Najua baadhi inawauma lakini huyu ataendelea kuwepo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Najua baadhi inawauma lakini huyu ataendelea kuwepo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jembejipya, Sep 23, 2010.

 1. J

  Jembejipya Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JAKAYA MRISHO KIKWETE
  1.Mtanzania pekee aliyewafanya wapinzani uchwara walie kuomba uongozi.
  2.Mtu pekee ambaye mafanikio yake kimaendeleo yanapingwa kwa porojo.(bila takwimu)
  3.Mtu pekee katika Tanzania ya leo aliyekubali kuacha sheria iwashughulike wanadhirifu wa mali za umma.
  4.Rais wa Tanzania 2005 - 2015.
  5.Aliyegeuza ilani ya CCM na mafanikio yake kuwa kama moto ambao kila mpinzani anaogopa kuukaribia.
   
 2. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Of course, as long as vipofu kama wewe wenye kutafsiri ufisadi kuwa ni mafanikio mkiendelea kuwepo kwanini mlezi wa mafisadi asiwepo?

  Halafu upofu wa aina hii sio wa bahati mbaya bali wa kuitakia,aidha kutokana na njaa, kujikomba au ubabaishaji tu. Hivi ni kwa ujira gani unaweza kuwasaliti ndugu zako kule kijijini wanaoishi katika hali mbaya zaidi ya ilivyokuwa zama za ukoloni?

  Kweli njaa yako ni muhimu zaidi ya rafiki zako wanaobambikiziwa kesi na polisi kwa vile tu hawana uwezo wa kuhonga wanausalama hao?Unawaambia nini akinamama wanaoahidiwa bajaji na Kikwete ilhali yeye na vigogo wenzie wanatanua kwa mashangingi ya mamilioni ya shilingi?

  Ni dhahiri umejiunga leo na JF sio kwa vile ulikuwa huifahamu au huipendi bali ni hayo maagizo kutoka kwa Usalama wa Mafisadi.

  Just be careful, usitukane mamba kabla hujavuka mto.
   
 3. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  Hapa kama unampigia mbuzi gitaa!! wanachadema watakaaa kwasababu ya ma highway wanayoyaona kule walipo!! basi wanadhani slaa na yeye atayaleta!

  ... asante kwa ujumbe!! wameusoma huo
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Tumgeukie huyo Kikwete wako

  JAKAYA MRISHO KIKWETE

  1.Mtanzania pekee aliyewafanya wapinzani uchwara walie kuomba uongozi.

  Kama unaongelea wapinzani uchwara, basi wewe una uongozi uchwara.Tafadhali tuambie kafanya nini kwa wapinzani ukweli, na sio wapinzani uchwara. You do not judge a leader's ability by how he works with his easiest challenges, but how does he work with his hardest ones.

  2.Mtu pekee ambaye mafanikio yake kimaendeleo yanapingwa kwa porojo.(bila takwimu)

  Mafanikio gani ? Takwimu zina tabia ya kuweza kudanganya vizuri tu.Ninaweza kuwaita watu wa Kikwete 100 na kuwauliza maswali ambayo yako favorable kwa Kikwete, wakatoa majibu ya kumpendelea Kikwete na kutoa headline kwamba katika survey fulani Kikwete amekubalika 100%. Mafanikio ya Kikwete zaidi ya mafanikio yakutegemewa kwa wastani wa kawaida yako wapi? Hizo shule zisizo na walimu wala majengo ? Hizo ahadi zisizotimilika ? Hebu tupe hayo mafanikio ya Kikwete tuweze kuyajadili. Inaonekana katika kuwashutumu watu kumpinga Kikwete bila takwimu, wewe ndiye unasema Kikwete ana mafanikio bila takwimu.

  3.Mtu pekee katika Tanzania ya leo aliyekubali kuacha sheria iwashughulike wanadhirifu wa mali za umma.

  Kikwete majuzi kawapigia kampeni Mramba na Lowassa, watu ambao uchafu wao unajulikana na umeelezwa vya kutosha.Kasema Lowassa hakufanya makosa anachafuliwa tu. Kwa kuwapigia kampeni na kutoa kauli kama hizo kuhusu watu hawa, wengine ambao kesi zao bado ziko mahakamani, Kikwete kashaingilia uhuru wa mahakama . Unawezaje kusema kwamba Kikwete kaachia mahakama imshughulike mtu kama Mramba ? Hivi Kikwete kama ana interest ya kumuona Mramba anashinda ubunge ili CCM ichukue kiti, kweli Kikwete anaweza kuwa serious kwa vita dhidi ya rushwa? Kama alikuwa serious kwa nini alimfanmyia kampeni Mramba ambaye kesi yake iko mahakamani na Lowassa ambaye kajiuzulu katika wingu la rushwa ?

  4.Rais wa Tanzania 2005 - 2015.

  We have lowered the bar so low now to the extent that almost anybody can be president, and this presidential clout business, to seriously thinking people at least, will not be a distinction by itself. What did he do as president ? Watanzania tuna tatizo la kutoa ofisi ambazo mtu kazishika kama distinction. Ofisi ambazo mtu kazishika si distinction. Ukitaka kutuonyesha distinction tuonyeshe huyo mtu kafanya nini katika ofisi hizo.

  5. Aliyegeuza ilani ya CCM na mafanikio yake kuwa kama moto ambao kila mpinzani anaogopa kuukaribia.

  CCM haina hata itikadi, much less ilani. Ilani gani ? Mafanikio gani ? Sio wewe uliyelaumu watu kumpinga Kikwete bila takwimu, sasa mbona unataka kumtetea bila takwimu na kuvunja sheria yako mwenyewe ?
   
 5. M

  Mutu JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Rejea mchanngo wa KIRANGA kasema vyema
   
 6. DaMie

  DaMie JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 24, 2010
  Messages: 686
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kiranga nimekukubali
   
 7. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #7
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kumbe anaekurupukaga CCM sio Mwalimu wa UPE peke yake. Wako wengi.
   
 8. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  JAKAYA MRISHO KIKWETE a.k.a Msanii,alipokuwa Ludewa ndo katia fora katoka na staili ya kupokea simu kabla ya kupanda jukwaani halafu anawambia wananchi alikuwa anazungumza na balozi wa Marekani, eti Obama kaahidi kuendelea kutoa misaada..tehtehteh ....kumbe alikuwa anaongea peke yake,jamaa msanii yule.. ehe....
   
 9. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Tuache ushabiki "maandazi" maendeleo ni pamoja na kubadili uongozi..
  Kula TANO Mkuu Kiranga...
   
 10. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama aliyofanya yanakubalika kwa nini anahangaika kiasi hicho kubandikwa kila kona ya nchi kama vile ni mgeni kwa wananchi. hadi kinana anasema inabidi siku za mapumziko zipunguzwe na kufanya kampeni nyingi zaidi kwa maana hali ni mbaya? CHEMA CHAJIUZA KIBOVU CHAJITEMBEZA. kama anakubalika mbona hata mikutano haina watu inabidi muwzombe kwa malori kutoka sehemu moja hadi nyingine?

  Hivi bado hujakubali kua JK amedorora tofauti na ilivyokua 2005. kwa taarifa yako watanzania 2010 Hawadanganyiki!
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe Wageni wapya wanakuja na moto lakini Moto wao huwa wa kuni tu haukawi kuisha mwache aje na kasi yake kwa kuwa anaonyesha ni CCM Damu unakaribishwa lakini usilete Matusi hapa. njoo na heshima yako Mkuu Jembejipya. Tunataka utupe ushahidi wako sio kuleta upinzani waTimu ya Simba na Yanga asante karibu tena.
   
 12. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Msemo wa Iza kwamba tuache ushabiki "MAANDAZI"
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Timkalibishe atoe maoni yake na atoe Evidence tatizo ni kwamba hawa wageni hawajui kuwa unapoingia humu njoo na evidence kuhakiki unachokisema hii si kwajili ya Chadema au ccm ni yawatanzania. Toa evidence tumpe kura jk bwana Jembe jipya.
   
 14. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Wewe kweli Jembejipya. Hata kunolewa halijanolewa. Post yako ya kwanza hata mashiko haina!!!! Kwani hizo ni sifa?

  Toa mifano ya mafanikio siyo pambo za jumla jumla.
   
 15. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kwanza bisha hodi. Halafu karibu. Naamini hapa tongotongo litakutoka tu.

  Tutakuelimisha hata kama uliishia la saba, hata kama ni M-CCM ambaye husikii wala huambiliki. Hata kama umetumwa kubandika vipost uchwara hapa.

  Mwisho wa siku RAIS WAKO NI DOCTOR SLAA.
   
 16. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Evidence kwa kipi kilichozungumziwa. Absent mind! lol
   
 17. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  '

  Ila huyu jamaa akiamua kushuka, huwa anashuka kweli, namkubali sana.

  Akipunguza ugomvi, na watu wakaacha kukaa wanamchokonoa chokonoa, JF ina hazina kubwa sana hapa. Principal ya kwenda vizuri na Kiranga, hata kama umegombana naye, msikilize vizuri hoja zake, na umjibu kwa hoja,..., basi!
   
 18. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Rais pekee aliyekimbia mdahalo!.

  Kama kuna mambo ambayo jk kafanya ambayo ni yakujivunia. mwambie akubali mdahalo ili atupe hizo takwamu.
   
 19. ismase

  ismase Senior Member

  #19
  Sep 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ongeza na haya
  -Kiongozi pekee aliyeimarisha utawala bora unaozingatia utawala wa sheria
  -kiongozi pekee aliyeimarisha democrasia nchini
  -kiongozi pekee aliyewachukulia hatua mafisadi bila kuangalia vyeo vyao
  -kiongozi pekee aliyekubali kupitisha sheria ya gharama za uchaguzi
  -kiongozi pekee aliyeboresha elimu chini (kafuta ada za mitihani, kajenga shule lukukii)
  -kiongozii pekee aliyejenga chuo kikuu cha kimataifa cha Udom
  -kiongozi pekee aliyeboresha soka nchini kwa kumleta kocha mbrazili (na kufuta usemi wa kichwa cha mwendawazimu)
  -kiongozi pekee aliyekuja na kauli mbio kilimo kwanza
  -kiongozi pekee anayechukia ufisadi
  -kiongozi pekee aliyezuia viongozi kununua magari ya kifahari (mashangingi)
  -kiongozi pekee anayeanguka majukwaani kwa dhiki kwa ajili ya wananchi wake

  NB: Mambo ni mengi ALIYEFANYA BABA HUYU, KWA REJEA SOMA ILANI YA UCHAGUZI CCM
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Yeah..ameyafanya hayo yote ktk DUNIA YA KUSADIKIKA au usingizini..walah mbavu zangu wajameni
   
Loading...