Najua, tunao wasomi wengi sana, lakini ukweli ni kwamba idadi yao ni ndogo

Dogo Lao

Member
Nov 2, 2011
94
38
Ndugu wana Jf, Asalamu aleykum, Tumsifu Yesu Kristo, Bwana Yesu asifiwe.
Baada ya salaam, nianze kwa kusema "ashikhum siyo matusi". Najua, tunao wasomi wengi sana, lakini ukweli ni kwamba idadi yao ni ndogo sana ukilinganisha na vilaza waliojaa.

Mbaya zaidi, vilaza hao ndio waliopewa dhamana ya kutuamulia maisha yetu ya baadaye. Na kwakuwa tupo katika mfumo wa wengi wape, basi kwa wingi wao wamekuwa ni washindi ktk kila jambo pale kura itakapopigwa. Hawa ndio wenye kuamua tuelekee wapi, hawa ndio wenye kuamua vipaombele vyetu, hawa ndio wa kuamua mustakabali wa maisha ya watoto wetu kwa miaka kadhaa ijayo.

Pamoja na umbumbumbu wao, ndio hawa utawakuta wakishikilia nafasi nyeti kabisa za uongozi, ndio hawa ambao wanategemewa kutunga sheria, kuandaa sera, kupitisha mipango ya mapato na matumizi, ndio hawa tunawategemea watuletee maendeleo endelevu.

Wasifu wao, maisha yao na uhalisia wao ni 'kukalili' yaliyosemwa na mtu mmoja wanayeamini kuwa ana akili zaidi yao. Utawajua tu kwa matendo yao, hawawezi kufikiri tofauti na yule wanayemwamini kuwa ndio genius, hawana mtazamo mbadala, wao kazi yao ni kuchekelea na kushabikia tu kile kinachosemwa na genius.

Daima huwa macho yao yamefumbwa na akili zao zimelala kiasi kwamba wapo tayari hata kuzikana jinsia zao ilimradi tu Genius kasema, na wanaamini na kusadiki.
Hawa ndio tumewapa dhamana ya uwakilishi/usimamizi wa rasilimali/utetezi wa maslahi ya wengi.

Kwa aina hii ya watu, wenye akili ndio wanaoumia. Ni bahati mbaya sana maumivu yao hayawezi kuonekana machoni pa vilaza, wala juhudi zao za kuikomboa jamii nzima haitatafsiriwa kama ni hatua muhimu ya maendeleo endelevu. Badala yake juhudi hizo zitavikwa kila aina ya uovu na uonevu, huku zikitafsiriwa kama uhujumu, uchochezi, usaliti na yote yafananayo na hayo.

Kundi hili la vilaza ni kubwa sana, hata JF wapo, na utawajua tu kwa comments zao, hata posts zao, maana huwa ni vigumu sana kuficha ujinga uliostawi kichwani mwa mtu.

Wazo mbadala kwao ni upinzani, na upinzani kwao ni uvunjifu wa amani. Hizo ndizo tafsiri zilizojaa ktk vichwa vyao. Hakika, bado tuna safari ndefu ya kujikomboa. Kujikomboa ninakosema mimi ni ule ukombozi wa fikra, ili hatimaye tafsiri sahihi zianze kufanya kazi sahihi kwa ajili ya matokeo sahihi.
Asanteni.
 
Hii Mbaya sana kuna watu walipata madaraka wakasahau kutumikia Wananchi

Ila tunamshukuru Mungu kwa kumleta Magufuli kwa wakati sahihi

Tanzania inapaa sasa
 
ni kweli ka unavosema,
ila ndio dunia ilivyo, wale waliokua wanaongoza sana mashuleni vyuo nk, huishia either kuwa walimu au lectures, walioishia la saba au form 4 ndio wanakua mapolisi huko na ndio hao wanakuja kukuhenyesha hata ww mwenye degree tano, na sisi ma middle men ndo tunajenga uchumi kwa biashara , mamido class wengine ndo wanaingia serikalini na kukutungia sheria ww mwenye akili zaidi yake, na kuna wengine ni vilaza pure waliopenya hadi wakaingia serikalini na wanahenyesha watu wenye akili zao, maisha hayana formula mzee
 
Hatima ya maisha yako yapo mikononi mwako na kwa aliyekuumba..Hakuna binaadamu anayemiliki hatima ya binaadamu mwingine. World is not a bed of roses..Ukitaka furaha,Amani,au uhuru hivi vitu huwezi kupewa. Huwa vinachukuliwa
 
Mwanafalsafa wa Ugiriki ya kale Socrates alisema, werevu ambao hawataki kushiriki kwenye siasa wamejihukumu wenyewe kutawaliwa na watu wasio na uwezo kama wao.

Kama watawala wetu ni vilaza, na kuna wengi wenye uwezo zaidi, hilo ni kosa la wenye uwezo zaidi pia. Wenye uwezo walitakiwa kuweza kuwatoa hao vilaza.

Natambua ugumu wa mtu mwenye roho safi kupanda katika mfumo wetu wa kisiasa. Kote, upinzani na chama tawala.

Ni kama vile ili mtu kupanda ngazi kisiasa inambidi awe na hila mbaya, atoe na kupokea rushwa, ajue na kurumia hadaa, ns kadhalika.

Natambua watu wengi wenye uwezo hawataki kujitosa katika uchafu huu unaoitwa siasa.

Lakini, kutojitosa kwao ndiko kunawapa nafasi hao wengine wasio na uwezo.
 
Chama ambacho kwa kadiri ya utafiti, CCM ndiko walikojazana wajinga. Na hao ndio walioshika dola. Inawatumia watu kutoka kundi lake la wajinga kututawala.

Ni fedheha chama chenye wajinga wengi kuongoza nchi maana ni dhahiri kwenye uongozi mtakuwa na viongozi wengi walio wajinga.
 
Sijapata kuelewa muktadha wa mtu mwerevu yu katika eneo gani hasa , kwamba ukiwa na imani fulani basi wewe uelewa wako unakuwa zero?

Kwa mtu mwenye uelewa kama unaousemea unashindwaje kujua kwamba kuna kitu kinaitwa imani? Je wajua mtu anapoamini ktk kitu? Wapata wapi ujasiri wa kujidhalilisha JF ?

Huwezi lazimisha mtu awe ktk kile ww unachokiona kipo sahihi kufanya hivyo tunasema wewe ni "POPOMA"

Usipende kuonekana wa maana kwa watu ,acha wao waseme, wakuonyeshe kwamba unafaa na siyo kusema basi mie ndo nafaa kuliko wengine , ndio maana maisha yako hivi yalivyo!

Mwisho uko hivyo ulivyo kulingana na kiwango chako cha kufikiri asante!
 
Tufikie mahara uongozi wa mihimili yetu hasa bunge pawepo na viwango vya elimu na hasa wabunge wetu wawe na kiwango fulani cha elimu sio anayejuwa kusoma na kuandika eti ndie awe mbunge anayekwenda bungeni kutunga sheria.Ukiangalia mabunge ya Uganda ,Kenya wana viwango.Sisi tumebakia na katiba ya zamani ya kujuwa kusoma na kuandika.Sampuli ya wabunge wa aina hii zaidi ni kusema naunga mkono asilimia kwa mia ,NDIOO uwezo wao wa uchambuzi wa mambo mbali mbali ya taifa unakuwa mdogo.
 
Na kwa ukweli hakuna msomi wa ukweli aliye au anayeweza kumwambia yule asiye na elimu kama yake kwamba ni kilaza Live!

Ila wengi wenye kauli kinzani na chafu kwa wenzake ni watu wenye roho za kifisi fisi!

Tamaa binafsi na wezi.

Hivyo wale mnaoona watu wakiwapinga humu pia mnapaswa kuheshimu mawazo yao.
Sio kila mtanzania anakubaliana na hayo mambo yenu ya julichafua taifa.

Shame on you!
 
ni kweli ka unavosema,
ila ndio dunia ilivyo, wale waliokua wanaongoza sana mashuleni vyuo nk, huishia either kuwa walimu au lectures, walioishia la saba au form 4 ndio wanakua mapolisi huko na ndio hao wanakuja kukuhenyesha hata ww mwenye degree tano, na sisi ma middle men ndo tunajenga uchumi kwa biashara , mamido class wengine ndo wanaingia serikalini na kukutungia sheria ww mwenye akili zaidi yake, na kuna wengine ni vilaza pure waliopenya hadi wakaingia serikalini na wanahenyesha watu wenye akili zao, maisha hayana formula mzee
Mleta mada aisee...kwanini unanigusa
 
Huu ni upuuzi mtupu.Watunga sera ni ninyi wasomi,watoa maamuzi ni ninyi wasomi,Watunga sheria ni ninyi wasomi,wanaosimamia demokrasia ni ninyi hao hao wasomi,wanaosimamia haki ni ninyi wasomi,kila kitu ni ninyi wasomi,leo kwa nini uanzishe uzi wa kulaani wale unaoita vilaza wengi wao wakiwa baba zako,wajomba zako na shangazi zako kama si mama zako?Hao waliojinyima ili wewe usome?

Au unataka kutuambia hao unaowaita vilaza,ndio wanaotunga Sera na kuandika sheria kandamizi?

Nasikitika sana kwa vile wengi wenu mnaojiita wasomi mmeaminishwa kwamba ili mtu awe na mafanikio katika nyanja yoyote lazima awe na karatasi leandikwa "degree! " Na kwa vile ninyi ndio mmetunga na sheria kujipa nyadhifa zote za kimamlaka,mmekuwa mkitumia nguvu kubwa sana kukandamiza na kuweka mifumo ya hawa wengi kuwatumikia ninyi huku mkikosa shukrani.

Mambo yanapoharibika anayetukanwa ni mnyonge aliyenyimwa elimu tena kwa tusi lililoidhinishwa rasmi na watukufu,wakati ukweli uko wazi kuwa ninyi ndio mnasumbua nchi hii kama kansa.

Nitamtuma mjukuu wangu awe rais,akate. Kansa hii kabla haijaleta mauti.Nitalazimisha jambo ambalo dunia haijawahi kufikiri. Nitafuta mfumo huu wa elimu ya kipu.mbavu inayompa mtu kiburi cha kutukana kuliko kutatua changamoto zilizopo.

Hawa mnaowaamini wahadhiri wenu leo watabaki wavhache sana.Sitataka kukaribisha ujinga urithishwe kwa vizazi vyetu kwa jina la profesa.

Nina mengi ya kusema ila nahisi ni kama muziki ninaojaribu kuwapigia "Mbuzi" wanaoamini wao kuwa viumbe wa daraja la kwanza kwa sababu wameambiwa hivyo shuleni,na vitabu vyao vinathibitisha hivyo,hata kama hakuna uhalisia katika maisha ya kawaida.
 
ni kweli ka unavosema,
ila ndio dunia ilivyo, wale waliokua wanaongoza sana mashuleni vyuo nk, huishia either kuwa walimu au lectures, walioishia la saba au form 4 ndio wanakua mapolisi huko na ndio hao wanakuja kukuhenyesha hata ww mwenye degree tano, na sisi ma middle men ndo tunajenga uchumi kwa biashara , mamido class wengine ndo wanaingia serikalini na kukutungia sheria ww mwenye akili zaidi yake, na kuna wengine ni vilaza pure waliopenya hadi wakaingia serikalini na wanahenyesha watu wenye akili zao, maisha hayana formula mzee
Hivi ninyi mnaowakejeli watu kwa elimu zenu mkipata nafasi ya kutawala si mtatutemea mate usoni?
 
Mkuu wapi nimekejeli mtu? mimi hapa nimesema ni middle class/bourgeoisie , mimi mfanyabiashara tu, elimu hata sina sana zaidi ya kidegree cha hapo jalalani ambayo sijaitumia popote, sijakejeli mtu na siwezi
Hivi ninyi mnaowakejeli watu kwa elimu zenu mkipata nafasi ya kutawala si mtatutemea mate usoni?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom