Najuta kumsema Rais Vibaya. Nipo ndani nimeambiwa nisitoke nje nyumba yangu imezingirwa

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
Nimeamka asubuh leo nlikuwa najiandaa kwenda kazini nlipowasha simu zimeingia meseji nyingi toka kwa majiran zangu wakinionya nisitoke nje maana nyumba yangu imezingirwa. kweli nimechungulia nimekuta nimezingirwa. nikakumbuka ni jana tu nlimsema rais kwa maneno makali kwa sababu ya hasira. lakini jaman nchi hii serikali itusaidie tupate uhuru wa kuongea. maana sasa hata ukiongea tu neno kidogo inakuwa shida.

tatizo lilikuwa kwenye text zangu nlizotuma whatsapp na facebook kuwa rais ni bwege na zombie kama aliyetoka yeye alikuwa ni zuzu, zezeta na zombiest. hayo yalikuwa maoni yangu kwa sababu niiangalia kiukweli huyu aliyepo sasa toka amekabidhiwa urais wa hii ngo inayojihusisha na mambo ya mazingira hajafanya lolote la maana. hata kuja kututembelea sisi wa maeneo ambayo yana mkondo wa maji.

nilivyosema maneno hayo kuna mtu akasema kuwa atamwambia kuwa nimemsema vibaya. lakini mi nlijiuliza kama huyu ni rais wa hiyo ngo ambayo inahusu mambo ya mazingira na ardhi oevu hajali kutembelea watu wake kujua nini wafanye hasa kitakapokuja kipindi cha masika. nani atatusaidia?

leo asubuh ndo naambiwa nyumba yangu imezingirwa na maji kote. na kuwa nisitoke nje maana inaweza kuwa hatari kwa maisha yangu. nahisi ni kwa sabab ya maneno nliyosema kuhusiana na rais na sasa ndo haya madhara yake. maana kama mvua jana ilinyesha kidogo tu wala haikuwa kuuuubwa kivileeee.
 
Tayari!!
9393370_orig.jpg
 
Unajifanya uko Chit chat, kumbe unatukana kweli !!! Jiulize kama unaweza msemea Baba yako maneno mabaya kama hayo hata kama ni matani.
 
Ukiwa huna nidhamu ni kielelezo tosha umelelewa katika misingi mibovu, Kwa hiyo unataka kuendeleza jamii ya misingi mibovu kwa sababu umelelewa katika misingi mibovu, haita kubarika daima. Nidhamu na heshima ni nguzo ya kwanza Duniani ya kuishi kwa amani na furaha.
 
Pole sana mh Rais wangu , ila naomba vyombo vya ulizi na usalama vichukue hatua kali sana kwa hawa watovu wa nidhamu , haiwezekani mh Rais ukadharirishwa namna hiyo, tabia mbaya ya namna hiyo haifai kuachwa hivo bila kuchukuliwa hatua, sio vibaya wakafungwa hata maisha jela ili iwe fundisho kwa wengine.
Pole sana my Rais
 
Pole sana mh Rais wangu , ila naomba vyombo vya ulizi na usalama vichukue hatua kali sana kwa hawa watovu wa nidhamu , haiwezekani mh Rais ukadharirishwa namna hiyo, tabia mbaya ya namna hiyo haifai kuachwa hivo bila kuchukuliwa hatua, sio vibaya wakafungwa hata maisha jela ili iwe fundisho kwa wengine.
Pole sana my Rais

kweli kabisa! hichi kitendo cha kutukana siyo msingi wa taifa letu! na nina kichukia sana! hatua lazima zichukuliwe! muheshimiwa RAIS lazima aheshimiwe sana na kwa heshima zote na kumwombea!
 
Hakuna Uhuru usiokuwa na mipaka tuache kuiga kila tunachosikia eti ni maendeleo ya dunia ya sasa.
 
Back
Top Bottom