Najuta kujenga kibanda changu uswahilini. Mswahili ni mtu duni sana

Kwenye huu uzi ukiufuatilia vizuri utangundua watu wengi wanashangaa jamaa anaishije na watoto wote hao bila mke. Swali langu ni kwamba kwanini single mothers ni issue ya kawaida kwetu ila linapokuja swala la usingle father haiwezekani?
 
upo sahihi,mi nakumbuka wakati nipo form 6 nilikua nasoma day school sasa jirani yetu kulikuwa na katoto fulani kapo darasa la kwanza ,kalikuwa kanapenda sana kuja kukaa na maza pale home ghafla nikajikuta tu namwambia maza awe anakarudisha kwao na kalikua kakija maza hayupo nakafukuzia mlangoni bila sababu tu,baada ya muda wa miezi kadhaa maza alimsikia mama yake kale katoto anakakanya kuja kwetu eti kisa kuna mtoto wa kiume (mimi) kwamba nitakabaka. hiyo kauli ilitusikitisha sana. nikawaza je ingetokea siku kamebakwa huko na mtu mwingine alafu mimi ningekua na mazoea nako si mama yake angeweza kusema ni mimi
Daahhh very sad
 
Chakula tu kinaua ujirani? Kuna siku utakuja kupata janga hao majirani watakucheka! Wewe jamaa ni mvulana sio mwanaume!
 
Baada ya kujibanabana hatimae nikajenga kibanda changu uswahilini.

Jirani yangu ana mpangaji wake. Huyo mpangaji wake ana mtoto mdogo (4yrs). Mimi nina watoto watatu mmoja la Saba wa kike wawili wakiume (5) and (3).

Sio kwamba Mimi ni mchoyo na mbinafsi, la hasha! Ila hakuna kitu nakichukia katika maisha yangu kama vikwazo. Hii familia ya huyu mtoto mdogo inashindwa kumdhibiti mtoto wao wa kike (4yrs).

Msosi umeiva huyo kaibuka. Tatizo sio chakula. Anakuta watoto wangu wanakula nimewawekea nyama kila mtu na vipande vyake Kwa bajeti yeye huyo mtoto doezi anafika anachukua plate ya chakula anan'gan'gania kisha anaanza kulia eti hataki watoto wangu wale. Hapo mama ake yupo nje.

Siku nyingine anatoka huko kwao anakuja kunywa maji kwangu. Akiwa anakula na wanangu wakitaka kunywa maji analia anataka yeye ndio awe wa kwanza kunywa.

Kero kero zipo nyingi sana. Mimi nilikuwa sina habari hizo cause sishindi home. Last week nimerudi home mapema nakuta madogo ndio wametoka shule halafu eti huyo mtoto analia hataki wao wale chakula walicho andaliwa na dada kazi kwamba kidogo apewe yeye tu.

Na analia kwa nguvu kama kachomwa na mkuki vile. Hapo mama ake yupo nje. Huwa naambiwaga upuuzi huu but sikuwahi kushuhudia. Nikasema hawa wanafanya huu ujinga kwasababu wananiona nimekaa Kikristo sana.

Basi nilimchukua huyo mtoto nikamnyanganya hiyo plate nikamshika nje hadi kwa mama ake nikaanza kumchana mama ake.

"Wewe Mwanamke msiniletee maswala ya ki...nge. Kwangu sio kituo cha kulelea watoto. Mtoto wako anafanya us..nge humkanyi.." Kuanzia leo sitaki kumuona mtoto wako nyumbani kwangu.

It was a surprise for her kwasababu nadhani alikuwa ananiona nimekaa kisomi kisomi na anavyosikiaga naweka ngoma za gospel kwangu basi anajua huyo Mtakatifu Matayo.

Basi kuanzia siku hiyo adabu imekuwepo. Mazoea hakuna tena. On top of that nimeanza kuwa napiga kwa nguvu nyimbo za kigumu.

Ngoma kama Hit 'Em Up na nyimbo nyingine za kigumu gumu ili at least wajue huyu jamaa msela hataki mambo ya kidwanzi.

Majirani kushirikiana kwenye mambo mengine sio kukerana kerana kiasi hicho. Kama una njaa njoo ukope hela umpikie mtoto wako sio kumuacha aje awakere watoto wangu.

Toto lako kula kwangu halafu siku likipata tatizo si ndio mwanzo wa kushikana uchawi huo. Sisi ngozi chafu huwaga sio wastaarabu kabisa

Ngoja nitafute hela nipige Mwanaukome. Ndio maana matajiri wakijenga nyumba zao huwa wanazipiga stop nonsense

#Walayhi nimeona umuhimu wa kuoa. Ukiwa na mke majirani hawawezi kufanya upuuzi kwa sababu wanajua mama mwenye nyumba Hawezi kukubali. Ila wakiwa wanakuona kibachela bachela hivyo wanakuchukulia ki-gentleman sana.
hahaha Hit Em Up
 
Back
Top Bottom