Najiuliza kwanini Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imeamua kuzika miili ya watu 6

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Najiuliza kwanini Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imeamua kuzika miili ya watu 6 waliookotwa mto Ruvu bila uchunguzi kufanyika, huku wakijua kuwa kuna familia zipo kwenye taharuki ya kupoteza ndugu zao. Hata kama miili ilikua imeharibika sana ilipaswa kuchukuliwa sampuli kabla ya kuzikwa. Sioni kuwa hili ni kosa la bahati mbaya, unless wanasheria watuambie sheria zinasemaje kwenye hili. Lakini bado maswali ni mengi kuliko majibu.!

Malisa GJ
 
Kasomeni upya habari hiyo, waliozika ni wavuvi baada ya kuokoa miili hiyo na kutokana na kuwa imeharibika sana wakaamua kuizika.
 
The number 6.Unakumbuka 666?Labda ni maagizo ya mganga,unajuaje?
Najiuliza kwanini Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imeamua kuzika miili ya watu 6 waliookotwa mto Ruvu bila uchunguzi kufanyika, huku wakijua kuwa kuna familia zipo kwenye taharuki ya kupoteza ndugu zao. Hata kama miili ilikua imeharibika sana ilipaswa kuchukuliwa sampuli kabla ya kuzikwa. Sioni kuwa hili ni kosa la bahati mbaya, unless wanasheria watuambie sheria zinasemaje kwenye hili. Lakini bado maswali ni mengi kuliko majibu.!

Malisa GJ
 
Yes, ila badae walijulishwa.

Chachu Ombara;
Niseme tu, mimi sio mtaalam wa sheria ila, kijiji kilichopo karibu, kikundi kilichofanya jambo hilo, kijiandae kuja kuifukua miili hiyo yoote very very soon kabla ya wiki hii kuisha.
Sheria haisemi hivyo. Ati zika halafu ukaripoti polisi. Tutajuaje kama mliwaua kwanza ndo mkawaficha majini?? Tutajuaje ka ni wapinzani wenu hapo kijijini au informers mliwaua?? Post moterm hufanywa kwanza, ndipo maziko. Si/vinginevyo.
 
Mi mwenyew nashangaa imekuwaje wazike bila ruhusa ya vyombo Vya sheria?au wavuvi waliwaua???kwanini polis had mdaa huh haeajafukua hiyo miili kwaajili ya uchunguzi?kwanini waziri wa ulinzi yupo kimya???
 
Daktari pekee ndio mwenye uhalali wa kuthibitisha kifo cha mtu....hata kama ukikuta mtu hana kichwa, unapokuta maiti popote unatakiwa utoe taarifa polisi wenyewe watakuja kuchukua mwili na kuupeleka hosipitali ili kupata ripoti ya kifo ambapo daktari ataandika kuwa marehemu anaitwa nani na sababu za kifo ni zipi....kwa taarifa hata kama ndugu yako (unadhani amekufa) nasema unadhani kwa sababu mwenye uhalali wa kuthibitisha kifo ni daktari...Mkiwa mnaenda kuzika mkasimamishwa na polisi wakaulizia ripoti ya kifo nyinyi wote ni watuhumiwa wa mauaji.....hili la bagamoyo linatisha
 
Hiyo miili ifukuliwe ili uchunguzi kamili ufanyike. Hatuwezi kufanya mambo yanayozua maswali kienyeji namna hiyo!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom