Najua wajua ila nataka kukujuza zaidi na zaidi kuhusu CAF Interclub

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
3,188
8,215
MCHAKATO WA DRAW INAYOFUATA.

30 April 2021 ndio siku ambayo Draw ya CAF katika kupanga timu zitazocheza Robo Fainali na pia Nusu Fainali na kuingia katika mfumo wa mpaka Fainali katika Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho pia.

KANUNI ZINASEMA HIVI:
1. Vinara wa makundi hawawezi kukutana.

2. Timu zinazotoka Kundi 1 hawatakiwi kukutana.

3.Kinara wa kundi atacheza na mshindi wa pili wa kundi jingine anaepatikana kwenye draw.

4. Kinara wa Kundi anakuwa ni mwenyeji katika mchezo wa pili (2nd Leg).

6. Kutakuwa na mechi 4 za robo Fainali washindi wa mechi ya 2 na 4 ndio watakuwa wenyeji wa mchezo wa pili wa nusu Fainali.

7. Katika nusu Fainali Timu yeyote toka kundi lolote na Taifa/chama chochote ni huru kukutana.

NAFASI YA SIMBA IKOJE HAPA

1. Ni wazi ndio Kinara wa kundi A hivyo hawezi kucheza na vinara wenzie kama Mamelod Sundown, Wydad Casablanca na Esperance de Tunis wala Al Alhy ambae ni kutoka kundi moja nae kwenye robo Fainali.

2. Timu ambazo anaweza kukutana nazo Robo Fainal ambazo itategemea na matokeo ya mechi za mwisho wa makundi 09 April 2021 ni kati ya hizi hapa zifuatazo

KUNDI B - CB Belouizdad / Al Hilal
KUNDI C - Horoya / Kaizer Chiefs
KUNDI D - Zamalek / MC Alger

Katika timu zote 6 ni timu 3 tu ndio zinapita kwenda Robo Fainali kama Washindi wa pili na kati ya hizo 3 ni Timu mojawapo ndio itakutana na Simba kutengemeana na Draw itakavyokuwa.

TAREHE ZA MECHI ZIFUATAZO

1. ROBO FAINALI
1st. Leg 14-15 May 2021 - Away
2nd. Leg 21-22 May 2021 - Mkapa

2. NUSU FAINALI
1st. Leg 18-19 June 2021
2nd. Leg 25-26 June 2021

DOKEZO:
Katika nafasi 12 za uwakilishi wa timu 4 Point tulizopata mpaka sasa 27.5 zinaifanya Tanzania inagombania nafasi ya 10-11, na Iwapo Simba ikiweza kufika Nusu Fainal ni point 32.5 itawezesha msimu ujayo wa timu nne 2021/2022 kuanza na Point 24.5 ambazo zinatuweka sehemu nzuri ya kushiriki tena msimu ule 2022/2023 mwingine unaofuata, Tanzania itakuwa ipo nafasi ya 8-10 na kufanya kazi iwe rahisi iwapo timu zinaweza kuingia tu Group Stage 2021/2022 Biashara itakuwa mapema sana timu nne mfululizo.

KUPANGA NI KUCHAGUA
1617642606483.jpg


H.MBAGA
 
Umejitahidi kufafanua vizuri. Hata hivyo naomba nikukosoe kuhusu hao 'vinara wenzie' na Simba ambao umedai kuwa 'ni wazi hawawezi kukutana na Simba'. Ukweli ni kwamba hao Mamelodi Sundowns, Esperance de Tunis na Wydad Casablanca wamekwishajihakikishia kucheza robo fainali, lakini sio kweli kwamba wote hao wamekwishajihakikishia kushika nafasi ya kwanza kiasi kwamba hawawezi kukutana na Simba.

Katika hao vinara watatu, ni Mamelodi Sundowns tu aliyekwishajihakikishia kushika nafasi ya kwanza na hivyo hawezi kukutana na Simba, lakini Esperance de Tunis na Wydad Casablanca wanaweza kushika nafasi ya pili baada ya mechi ya mwisho, na hivyo wanaweza wakakutana na Simba katika robo fainali. Msimamo wa kundi C na D upo hivi hadi sasa kukiwa kumesalia mechi moja:

1617657321892.png

NB: Kuwa kinara kabla ligi haijaisha si lazima kupelekee kumaliza namba moja juu ya msimamo. Hata Yanga ni kinara wa ligi ya Bara kwa sasa, lakini wote mnajua kitakachoendelea
 
Umejitahidi kufafanua vizuri. Hata hivyo naomba nikukosoe kuhusu hao 'vinara wenzie' na Simba ambao umedai kuwa 'ni wazi hawawezi kukutana na Simba'. Ukweli ni kwamba hao Mamelodi Sundowns...
Umenena vyema mkuu, chochote kinaweza kutokea Kwa hayo magroup tajwa kuhusu kiongozi wa group

Ila Nimepanda zaidi hapo kwenye NB na ujumbe wake
 
yote kwa yote mechi kati ya simba na al ahly ndio itatoa picha halisi ya nguvu ya simba kwenye michuano hii..
Picha halisi imeshaisha, Simba ataendelea kuwa juu ya msimamo wa kundi akifuatiwa na Ahly, imeshaisha hiyo, tunaenda kukamilisha ratiba tu
 
yote kwa yote mechi kati ya simba na al ahly ndio itatoa picha halisi ya nguvu ya simba kwenye michuano hii..
Duu mkuu bado t mnawaswas na Simba kila siku mnalengine.

Simba ndo best kwenye kundi lake sababu ndo aloongoza kundi.

Na Kazifunga Tim zote kwenye kundi lake
 
Back
Top Bottom