi ya Tokyo kutoka ndani ya mint na kwenda nje pia anakamatwa na baadae anafanikiwa kuwatoroka polisi Ila cha ajabu anarudi tena ndani ya bank ili akagongwe miti(ebu fikiria mtu anatoroka polisi chini ya ulinzi mkali lkn baadae anaamua arudi tena ndani akakutane na wenzake badala ya kupanga mipango ya kuwaokoa wenzake akiwa nje)

Season 4: mara baada kufanikiwa kuiba pesa(movie haijatuonesha waliondoka vipi Spain na kukimbilia Caribbean countries Ila tunaona Tu jamaa wapo huko wanakula bata).
Nilishangaa kuona Kwa mara ya Kwanza majambazi ni mashoga kuna kipande kinaoneshwa jamaa wanakula mate(hii movie haifai kuangalia na watoto Hilo ni angalizo hata Kwa wale wenye kuipenda hii movie Yao watakubaliana na Mimi)

Mwisho katika season zote 4 sijaona sehemu yeyote ambayo professor ametumia akili au tukio Fulani ambalo Lina uhalisia hakuna kitu kama hicho, Kwa wale ambayo wanataka kuitafuta hii movie nawasihi haina haja ya kusumbua muda wao... Movie ambayo muda wote Tokyo anapigwa miti itakusaidia nini?

Kuifananisha money heist na 24, traveller na prison break ni dhambi kubwa tena Kwa mtu ambaye asiyejua lolote na mshamba wa movie asifananishe na UJINGA wa professor na akina jack Bauer
 

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
5,309
2,000
Nimeangalia season one na two. Ulichokiongea hapo so kweli.

Unaposema walikaa ndani kwa ajili ya mapenzi badala ya mipango ya Naman ya kutoka, unakuwa umedanganya kwa sababu wao walikuwa wanachapisha note na walihitaji kukaa siku nyingi ili wachapishe zaidi na utagundua kuwa walikuwa wanafanya matukio mengi ili kuendelea kukaa mule ndani kwa siku nyingi zaidi. Lakini pia mpango wa kutoka mule ndani ulikwisha pangwa muda mrefu kabla hata hawajaingia ndani, na ndio maana walipoingia ndani tu, Moscow alianza kuchimba tunnel ambayo ingekutana na tunnel iliyokuwa inachimbwa kutoka upande wa professor.

Ingetosha kusema money heist siyo Kali Kama au zaidi ya prison break kwa Sababu ambazo ungeandika vizuri kabisa, kuliko ulichoandika ambacho kinasadifu kwamba HAUJAIELEWA KABISA MOVIE

kutoielewa kwako hii movie kunatokana na either kuangalia ikiwa imetafsiriwa kiswahili. Lakini pia inawezekana hukuielewa kwa sababu ya wao kutumia lugha ya kispanish na wewe kuamua kuiangalia hivyo hivyo bila ya kutafuta subtitles za kiingereza na kujaribu kuelewa Kila tukio.

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
Nimechek ambayo wanaongea kiingereza Mkuu
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,698
2,000
Hebu pendeoeza series nyingine tofauti na hizo ulizotaja.

Meanwhile... Angalia zifuatazo
Tredstne
Hanna

Zafaa kwakupotezea muda wakati tunasubiri series tamu nyinginezo
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
23,263
2,000
Kiukweli mimi nimeishia 3,ilianza kunikera pale watu wako bank,badala ya kufanya mambo kwa tahadhari ya hatari iliyopo,mara kuna wapenzi humo wana yao.

Nikaanza kuhisi utopolo.labda mbele huko ilichangamka sijui.
 

Kelevra

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
1,055
2,000
Traveller....walitukosea sana kuachana kitu..tangu miaka hiyo hadi Leo jina la Will Traveller halitoki kichwani mwangu.
Money Heist imepoteza mvuto kiasi baada ya watu kuanza kuifananisha na Prison Break tatizo likaanzia hapo.
Angalia tu "Banshee" ni ya muda but inaonekana inakufaa kwa Series ulizo mention hapo zipo 4 seasons mzigo ulishaishaga.
 

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
3,742
2,000
Sasa ulitaka wacheze vile wewe unataka..afu ile movie hawakucheza ku entertaining watu kama sisi ndio maana unaona hivyo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom