Najua wengi hatumpendi Rais Magufuli ila tunayaonaje haya?

lloydsam

Member
Nov 8, 2015
42
55
NAJUA WENGI HATUUPENDI UTAWALA WA RAISI MAGUFULI ILA TUKUMBUSHANE TUU:

1: Takribani miaka 107 imeshapita tangu zilivyotengenezwa reli nchini Tanzania na wakoloni mnamo miaka ya 1912, Raisi Magufuli amekuwa raisi wa kwanza Tanzania kutengeneza tena RELI.

Na kama ilivyo kawaida ya TANZANIA kufanya Project bora zaidi ya wenzetu East Africa na hata Africa kwa ujumla, Magufuli akaamua kutengeneza SGR bora zaidi kuliko ya wenzetu WAKENYA ambayo yao inatumia matreni ya diesel tofauti na zetu zitakazokuwa zinatumia njia za umeme kama Marekani & China.

Kwa africa.. Morocco, Ethiopia & South Africa ndizo nchi pekee zenye mradi kama huu.

2: Ndani ya miaka 57 tangu tupate uhuru, serikali ya Tanzania imefanikiwa kujenga hospital 77 tuu mpaka sasa ila kwa kipindi cha mwaka 1 na nusu au miezi 18, MAGUFULI amefanikiwa kujenga Hospital Mpya 67 na vituo vipya vya Afya vipatavyo 352 Nchi nzima. Na wanatarajia kuongeza vingine 27 katika bajeti ijayo..

HII NI MIRADI ILIYOWAZI, WAKENYA TUNAWAACHA MUDA SI MREFU.. NIMEWATAJA WAO MAANA NDIO KAMA WATANI WETU WA JADI KWENYE SUALA LA MAENDELEO IN EAST AFRICA.

Wakiwa katika mkakati wa kupanua Bandari yao ya Mombasa, TANZANIA nayo imeshatoa fungu la kupanua Bandari zake zote ambayo Upanuaji wa Bandari ya Dar Es Salaam utahusisha ujengaji wa Port kwa ajili ya Cruise ship, zile meli kubwa za starehe zitakazokuwa zinaanza kutunga nanga nchini kwetu na kushusha Watalii wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwekezaji haufanywi ili eti uwe wa kwanza kufanya jambo fulani bali ni kutokana na mahitaji na tija ya mradi husika.
Hakuna mtu mwenye akili timamu atakaesifia kujengwa reli au kununuliwa ndege ikiwa mwisho wa siku zitaendeshwa kwa hasara na kugeuka mzigo kwa serikali. Tumeshafanya sana huu ujinga awamu ya kwanza lakini nadhani ubongo wa mwafrika hauwezi kujifunza ndio maana tunaburuza mkia kwenye kilakitu.
 
Hivi reli ya Tazara ilijengwa lini? njoo taarifa sahihi kwanza. Hizo hospital 67 zimejegwa wapi? Maana serikali ina hospital kubwa mbili tu zenye hadhi ya kimataifa Muhimbili na ndugu yake Mloganzila, hizo zinazoitwa hospitali za rufaa ni majanga kwasababu tu ya umaskini ndo maana tunatibiwa huko

Sent using Jamii Forums mobile app
Reli ya TAZARA ilifunguliwa mwaka 1975 nahisi hata wazazi wako walikuwa wameshazaliwa

Naomba unipe maana ya Hospital coz kutokana na maelezo yako ambayo ume define Hospital ni Muhimbili & Mloganzila tuu then i guess wengi hatujui.. Maana mi bado najiuliza zile za Amana, Temeke, Sinza ni zahanati au ni nini

Sasa Mbona hapendwi??
 
Hii ndio shida ya akili zinazotokana na elimu duni na ya hovyo ya Tanzania, uwekezaji haufanywi ili eti uwe wa kwanza kufanya jambo fulani bali ni kutokana na mahitaji na tija ya mradi husika.
Hakuna mtu mwenye akili timamu atakaesifia kujengwa reli au kununuliwa ndege ikiwa mwisho wa siku zitaendeshwa kwa hasara na kugeuka mzigo kwa serikali. Tumeshafanya sana huu ujinga awamu ya kwanza lakini nadhani ubongo wa mwafrika hauwezi kujifunza ndio maana tunaburuza mkia kwenye kilakitu.
So unachosema ni kwamba, Hakutakiwa kujenga Relii Inawezekana wenzio tupo tupo kama ulivyosema kutokana na elimu yetu duni, so embu tuambie wewe mwerevu je ulitaka ajenge nini maana Unaposema nataka kuanzisha Nchi Ya Viwanda it means una miundombinu ya kutosha ambayo itawavutia wawekezaji ili waweze kuwekeza kwenye Nchi yako..

Sasa anaanza kuweka miundombinu ya kisasa na kuboresha au kufufua iliyokufa mnamkebehi afu at a same time bado mnakaa vijiweni na kuanza kuulizana hivyo viwanda alivyosema viko wapi.. Yaani hapo tuu ndipo mnaponiachaga hoi mtanzania mimi nisie na elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reli ya TAZARA ilifunguliwa mwaka 1975 nahisi hata wazazi wako walikuwa wameshazaliwa

Naomba unipe maana ya Hospital coz kutokana na maelezo yako ambayo ume define Hospital ni Muhimbili & Mloganzila tuu then i guess wengi hatujui.. Maana mi bado najiuliza zile za Amana, Temeke, Sinza ni zahanati au ni nini

Sent using Jamii Forums mobile app
Ma-architect au wabunifu wa majengo na madaktari wanasema hizo unazita hosipitalni vituo vya afya ( health centres).
Dogo we bado sana katika ulimwengu wa wajuvi wa mambo
 
Magufuri anafanya vizuri lakini kuna baadhi ya maeneo ayafanyie kazi;
1. Mapato --Bado suala la ukusanyaji mapato liko chini ,toka aingie madarakani TRA report zao ni trl1.3,1.2,1.5 etc, ina maana katika miaka yote hiyo minne na uwekezaji unaofanyika bado makusanyo ya kodi ni yale yale tu? TRA waandae mfumo mzuri ambao utahakikisha atleast 60% ya watanzania na wafanyabiashara wanalipa kodi, pia kila mwaka wawe na target ya kuongeza makusanyo, sio wanakuwa wanaongeza kutoka trl 1.3 (2019) hadi trl1.3 na mil 200 (2020),this is the joke, kama mwaka huu wamekusanya trl1.2 tunategemea mwakani iwe trl 1.5 au trl 2, wafikirie Zaidi .

2. Viwanda, kuna kiwanda kama mchuchuma, serikali ni lazima wafanye kila liwezalo kiwanda hiki kisimame miaka hii, kama wawekezaji wanasuasua serikali inaweza ingia ubia nao, au serikali ikope na isimamie vizuri tuuze chuma tukirudisha mkopo taratibu, ni lazima tuuze chuma kuongeza pato la taifa. Sawa tuna viwanda vingi tunajenga na kuzindua lakini viwanda hivyo ni vidogo vidogo ambavyo havitoi ajira nyingi kwa vija ukilinganisha na kiwanda kama cha mchuchuma kikianzishwa, kwahiyo Magu priority yake na wizara ya fedha /uwekezaji ingekuwa kwenye mchuchuma, chupa tu tukisimamia vizuri tunaweza kutoka.
 
Hizo hospitali 67 zimejengwa wapi?

Hii serikali ya majigambo na hawataji hizo hospitali wamezijenga wapi, ni sawa na hadithi za viwanda, unasikia tumejenga viwanda 4,500 na vimeajiri watu 36,000,unajiuliza inamaana kila kiwanda kimeajiri watu 8? Na hawasemi vimejengwa wapi.

Sasa kuna hadith ya hospitali 67, unajiuliza kwa hela ipi? Mama hospitali ya kigamboni tu haina hata xray machine miaka yote, madaktari hawajaajiriwa miaka 5, hizo hospitali zinatibu na wachawi?
 
Utajuaaje ukiwa uko bize na migalala +pornography daily
Hivi reli ya Tazara ilijengwa lini? njoo taarifa sahihi kwanza. Hizo hospital 67 zimejegwa wapi? Maana serikali ina hospital kubwa mbili tu zenye hadhi ya kimataifa Muhimbili na ndugu yake Mloganzila, hizo zinazoitwa hospitali za rufaa ni majanga kwasababu tu ya umaskini ndo maana tunatibiwa huko

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi reli ya Tazara ilijengwa lini? njoo taarifa sahihi kwanza. Hizo hospital 67 zimejegwa wapi? Maana serikali ina hospital kubwa mbili tu zenye hadhi ya kimataifa Muhimbili na ndugu yake Mloganzila, hizo zinazoitwa hospitali za rufaa ni majanga kwasababu tu ya umaskini ndo maana tunatibiwa huko
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni vema akajibu kwa ushahidi,orodha yake,hivyo vitu vilipo na picha juu.Wapiga zumari wamekuwa na mbinu za ajabu sana ili mradi kuijenga hadaa tu.
 
Sasa Mbona hapendwi??
BINAFSI NAAMINI HAPENDWI KWASABABU HIZI

1: Chama Alichopo, maana watu walishakosa matumaini kabisa na chama hicho so Raisi alipopita tena kwenye chama kile kile kila mmoja kaishiwa pozii.

Sasa shida ni kwamba, kutokana na watu wengi kuamini kuwa CCM haiwezi kuwaletea maendeleo wayatakayo na badala yake kugawana Kodi zao na wengine kuwaletea dharau kabisa Wananchi bila hata haya kwa kusimama mbele ya umati na kudiriki kuyaita Mabillioni ya kodi zao vijisenti basi kila anachofanya Mh. Magufuli bado wanahisi ni propaganda hali ya kuwa mambo yanafanyika kwelii..

Nina rafiki yangu mmoja na smartphone anayo ila bado haamini kama Ujenzi wa reli unafanyika maana anaishi Arusha, pia bado haamini kama ujenzi wa Ubungo Interchange umeshaanza pale ubungo na ukimuambia Daraja la Salenda ndo kabisaaa hataki kusikia anasema sisi bado kabisa labda 2050 Je unahisi ni Watanzania wangapi wameathirika na hili ikiwa bado Wapinzani wamekuwa wakikosoa kila alifanyalo na kusema ni uongo, Huku wakidai hizo sio Kodi za wananchi na at a same time Wanadai WORLD BANK na Mataifa makubwa yamekataa kumpa mikopo sasa swali ni Je, hizo pesa anatoa wapiii hapo ndo ujue kuwa watu wapo kumkosoa tuu na kuzidi kuwapotosha wananchi just because Magufuli yupo CCM

KAMA UNAAKILI TIMAMU BASI JIBU NI MOJA KATI YA HAYO MAWILI HAPO JUU

I mean, Hii miradi ni Kodi zetu na kama sio kodi zetu basi WORLD BANK au Mataifa makubwa wanatufadhili, achana na stori za watu wanazojaribu kutuaminisha maana kama sio moja kati ya hayo mawili basii watuambie Magufuli pesa anazitoa wapi???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom