Najma Abdalah wa RFA unajua tofauti ya IMF na IFM kweli?

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,945
728
Leo katika kipindi cha yasemavyo magazeti kinachorushwa na Radio Free Africa mtangazaji Najma Abdallah aliisoma habari inayosema "IFM waionya Tanzania" nijuavyo mimi IFM ni Chuo cha usimamizi wa fedha nikasubiri asome kwa undani lakini akaendelea kutaja kuwa IFM ni shirika la fedha duniani zaidi ya mara tatu .

Nijuavyo mimi neno sahihi ni IMF na sio IFM hivyo Dada Najma kama msomi hukutakiwa kurudia makosa haya hata kama mwandishi alikuwa amekosea maadishi.

Ni makosa madogo lakini yanaleta ukakasi katika taaluma yenu.
Kazi njema.
 
Je, gazeti lenyewe limeandika IMF au IFM?

vyovyote iwavyo....ila wanatakiwa wajiongeze kielimu.......hata kama mwenzie kakosea....ndio na yeye acopy makosa.....?..
RFA kidogo hawapo vizuri.......mara nyingi hata kwenye jografia....huwa wananiangusha sana........
 
IFM na IMF kiukweli vinachanganya.Na wewe msikilizaji jiongeze sio kila kitu uje kushitaki humu JF
 
Kama mtu hafahamu kwamba IFM ni Chuo Cha Usimamizi wa Fedha ni lazima achanganye kati ya IFM na IMF!!.

Ndugu acha umbea, fanya Kazi!
 
vyovyote iwavyo....ila wanatakiwa wajiongeze kielimu.......hata kama mwenzie kakosea....ndio na yeye acopy makosa.....?..
RFA kidogo hawapo vizuri.......mara nyingi hata kwenye jografia....huwa wananiangusha sana........
Kujiongeza ni sawa na ni vizuri lakini inategemea na ufahamu wa msomaji husika katika mambo mbalimbali kama hayo mashirika ya UN hususani IMF na IFM, na hata mambo ya jiografia kama ulivyosema.
Kwa wanahabari wetu hawa wa D 4 tena za O-Level ni jambo la kawaida kutokuwa na wide general knowledge zaidi ya kusoma tu kama msomaji wa somo kanisani. They only read whatever on the paper or ppt regardless is correct or not.
Hapa ndo umuhim wa masomo mengi O-Level, na kutojikita kwenye masomo fulani tu (art or science or business studies) unapoonekana. Vile vile ufuatiliaji wa mambo mbalimbali kupitia kusoma vitabu na majarida, na kusikiliza news.
 
Back
Top Bottom