Uchaguzi 2020 Najiuliza, ni Mwananchi wa aina/fani gani atampa kura Magufuli mwaka huu

Clark boots

JF-Expert Member
Jun 5, 2017
6,401
5,525
Yaani nipo hapa najiuliza sipati jibu ni mwananchi wa fani/aina gani atampa kura Magufuli mwaka huu.
Maana kama;-

WAFANYA BIASHARA.
Hawa wamenyanyaswa sana ndani ya miaka 5 hii iliyoisha, refer msoto wa Manji alioupitia toka Magufuli aingie madarakani na wafanya biashara wengine kedekede, mwenyewe ni mashahidi.

WAFANYAKAZI.
hapa nazungumzia waajiriwa serikalini sekta mbalimbali jinsi walivyovuka kwa shida hii miaka 5 pasi na nyongeza yoyote ya mshahara tena na vitisho au maneno ya kebehi kana kwamba kama umechoka kazi basi acha. Hapa kumbuka kuna wale waliofukuzwa kazi kuanzia ile 2016 (vyeti feki) sijawazungumzia ila naomba niishie hapa.

WAHITIMU WA ELIMU ZA JUU NA KATI.
Hawa ndo hatari tupu, naamini wahitimu walio wengi waliohitimu toka 2015 hawana kazi rasmi labda awe na connection ndo anaweza akaja hapa na kutuambia kuwa amepata permant job serikalini.

WAOMBAJI MIKOPO ELIMU YA JUU.
Hawa nao ni majanga tu mikopo ya elimu ya juu imekuuwa kama betting tu kama huna kismart basi kwisha habari yako.
Hao wanaendelea na masomo na walibett na kupata zali LA mkopo show wameiona mwaka huu kwa kupunguziwa mabomm yao eti kisa Corona.

WAKULIMA.
Huku nako ni chenga tu. Jaribu kwenda Lindi na Mtwara ukaone watu wanavyoteseka na zao la korosho na wengine walidirika mpaka kujinyonga..eti wanaambiwa korosho hawajalima wao wao ni Kangomba.

Heeeeee, hadi nimechoka kuandika jamani ongezeeni na mengine naamini ni mengi sana. Ndio maana najiuliza hapaa huyu Magufuli mwaka huu atapata kura ya mtanzania gani?
 
Nimeikuta sehemu nikaona si mbaya tuwaze wote.
Screenshot_20200902-150655.jpg


Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Kuna mataga mkuu!! Hawajali chochote zaidi ya buku 7 itapendeza.
Wewe huna sababu za kumyima Kura Magufuli! Labda hasira za kutimuliwa kazi Kwa zile cheti hewa zenu au kule kuvuna mahali usipopanda!

Utakuta mtu hata nyumba yake pesa yake iliyotumika kuijenga ilitosha tofali 10 pekee, zingine zote alikwapua au aligisadi, hapo si ni Sawa na mtu anaishi kwenye nyumba ya watu wengine?

Kama mlizoea Kwa Aina hiyo na hamuoni haya hata Mbele za Mungu, lazima utamchukia Magufuli

Tutampa tena Ili muendelee kuonja ubaya wa kuishi maisha ya kitapeli
 
HUYU KIUMBE HAFAI KUPEWA TENA NAFASI YA URAIS WA TANZANIA HATA BURE.....ARUDI KWAO AKAMUUGUZE MAMA YAKE MZAZI....KWANI NI LAZIMA AENDELEE KUWA RAIS? KAZI ZIPO NYINGI HATA UGANGA WA JADI UNAMFAA LAKINI SIO URAIS WA TANZANIA.
Kabisa kabisa
 
Magufuli atapigiwa kura na wale anaopenda kuwaita wanyonge.

Wanyonge = wananchi wasiojitambua.

Mimi nilishakataa kuwa mnyonge wa ccm tangu Magufuli akiwa waziri hivyo asitegemee kupata kura yangu.
Ushachaji Simu umelala kwa Amani na Sasa unatamba Na Simu ... Maisha Safi hata usipompigia kura MAGUFULI NI KAMA MAJI USIPOYANYWA utayaoga
 
Labda utupemwanga ni nani mwingine mbdala wa JPM ili na yeye tumuangalie tuone kama atatuwatanzania.
 
Wameanza onja joto ya uchaguzi,
Bila muziki watu hawaendi kuwasikiliza, majaliwa makosa watu Babati, samia imebidi alazimishe shule zifungwe ili apate wasikikilizaji,

Huku Lisu na zito wanazidi kupata uungwaji mkono
Hizi propaganda zilimponza lowassa 2015. Kama hao walikosa watu. Mtumeni hata Mbowe jimboni kwake Hai, tuone kama atapata hata fisi wa kumsikiliza.
 
Binafsi mm naona labda wamachinga ila kwa mfanyabiashara huez mpa kabisa. Magufuli katesa sana wafanyabishara kipindi chake,TRA imekuwa kama genge la walanguzi kwa sasa
Mmeshasahau wakati mnalalamika kwamba wafanyabishara wanakwepa kodi na ikulu ni kama sebule kwao. Leo wamebanwa mnarudi kuwatetea.
 
Back
Top Bottom