uwiiiiiiii
JF-Expert Member
- Jul 11, 2016
- 341
- 365
Habari zenu wadau,
Nimeamua kulileta hili si kwa lengo baya naombeni ushauri wenu maana nasikia kuumwa kichwa nimechanganyikiwa sana.
Naishi na mwanaume na tuna mtoto mmoja pia ninaujauzito mwingine pindi tunaanza mapenzi na huyu mwanaume tuliweza kukaa na kuongea mengi ya kila mmoja ya nyuma tukaridhiana mapenzi yakaendelea.
Baada ya muda huyu bwana kupata kazi mkoa mwingine mwenzangu amebadilika sana, dharau, umalaya, pombe, hajipendi, napigiwa na wanawake zake wa nyuma, kejeri, kibaya zaidi si mwanaume anayejitambua, ni mtu hana malengo huwezi kumshauri cha maana akafanya, kutokanana na umalaya na tabia nyingi nilizoona ukweli nimegundua ni mtu hana mapenzi na mimi. Niligundua hili siku moja alinipiga bila sababu ya maana huku nikiwa mjamzito.
Naamini pesa zinatafutwa hata pindi nilipokutana nae hakuwa nazo kama aliangaika naamini ipo siku na mimi nitapata, nachojali mimi ni amani yangu, napenda furaha vingine vitakuja, naumia kwa mtoto wangu pamoja na ajaye kuishi bila baba maana nimechoka na manyanyaso, naona ni heri niangaike ili niweze kuwalea watoto wangu.
Naombeni ushauri wenu wapendwa.