Najivunia kuwa mwanachama wa CHADEMA.

oldonyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
549
86
Ndugu zangu wanajamvi kama katiba yetu inavosema kila mtanzania ana haki ya kuwa na dini yake, kujiunga na chama anachopenda na uhuru wa kuishi mahali popote, leo mimi najitokeza kuwambia najivunia kuwa mwanachama wa cdm kwasababu ni chama makini ni chama kinachoitakia Tanzania yetu mema kwa kupambana na ufisadi na licha ya ivo kina sera ambazo zinataka kumkomboa mtanzania kutoka ktk lindi la umasikini.

Pia wanajamvi kitu kinachonipa faraja na kunifanya nitembee kifua mbele ni kuona sera za chama hiki pamoja na ilani yake kuchukuliwa na magamba kama mtaji wake wa kisiasa mfano ufisadi. Si ivo tu kuna kamanda mmoja anaitwa freman Aikael Mbowe aka kamanda wa anga huyu jamaa ktk kampeni zake za kuusaka uraisi mwaka 2005 aliweza kuonyesha ubunifu wake kwa kutumia helikopta kupigia kampeni.

Kama tujuavyo magamba walimkejeri kwa kusema mara anafadhiliwa na wamarekani mara ni matumizi mabaya ya ruzuku lakini leo tumeshuhudi nao wamekodi helikopta tena mbili na CUF nao nasikia wanatumi huko Igunga hadi mara nyingine huwa nakaa na kujiuliza hivi chama tawala cha Tanzania ni kipi? Hivi wanajamvi sijutii kuwa mwanachama wa CHADEMA bali najivunia kuwa mwana CHADEMA.

Nawasilisha.
 
Ndugu zangu wanajamvi kama katiba yetu inavosema kila mtanzania ana haki ya kuwa na dini yake,kujiunga na chama anachopenda na uhuru wa kuishi mahali popote,leo mimi najitokeza kuwambia najivunia kuwa mwanachama wa cdm kwasababu ni chama makini ni chama kinachoitakia tanzania yetu mema kwa kupambana na ufisadi na licha ya ivo kina sera ambazo zinataka kumkomboa mtanzania kutoka ktk lindi la umasikini.Pia wanajamvi kitu kinachonipa faraja na kunifanya nitembe kifua mbele ni kuona sera za chama hiki pamoja na ilani yake kuchukuliwa na magamba kama mtaji wake wa kisiasa mfano ufisadi.Si ivo tu kuna kamanda mmoja anaitwa freman aikael mbowe aka kamanda wa anga huyu jamaa ktk kampeni zake za kuusaka uraisi mwaka 2005 aliweza kuonyesha ubunifu wake kwa kutumia helikopta kupigia kampeni,kama tujuavyo magamba walimkejeri kwa kusema mara anafadhiliwa na wamarekani mara ni matumizi mabaya ya ruzuku lakini leo tumeshuhudi nao wamekodi helikopta tena mbili na Cuf nao nasikia wanatumi uko igunga hadi maranyingine huwa nakaa na kujiuliza hivi chama tawala cha tanzania ni kipi?ivi wanajamvi sijutii kuwa mwanachama wa cdm bali najivunia kuwa mwa cdm.nawasilisha.

Utoto huo.
 
Duu haya bana, maana kila mtu akianzisha uzi wa 'kujivunia' sijui itakuwaje......hebu fikiria najivunia kuwa CDM,najivunia kuwa CCM,najivunia kuwa TLP, najivunia kuwa CUF,NCCR...........
najivunia, najivunia.......
Tujipambanue zaidi kwa kuchambua hoja na sera za msingi.......
 
Ndugu zangu wanajamvi kama katiba yetu inavosema kila mtanzania ana haki ya kuwa na dini yake,kujiunga na chama anachopenda na uhuru wa kuishi mahali popote,leo mimi najitokeza kuwambia najivunia kuwa mwanachama wa cdm kwasababu ni chama makini ni chama kinachoitakia tanzania yetu mema kwa kupambana na ufisadi na licha ya ivo kina sera ambazo zinataka kumkomboa mtanzania kutoka ktk lindi la umasikini.Pia wanajamvi kitu kinachonipa faraja na kunifanya nitembe kifua mbele ni kuona sera za chama hiki pamoja na ilani yake kuchukuliwa na magamba kama mtaji wake wa kisiasa mfano ufisadi.Si ivo tu kuna kamanda mmoja anaitwa freman aikael mbowe aka kamanda wa anga huyu jamaa ktk kampeni zake za kuusaka uraisi mwaka 2005 aliweza kuonyesha ubunifu wake kwa kutumia helikopta kupigia kampeni,kama tujuavyo magamba walimkejeri kwa kusema mara anafadhiliwa na wamarekani mara ni matumizi mabaya ya ruzuku lakini leo tumeshuhudi nao wamekodi helikopta tena mbili na Cuf nao nasikia wanatumi uko igunga hadi maranyingine huwa nakaa na kujiuliza hivi chama tawala cha tanzania ni kipi?ivi wanajamvi sijutii kuwa mwanachama wa cdm bali najivunia kuwa mwa cdm.nawasilisha.

Serikali ya maisha yako ni kichwa chako sio CDM.
Tafakari!
 
Utoto huo.
Inawezekana ukubwa ni kujivunia uana CCM. Tatizo la mijitu mingine haitaki kuwa serious wakati wa Kuchangia thread, haiwezekani Great thinker uishie kusema "huo ni utoto" bila kufafanua. Je ni utoto mtu kujieleza yeye ni mwanachama wa chama gani? au utoto wake ni kuandika thread yake bila kuwa na paraghraph? je utoto wake umeugunduaje, unapo coment hakikisha coment yako inakuwa user friendly
 
Weka namba ya kadi yako au wewe ulikuwa chadema kwa jina?

Hata ukiondoka utakwenda wapi na kujitangaza?
 
Weka namba ya kadi yako au wewe ulikuwa chadema kwa jina?

Hata ukiondoka utakwenda wapi na kujitangaza?

mkuu siamini kama hiyo thread umeisoma au ulikuwa unasoma tofauti na hii au unamanisha nini?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom