Najiuliza nilikosea kumuoa wife au ni tamaa au labda shetani?

BABU KIDUDE

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,545
2,000
Ndugu zangu, Wife bana kajifungua kama mwezi hivi, tunashukuru sana kwa Mungu mtoto wa 2 sasa. Safari hii tofauti na mwanzo kajifungulia hapa hapa na tukiwa tushaamia mjengoni nje ya jiji hukoo sijui.

Kama ilivyo kawaida japo tuna Dada wa kazi lazima tupate mtu wakukaa na Mzazi hapo ndo napata tabu kidogo. Mke wangu kwao wamezaliwa watano, Mwanaume mmoja na Wanawake ni wanne, yeye ni wapili kwa kuzaliwa wa kwanza ni Kaka kisha waliobaki ni wadogo zake wakike na wote wameolewa.

Picha linaanza…..

Siku mbili baada ya wife kujifungua alikuja Mdogo wake anayemfuata kaolewa Tanga huko, alikaa kama wiki 2 hivi kisha akaondoka kurudi kwake. Baada ya kuondoka akaja wa mwisho kwa kuzaliwa naye kaolewa Morogoro akakaa kama siku 10 kisha kaondoka. Juzi kaja wanne kuzaliwa kaolewa Moshi yupo mpaka sasa.

Kipindi cha kuja kwa mashemeji zangu hawa kimenifanya nijiulize nilikosea kumoa wife au ni tamaa au labda shetani? Shemeji zangu hawa wamekuwa wakinihudumia vizuri kuliko hata mke wangu kwa miaka yote 9 ya ndoa. Wamenionyesha Upendo, Mapenzi, mahaba heshima na kunijali haswaa wanne kuzaliwa . Nimejikuta najiona Mwanaume.

Uwepo wake unefanya niwe na bashasha muda wote nikiwa nyumbani she is so charming and humble. Huyu wanne kwa uzuri hamshindi mke wangu lakini Mashallah. Mama mkwe kazaa bana na ndio aliyefanana naye sana japo wote ni wazuri kwa kweli ukiacha Rangi ya Mtume waliyo copy toka kwa Baba yao.

Mimi ni mpenzi sana wa kupika ni hobi (Wife anachukuliga poa sana nikiingia jikoni ananifukuza) lakini meshemeji zangu wanajua hilo mara nyingi wamekuwa wanivuta jikoni saa nyingine najikuta nipo nao jikoni tunapika pamoja ilimradi tuwe Karibu.

Wote kwa nyakati tofauti wekemkuwa wanasifia kupitia dada wa kazi kwamba dada yao (Wife) kapata Mume Mwema sana, dada wa kazi ni wakutoka kwetu huko so ananipaga stori

Uwepo wao umenifanya niendelee kuvumilia kutomcheat wife wamenifanya mtu mwema. Ukiacha aliyopo hapa sasa nimekuwa kila mara nawapigia Mashemeji zangu waje niishi nao najisahau wana maisha yao, wanaume zao na wana watoto wao. Inafikia kipindi nawaonea wivu kwa waume zao hapo ndo shidah waungwana

Nampenda sana Wife wangu japo nishamcheat mara kadhaa, na pia sifikiri kabisa kumcheat kwa wadogo zake hawa au ndugu zangu hawa, lakini wamenionyesha Upendo, Mapenzi, mahaba heshima na Kunijali Sana bila hata kuwafanyia jambo kubwa la maana sana.

Sijawai kuwatamani kingono but kiukweli nimetokea sana kuwapenda kiasi cha kutaka kuishi nao wote kwa pamoja.

Haya mamboo yaache tuu
 

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
15,492
2,000
Ujinga mtupu.. kwan kuna baya gani ndugu wa Mkeo kukujali wewe zaidi ya anavyofanya dada yao??

Wanafanya ivo kuhakikisha kwamba hujihisi kupungukiwa chochote ktk kipindi iki ambacho dada yao mapenzi yote kaamishia kwa mtoto.

Shukuru umepata mashemeji wema.... kwan wameshawahi kukutega kimahaba ??? Au huduma unazopewa ndo zafanya ujishitukie?

Acha zako bana, nawao wanapenda sana Waume zao...

Acha kufikiria Ujinga .
 

Msweet

JF-Expert Member
Mar 26, 2014
1,952
2,000
Kaka..... tunaomba fafanua kidogo..... Hapo mashemeji walipokuhudumia vizuri, walipokuonyesha Upendo, Mapenzi, Mahaba, Heshima na Kukujali Haswaa yule wa NNE kuzaliwa ....... Mpaka ukajikuta unajiona Mwanaume tena 😅😅😅
 

toughlendon_1

JF-Expert Member
Feb 7, 2018
1,777
2,000
Gonga like if you know the story is still developing and the whole thing is pulling this man deep down that black hole, and he does not know. Its just the beginning ya'll its just the beginning...


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Castle_Lite

JF-Expert Member
Sep 10, 2016
543
1,000
Muheshimu Mkeo.

Wasingeweza kukuhudumia hivyo bila Mke wako kuwaambia/kuwaongopea/kuwaongezea Mazuri ya kwako.

Daima , wanayofanya mashemeji yanatoka moja kwa moja kwa jinsi maneno ambayo Mkeo kawaambia/huwa anawaambia kuhusu wewe.

Kwahiyo nadhan hujakosea kuoa ila umepatia.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom