Najiuliza kama Spika aliapa kuilinda na kuitetea Katiba, kwanini anaivunja?

Duh...!. Kuna kitu umekisema hapa kuhusu kuapa kwa jina la Mungu kuwa utailinda, kuitetea na kuitekeleza katiba ya JMT, hivyo kiapo ni maagano kati yako na Muumba wako, ukikiuka...!. Usikute hata naniliu amenaniliu kwa sababu ya kuinaniliu hii naniliu!.
Karma is real!.
P
Umeeleweka sana maana si mara ya kwanza unalisema hili la Karma.
 
Mkuu unawajua "wachumia tumbo" au unawasikia? Wenyewe kuapa viapo vya uongo au kumshirikisha Mungu kwenye uovu wao si sehemu ya maisha yao ya kawaida kwa maana hawana hofu ya Mungu wala hawaamini kama kuna kufa!!!
WADAU Nawasalimu. Hakika Kati ya Vitu ambavyo Hayati BABA wa TAIFA alivisimamia na Kuvisemea Muda wote na Kwa Nguvu zake zote ni KATIBA ya NCHI. Hayati BABA Wa TAIFA alikuwa Anasisitiza VIONGOZI wote WALIOAPA Kuitii, Kuiheshimu na Kuitetea KATIBA.

Katika UTAWALA wa AWAMU ya PILI kulikuwa na UVUNJIFU wa KATIBA lakini Hayati BABA Wa TAIFA Hakusita KUUKEMEA. Leo Wote Watanzania ni Mashahidi hakuna AWAMU iliyochezea KATIBA ya NCHI kama AWAMU ya TANO.

Tumeshuhudia SHERIA Katili na Kandamizi Zikitungwa na Zikipitishwa Kama za Kujiwekea KINGA kwa baadhi ya VIONGOZI wetu, Sheria za Vyombo vya Habari, Vyama vya Siasa, Tume ya Uchaguzi Dhamanan.k.

Isitoshe tumeshuhudia SPIKA wa BUNGE Kiongozi wa MHIMILI wa NCHI Anakiuka Kwa Makusudi KATIBA ya NCHI kwa Kuwatetea WABUNGE Waliofukuzwa na CHADEMA Licha ya kutokuwa na SIFA za kuwa WABUNGE. SPIKA Ndugai ALIAPA kuilinda na kuitetea KATIBA lakini leo ndio KINARA wa KUIVUNJA najiuliza kama SPIKA Aliapa Kuilinda na Kuitetea KATIBA kwanini ANAIVUNJA?

Je Yeye ni Nani mpaka Afanye hivyo na Hakuna wa Kumkemea? Wakati umefika kwa wenye MAMLAKA hasa RAIS WETU Kuhakikisha Anawakemea wale Wote Wanaoichezea na Kuivunja KATIBA ya NCHI na Kuwataka Waiheshimu KATIBA yetu kama Walivyoapa.

Tukumbuke Wakati wa KUAPA Tulimshirikisha MUNGU WETU. Hivyo MUNGU Asidhihakiwe.
 
Duh...!. Kuna kitu umekisema hapa kuhusu kuapa kwa jina la Mungu kuwa utailinda, kuitetea na kuitekeleza katiba ya JMT, hivyo kiapo ni maagano kati yako na Muumba wako, ukikiuka...!. Usikute hata naniliu amenaniliu kwa sababu ya kuinaniliu hii naniliu!.
Karma is real!.
P
Mkuu "Mwanakawe.." mbona unaogopa kumtaja huyo "naniliu" kwani wale "wasionaniliu" wangaliko baada ya "naniliu" kunaniliu?
 
Mkuu "Mwanakawe.." mbona unaogopa kumtaja huyo "naniliu" kwani wale "wasionaniliu" wangaliko baada ya "naniliu" kunaniliu?
No, ni kwasababu, hata kabla naniliu, hajananiliu, kulizuka minong'ono mingi kuhusu hali ya afya ya naniliu, na kwamba alikuwa hoi bin taaban, katika kujaribu kuokoa maisha yake, akakimbizwa kule naniliu, ikashindikana, ndio akananiliu akiwa kule, ikaonekana itakuwa ni aibu dunia ikijulishwa naniliu ali naniliu kule kwa ugonjwa wa naniliu, sasa kwa vile taifa lilishatangaziwa rasmi, alinaniliu tarehe fulani kwa ugonjwa wa naniliu, ukitoa sababu nyingine yoyote, au tarehe rasmi ya kunaniliu, utakuwa umemfanya naniliu naye, aonekane muongo, hivyo bora kuendelea kuamini kile tuu tulichotangaziwa rasmi.
P
 
Hajui maana ya KIAPO...anafiiri kuapa ni justification tu kumbe ni kitu muhimu na kibaya saana kama hutayatii hayo uliyouyaapa kwani yaweza kuwa chanzo cha laana / roho za kukataliwa etc ... na mbaya zaidi laana hurisishwa hadi vilembwe (kizazi cha nne cha mpata laana).

Laana yaweza kuwa ni adhabu nyingi hata pamoja na kuwa na maisha mafupi hapa duniani.(kifo).

Kuna sheria nyingi za ulimwengu wa kiroho wanasiasa hawazijui ama wanadharau...ulimwengu huu unataliwawa kwa sheria...

Mwacheni aendelee kukiuka kiapo chake...ataona mwisho wake !!
 
No, ni kwasababu, hata kabla naniliu, hajananiliu, kulizuka minong'ono mingi kuhusu hali ya afya ya naniliu, na kwamba alikuwa hoi bin taaban, katika kujaribu kuokoa maisha yake, akakimbizwa kule naniliu, ikashindikana, ndio akananiliu akiwa kule, ikaonekana itakuwa ni aibu dunia ikijulishwa naniliu ali naniliu kule kwa ugonjwa wa naniliu, sasa kwa vile taifa lilishatangaziwa rasmi, alinaniliu tarehe fulani kwa ugonjwa wa naniliu, ukitoa sababu nyingine yoyote, au tarehe rasmi ya kunaniliu, utakuwa umemfanya naniliu naye, aonekane muongo, hivyo bora kuendelea kuamini kile tuu tulichotangaziwa rasmi.
P
Kabisa Mkuu saa zingine inabidi kunaniliu ili tuendelee kunaniliu pasipo kuleta misigano na kina naniliu... ila "karma" haitawaacha wanaovichezea viapo kwa maana imeandikwa "...na wala msiape! Msiape kwa uongo! Msiape viapo kwa upuuzi!! Ole wao waapao..." hadi hapo uzito wa kuapa uko wazi...
 
Mbowe aliapa kanisani wakati wa kufunga ndoa kuwa atakuwa na mke mmoja tu na hatakuwa na wengine

Joyce MUKYA vipi? Mbowe ilikuwaje tena akawa na Joyce Mukya? kiapo cha bungeni na kanisani kipi kikubwa?

Mbowe anamudhihaki Mungu au?

Usihukumu usije ukahukumiwa

Usipende kutajataja watu na mahusiano yao ya faragha. Ni utoto.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom