Najiuliza, kwanini marais wa Afrika hawakupewa nafasi ya kuhutubia kwenye kuaga mwili wa MANDELA?

Makaura

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
894
195
Wandugu, mbona sikumuona Rais wa kiafrika aliyehutubia jana kwa Madiba isipokua rais mwenyeji? Je, kuna sababu gani? Au ni ukoloni Maomboleo? Au uwezo mdogo?
 

gmosha48

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
2,401
2,000
Marais wetu waligubikwa na simanzi sana. Hawakuwa kwenye mood ya kuhutubia.
 

kiparah

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,174
0
Wote mnategemea misaada kutoka kwao, sasa watu wa protocal waliogopa wanaweza kujisahau na kuelezea shida zao.
 

scramble

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
1,593
0
Waliozungumza waliwakilisha mabara happy Brazil na Cuba wanatoka bara moja. Afrika iliwakilishwa na rais wa namibia. Vikevile AU iliwakilishwa na mama zuma. Ikumbukwe kuwa rais zuma nae aliiwakilisha afrika kusini na afrika kwa ujumla
 

kikule

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
217
225
ni afadhali marais wengine wa afrika hawakupata nafasi maana wangeanza kusema kuwa mandela alikuwa mtu wa kusamehe basi obama naye anatakiwa awasamehe magaidi
 

TsafuRD

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
1,908
2,000
Wandugu, mbona sikumuona Rais wa kiafrika aliyehutubia jana kwa Madiba isipokua rais mwenyeji? Je, kuna sababu gani? Au ni ukoloni Maomboleo? Au uwezo mdogo?
Rais wa NAMIBIA alihutubia baada ya Rais wa Brazil.
 

Du Bois ideas

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
428
0
Wandugu, mbona sikumuona Rais wa kiafrika aliyehutubia jana kwa Madiba isipokua rais mwenyeji? Je, kuna sababu gani? Au ni ukoloni Maomboleo? Au uwezo mdogo?

Badala ya hotuba ya kuomboleza wangeanza kunadi fulsa za uwekezaji kwa Mataifa yaliyokuwapo pale. Wengine wangesema sasa tuna gesi nyingi wengine mafuta nayo baharini na mwisho wangeomba pesa kwa Obama
. Watu wa protocal waliiona hiyo wakawapiga burn
 

Offline User

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
3,836
2,000
Nilisoma jana humu eti JK angeongoza marais wengine kwenye kuaga/mazishi ya Madiba? Vp wadau, ilikuaje tena maaana hata kamera za uwanjani hazikumnasa kabisa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom